Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Ukisikia ninapofikia hata pointi ya kuikana hii NCHI ndio hapa! Upuuuzi upuuuzi upuuzi! Hivi jamani kwani ni baadhi ya watanzania tumeishiwa kufikiria????
 
Kipindi Speaker Samuel Sitta anatuhumiwa na matumizi ya fedha nyingi kwa ajili ya matibabu MBONA HAWAKUSEMA KITU yule mzee si mzee wao wa tabora tena ni speaker wa bunge.............hawa ndiyo viongozi wetu wa kesho.....halafu watu wakikana utanzania wao mnakasirika....
 
Kapuya amekwishakuwa waziri wa kazi na yeye ndie mwenye kupendekeza kwa Rais nani awe Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF na kama waziri huteua wajumbe wa bodi!! Kwa taarifa tu akiwa waziri mwenye dhamana, alimpetekeza Siraju Juma Kaboyonga akawa mwenyekiti wa NSSF wakati Manji anakomba fedha za wafanyakazi. Na kaboyonga sasa ni mbunge wa Tabora mjini anayewatetea mafisadi bungeni[ Mtetezi wa kampuni iliyokodisha reli RITES na mmoja wa wapinzani wakuu wa hoja za DR. Slaa]. GT kwahiyo Kapuya anaproxies!!
QUOTE=Field Marshall ES;436819]2. Kapuya - A. (alisaidia kumfunga Rage, asigombee ubunge jimbo la jirani yake Kapuya & Patners kwenye migodi).

FMES![/QUOTE]

Bulesi, asante kwa hilo hapo juu. Nafikiri mnaona jinsi Tabora ulivyo mkoa wa ovyo.
Nilishawahi sema mara nyingi kuwa Jamani, Tabora bado tuko mwaka 1970 wakati Tabora Jazz wanaimba " Muumba, dua tunakuomba pokea...tukae kwa usalama..." Hilo tu ndiyo kwetu muhimu na zaidi ya hapo wala hatuhitaji zaidi.

Tabora/Sikonge ni mkoa masikini sana kimaisha na kifikra. Ndiyo maana utashangaa hata uchaguzi ujao, Kikwete atashinda kwa kishindo Tabora maana huko huhitaji hela nyingi kupigiwa debe. Huyo Rage mwenyewe nilishangaa Wapambe wanavyomgombania hadi kwenye ndege. Kila sehemu wanasubiri tu yeye anunue na wao ni watumiaji na wakitoka hapo ahhh, jamaa ni kusifiwa tu.

Tabora mjini penyewe hata internet ni za shida. Sasa huku wilayani ni hadi uwe na notebook/mtandao na hapo ukichanganya na tatizo la umeme, basi ni choka mbaya.
Ngoja niweke tena picha za vijiji vyetu ili mmpate hali halisi ya maisha ya kule na jinsi Tumbaku inavyomaliza misitu na watu. Watu wamechoka hadi Moravian church wanaomba wenye pesa zao waki-adopt kijiji. Sasa akija Mengi au RA/Manji, wao hawana maneno na kwao huyo ni mwokozi.

Ila kwa Tabora uongo mbaya, ka-Uarabu kametufikisha tulipo. Angalia picha hapa chini kwenye hii site:- Album * Moravian Board of World Mission

NB: Katika hizo picha, jamani kuna za kijiji changu ila kwa kuwa hapa tunaficha majina, sintasema wapi maana itakuwa rahisi kunipata. Hapa ni mtu pekee mwenye mtandao ila kwa wilaya ya Sikonge, basi tupo wengi. Hizo picha ni za kweli na sehemu nyingi/watu wengi nawafahamu humo ndani.
 
Last edited:
Mtumikie kafiri........................................These poor sods are only doing their jobs waliyotumwa na 'mfadhili' and they are doing so kwa njaa zao, njaa mbaya jamani!
 
UV-CCM!! Siamini kabisa! Lakina lazima wafanye hivyo. Tanil Somaiya juzi juzi kawapa shs 400 milioni kufadhili uchaguzi wa Taifa ni lazima walipe fadhila. Mbona Dr. Slaa alimtuhumu Rostam Aziz pale Mwembe Yanga 2007 na hawakubweka kama safari hii. Jamani tukisema kwamba CCM imetekwa na matajiri watu watuamini. UV-CCM walikuwa wapi wakati Dr. Salum Ahmed Salum anabaguliwa kwa rangi yake katika mchakato wa Urais ndani ya CCM 2005? Leo hii kwa kuwa watu 5 katika kundi la raia wengi wametajwa kwa vitendo vyao vya ovyo ovyo ndio UV-CCM imeona Mengi ni mbaguzi? Mbona hawakulaani ubaguzi dhidi ya Dr. Salim? Mwizi ni mwizi hata akiwa rangi gani au wangapi tukiwashuku lazima tuwaseme kwa nguvu bila kujali rangi au jinsia. UV-CCM ziiii!!
 
Kipindi Speaker Samuel Sitta anatuhumiwa na matumizi ya fedha nyingi kwa ajili ya matibabu MBONA HAWAKUSEMA KITU yule mzee si mzee wao wa tabora tena ni speaker wa bunge.............hawa ndiyo viongozi wetu wa kesho.....halafu watu wakikana utanzania wao mnakasirika....

Sitta ana vijisenti vya kuwalipa? Pesa ni kitu cha hatari. Nadhani kati maadui wtu 4 wa zamani tuongeze adui mwingine ambaye ni PESA za kifisadi!
 
Jamani ehh, msieleze vitu vigumu sana juu ya hawa vijana. Hawa hawajui hata mchezo gani unaendelea. Tungelisema kuwa, bado wanasubiri washushe bendera ya TANU na kuweka ya CCM. Ukiwauliza walikuwa wapi watakuambia walukuwa busy wakichoma tumbaku na kuvuta bangi. Usiku walikuwa wanaongeza nyumba ndogo maana hawa wakirudi kesho huko Sikonge, wanaonwa kama miungu fulani hivi.

Ni sawa na rais wa Africa na Mkewe wanaenda Ulaya kuomba misaada na mke wa Rais wa Africa kavaa pamba kali kumzidi mke wa Rais mtoa misaada...🙂 Ila sisi pia wa Tabora tuna ushamba wetu na njaa yetu vilevile.

Labda la muhimu kujiuliza na kupanga ni JINSI YA KUWAAMSHA NDUGU ZANGU HAWA.
 
Chadema yawashukia wanaompinga Mengi

2009-04-30 16:58:54
Na Muhibu Said

Chama Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimewabeza baadhi ya viongozi wa serikali na vyama vya siasa wanaomjadili Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, kwa kuwataja wanaotuhumiwa kwa ufisadi mkubwa nchini.

Kimesema hatua ya viongozi hao inashangaza kwa vile watu hao, ambao Mengi alisema kuwa wanatuhumiwa kuwa ni `mafisadi papa`, si wapya kutajwa kuhusika na tuhuma zinazohusu ufisadi nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Chadema, jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Masuala ya Bunge wa Chama hicho, John Mrema alisema baadhi ya watuhumiwa hao, walianza kutajwa kuhusika na tuhuma za ufisadi tangu mwaka 1992, lakini hadi sasa hakuna hatua zozote zilizokwishachukuliwa dhidi yao.

Mrema alisema mwaka 1992, Tume iliyoongozwa na Robert Aila kuchunguza kashfa ya Chavda, ilimtaja Shubash Patel kuhusika na kashfa hiyo, pia Tanil Somaiya, miaka michache iliyopita alitajwa kuchunguzwa katika kashfa ya ununuzi wa rada ya serikali, lakini hadi sasa wote hawajachukuliwa hatua.

Alisema watuhumiwa wengine, ni Yusufu Manji, ambaye miaka michache iliyopita, alituhumiwa kuhusika na ufisadi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Rostam Aziz alitajwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa kupitia ushirikiano wa vyama vya upinzani Septemba 15, 2007 kuwamo katika orodha ya watuhumiwa 11 wa ufisadi nchini.

``Sasa ni lipi lake (Mengi) jipya? Sisi (Chadema) tuko pamoja na Mengi, tunataka mafisadi wote na si mapapa peke yao washughulikiwe. Tunajua CCM wananufaika vipi na watu hawa,`` alisema Mrema.

Kutokana na hali hiyo, alimtaka Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba aueleze umma kwanza alikopata fedha za kampeni ya uchaguzi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kabla ya kumjadili Mengi kuhusu suala hilo.

Pia, alisema ameshangazwa na kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye huko nyuma aliwahi `kuushikia bango` ununuzi wa rada kwa madai kwamba, ndani yake kuna harufu ya rushwa, lakini leo anadai watu hao hawakukosea.

Katika hatua nyingine, Chadema jana ilitoa tamko kushutumu hatua ya baadhi ya vyombo, watu, wakiwamo wabunge kutaka kumshughulikia Dk. Slaa kwa kutaja hadharani mshahara anaopokea bungeni.

Akisoma tamko hilo jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Victor Kimesera, pamoja na mambo mengine alitaka iundwe kamati maalum ya kudumu ya kupanga na kuratibu mishahara ya wabunge badala ya kuacha suala hilo kupangwa na wabunge wenyewe.

SOURCE: NIPASHE
 
Labda la muhimu kujiuliza na kupanga ni JINSI YA KUWAAMSHA NDUGU ZANGU HAWA

Hao wameshindikana dawa yao nikuwapiga Polonium, na kuanza upya! na kizazi kipya
 
hawa ndio vijana wanaoandaliwa na ccm kuwa viongozi wa kesho. Nadhani hiyo kesho yao itakuwa mbaya sana kuliko leo
 
Hivi mengi anawagaia fedha kama alivyotoa kwa CCM kuwasaidia katika shughuli zao za kuangamiza upinzani ? Mengi amewataja mafisadi na kuwawacha wengine kama haitoshi amempongeza Raisi Kikwete ,sasa mnataka Chadema tuwaelewe kuwa mpo pamoja na Mengi kuhusiana na msimamo wake ? Mkiambiwa kuwa Chadema ni mamluki wa CCM mnapiga makelele .
 
Safi sana CHADEMA. Tutafika tu, kwani siyo Watanzania wote wako kwenye payroll ya RA na washikaji wake!
 
Pia, alisema ameshangazwa na kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye huko nyuma aliwahi `kuushikia bango` ununuzi wa rada kwa madai kwamba, ndani yake kuna harufu ya rushwa, lakini leo anadai watu hao hawakukosea.

Prof Lipumba hakuwa na kumbukumbu hiyo ya rada, alichotaka ni yeye kusikika akizungumzia swala hilo bila ya kujali atazungumza kitu gani.
 
Mrema wa Chadema anasema kuwa wana CCM wananufaika na hao mafisadi.kwani Chadema nao hawanufaiki na Mengi?

Mengi ndio mfadhili wa helkopta za Chadema unategemea watamsema vibaya?
kwenye ununuzi Ndege ya rais na rada kuna wafanyabiashara wazalendo toka mkoa wa kilimanjaro wanahusika na MENGI anawajua lakini hawajatajwa.
hapa kila upande unatizama maslahi yake.kama vijana wa UVCCM walivyotoa tamko kumsafisha RA na chadema nao wanamsafisha mfadhili wao.
 
Soma vizuri kauli ya Mrema ndio ujadili sio kukurupuka
 
Mnataka kuchezea mkate wao wa kila siku! thubutu. Yaani Rostam ndio shibe ya Familia yao na lazima wabwatuke. Najaribu kukumbuka enzi za ukoloni au katika ile picha ya SARAFINA pale jamaa yule mswahili akiwa anajipendekeza kwa wazungu lakini zake zilipotimia walimshikisha adabu. Acha bwana njaa si mchezo, hawa jamaa bila Rostam hawashibi.

Lakini kuna siku yatafika mwisho. Moto aliouwasha Mengi umeanza kuunguza na hapa tutamjua nani ni nani
 
Hivi mengi anawagaia fedha kama alivyotoa kwa CCM kuwasaidia katika shughuli zao za kuangamiza upinzani ? Mengi amewataja mafisadi na kuwawacha wengine kama haitoshi amempongeza Raisi Kikwete ,sasa mnataka Chadema tuwaelewe kuwa mpo pamoja na Mengi kuhusiana na msimamo wake ? Mkiambiwa kuwa Chadema ni mamluki wa CCM mnapiga makelele .
Patamuu mkuuu...

kuna jambo laja......
 
Du kazi kwelikweli, kumbe ndo maana walisema akili ni nywele
 
Back
Top Bottom