Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Kwa nini wewe unaamini kuwa kuna baba zao? inawezekana hawa ndio mababa labda kama unataka Mengi e-expand list yake.
Haujaelewa swali langu..kwanini ukiwa baba hauwezi kuwa na baba?yes kuna mbaba zao awataje basi..mie kuna kitu anchoogopa..

kuwataja tu wenye asili moja ndilo tatzio langu la kwanza

2.Amekuwa na ugomvi na hawa watu kwa muda mrefu
 
tamko la umoja wa vijana wa ccm mkoa wa tabora

ndg wanahabari,
waheshimiwa ndugu waandishi tunashukuru sana kwa kujitokeza siku ya leo kuja kutusikiliza, tunaomba muendelee na moyo huo kutumikia jamii kwa kutoa habari za uhakika zenye tija na taifa letu.mungu awabariki sana kwa hilo.

Tungependa kwanza kutumia fursa hii kuwapa pole wakazi wa jiji la dar es salaam, hasa maeneo ya mbagala na maeneo yote kwa ujumla kwa tukio la jana la milipuko ya mabomu, na kuwapa pole majeruhi wote walioathirika na tukio hilo, na pia kuwapa pole familia zote waliofiwa na ndg zao kutokana na tukio hilo, mungu azilaze pema peponi roho zao, na tunawaombea majeruhi wapone haraka.

Tuliopo hapa mbele yenu ni mwenyekiti uvccm mkoa, mjumbe wa baraza kuu taifa na wenyeviti wa uvccm wa wilaya zote za mkoa wa tabora, maana yake wilaya ya tabora mjini, nzega, sikonge, igunga, urambo,na uyui. Pia tunaye katibu wa uhamasishaji uvccm wa mkoa wa tabora. Tumekuja hapa dar-es-salaam tangu juzi kwa ajili ya kufuatilia maandalizi ya fundraising kwa ajili ya miradi ya vijana wa mkoa wa tabora, na tunaomba tuwahakikishie vijana wenzetu kwamba mipango inaendelea vizuri sana, na inshaalah mungu akijalia, maandalizi yatakuwa yamekamilika wakati tunarejea tabora.

Aidha tumeamua kuongelea kauli ya mfanyabiashara wa ipp, ndugu reginald mengi aliitisha vyombo vyake vya habari na kuanza kutukana na kuhukumu watanzania wenzake, ni kauli ambazo hazivumiliki kwa mtu aliyestaarabika kutuhumu watu kwa maslahi binafsi na anyoyafahamu mwenyewe bila kufata misingi ya sheria.

Kauli hizo licha ya kuleta harufu ya ubaguzi wa rangi pia inakuza chuki ya raia dhidi ya wenzao kwa mtazamo kuwa umasikini wao unakuzwa na kundi la watu kwa manufaa yao. Aidha linatoa taswira kuwa serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake kwa kiwango cha kuwaruhusu baadhi ya watu kuharibu nchi, jambo ambalo lina lengo la kuigombanisha serikali na wananchi wake.

Bila kujali utawala wa sheria na haki ya msingi ya binadamu, tunaamini kila mtanzania anayo haki sawa kabisa. Tunapenda kuishukuru na kuipongeza sana serikali kupitia waziri wa utawala bora na waziri wa habari kwa kukemea kitendo hicho na kuendelea kusisitiza taifa lenye utawala wa sheria.

Kilichotusukuma sisi leo kama vijana wa ccm wa mkoa wa tabora ni jinsi ambavyo ndugu mengi alimtaja mjumbe wa kamati kuu ya ccm - mhe rostam aziz, ambaye vilevile ni mbunge wa igunga. Wadhifa nyigine ambazo amewahi kushika ni pamoja na mweka hazina wa ccm taifa, pia kwa sasa ni mjumbe wa nec kupitia mkoa wetu wa tabora na kamanda wa uvccm wilaya ya igunga, maana yake ni kada kwelikweli wa ccm na nyumbani kwao ni mkoa wa tabora, tukaona hili haliwezi kupita bila sisi kama vijana kuja kutetea chama chetu. Kazi kubwa ya umoja wa vijana ni kutetea uhai wa ccm na viongozi wake pale tunapo amini kuwa wanasimamia maslahi ya taifa.

Hivi karibuni kumetokea hali ya mabadiliko ktk mfumo/tabia yetu ya kutoa mawazo kama wananchi wa jamhuri ya muungano wa tanzania.
Ikiwa ni haki ya mtu kutoa mawazo, ni haki iliyoainishwa katika katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania, lakini haki hiyo inapotumiwa vibaya kwa maslahi binafsi, na kwa nia ya kuwachafua wengine haki hii hugeuka kuwa vurugu na vurugu hizi zinaweza kupelekea hata machafuko kwa kupandikiza chuki miongoni mwa jamii yetu.

Ndg wanahabari, baada ya utangulizi hapo juu, sisi kama viongozi wa uvccm wa wilaya zote na mkoa wa tabora na kwa niaba ya uvccm (m) tabora, tunaomba kusema yafuatayo:

1. Tunalaani kauli kuwa mh rostam aziz, kama kiongozi wetu na kamanda wa umoja wa vijana wilaya ya igunga kudhalilishwa hadharani na mtu bila kuleta ushahidi wowote, tunamtaka mzee reginald mengi atuombe radhi wana ccm wa mkoa wa tabora kwa kumtuhumu kiongozi wetu ambaye wananchi wake wana imani naye sanjali na wana tabora, na amechaguliwa kidemokrasia na wananchi wengi tu. Tukiacha kauli yake bila kukemea maana yake tumekubaliana, jambo ambalo siyo kweli na kazi zake katika mkoa wa tabora na wilaya ya igunga ni ushahidi tosha.

2. Tunalaani matamshi ya ndugu reginald mengi dhidi ya raia wenzake, na tunahoji nafasi ya ndugu mengi kwenye jamii mpaka achukuwe nafasi ya kutuhumu, kuchunguza na kuhukumu. Raia yoyote wa tanzania mwenye nia njema anaruhusiwa kisheria kupeleka ushahidi au kushitaki na kufungua kesi dhidi ya yeyote anayehujumu taifa, kama kweli anayosema kwanini asiende mahakamani kuwafungulia kesi watu hawa na kuishtaki kwa maslahi ya nchi. Tunaomba serikali kama ambavyo mhe mkuchika amesema, kuchunguza kauli za ndugu mengi na kumchukulia hatua kali zakisheria ili watu waheshimu utawala wa sheria nchini.

3. Tunahoji nafasi yake ni nini kwenye ccm? Na kwanini anatumia majukwaa ya ccm kutukana viongozi kama anavyojisikia,na kutamka kuwa wateule wa rais ni wezi. Ndugu mengi anayo historia ya kulumbana tena kwa kashfa na mawaziri wengi nchini, tunamtaka aache mara moja na kama anataka siasa aingie kwenye ulingo wa siasa na tutakuna nae kwenye majukwaa ya kisiasa

4. Tunaiomba serikali iangalie upya sheria na matumizi haya mabaya ya vyombo vya habari ambayo yanaweza kuleta mtikisiko mkubwa kwenye nchi, mgawanyiko na serikali iweze kupiga marufuku tabia hii ya bwana mengi kutumia umaskini wa watanzania kupandikizia chuki watu wengine.

5. Tumefuatilia kwa karibu mwenendo na ziara za ndugu mengi akiwa na msafara wa wabunge huku akitoa misaada mbali mbali, na tumepata taarifa kwamba anakuja katika wilaya ya mkoa wa tabora, uvccm mkoa wa tabora inatoa angalizo ikiwa kama misaada yake inaendana na tabia ya kutukana na kuwaundia majina mabaya viongozi wetu wa chama, tunamuonya kama vijana wa tabora na kamwe hatutavumilia jambo hili. Wananchi wa tabora wana matatizo mengi, lakini vilevile wanaheshimu utu na kamwe hatuwezi kukubali matatizo yetu yatumike kudhalilishwa utu wetu na wa viongozi wetu tuliowachagua kidemokrasia.

6. Uvccm tunamuunga mkono mnec wa mkoa wa tabora mh rostam aziz(mb) na kuwaambia watanzania kuwa mkoa wa tabora tuna imani naye na hatuna shaka juu ya uzalendo wake kwa taifa hili tunafahamu anafanya biashara zake halali na hajawahi kushtakiwa na serikali kuwa amekwepa kodi zozote anazotakiwa kulipa na kwa hili uzalendo wake hauna shaka , na kumtaka asivunjike moyo, hizi ni kelele za watu wenye nia mbaya na tunamuahidi tutakuwa naye bega kwa bega katika kipindi hiki na hatutaruhusu kauli chafu dhidi ya kiongozi wetu. Tunathamini sana mchango wake wa muda mrefu kwa chama cha mapinduzi na maendeleo anayohangaika nao kwa wananchi wa jimbo la igunga na mkoa wa tabora kwa ujumla.

7. Uvccm mkoa wa tabora, tunatoa angalizo kwa watanzania wenzetu kuwa tusiruhusu ukaburu kutuingia kwa mtu kuja na hoja ya ubaguzi ili kuwajengea chuki watanzania . Tabia hii baba wa taifa aliwahi kuikemea na kuifananisha na ukaburu tusiruhusu makaburu kuibuka katika nchi yetu.

8. Uvccm mkoa wa tabora, tunakemea na tunashauri chama cha mapinduzi kuchukua hatua kurudisha nidhamu ndani ya chama na serikali kwani ccm ndiyo chama tegemeo. Kwani hivi sasa kuna kashfa, malumbano ambayo hayasaidii nchi na kutoruhusu mijadala ambayo itatuyumbisha kama taifa, tabia ya aina hii si jambo zuri bali ni hatari kwa mustakabali wa nchi yetu.

9. Mwisho tunapenda kuwahakikishia wanahabari na watanzania kwa ujumla uvccm mkoa wa tabora tunamuunga mkono mnec wetu na hatuko tayari kuona anadhalilishwa bila kuwa ushahidi wa jambo lolote na imani serikali haitaruhusu tabia ya watu kujitafutia umaarufu kwa gharama za kuchafua wengine.

10. Uvccm mkoa tunatoa angalizo kwa wabunge wa majimbo yote ya mkoa wa tabora ,na wa viti maalum kuwa wakasimamie utekelezaji wa ilani ya ccm kama walivyoahidi kwa wapiga kura, pia tunatoa wito kwa wabunge wa mkoa wetu wanaoambatana na misafara ya bwana mengi wajiepushe na misafara inayokashifu na kuita majina mabaya viongozi wetu na wao kuwa sehemu ya jambo hilo wakishangilia. Kwa kuwa mwenyekiti wa makampuni ya ipp ana tabia ya kutumia majukwaa ya ccm na kukashifu watendaji wakuu wa serikali na wakati huo huo kumsifia rais kwani huwezi kumsifia rais wakati unakashifu na kuwaita watendaji wake wa chama na serikali kuwa ni mafisadi na hawamsaidii rais kimantiki ni kwamba anakosoa uteuzi wa rais na kuonyesha kuwa unamapungufu. Vijana hatutakuwa tayari kubeba wabunge 2010 wanaoshiriki katika ziara ambazo zinakichafua chama na serekali kupitia kivuli cha kusaidia wanyonge.

11. Tunasisitiza tunalaani kauli ya mengi na tunaomba serekali itekeleze alichosema mh mkuchika.

Ahsanteni sana, mungu awabariki

kidumu chama cha mapinduzi







yah kitadumu chama mafisadi na hakiwezi kudumu bila rostam azizi,
 
He he he!

Huyu mama alikurupuka kuwasafisha mapapa. Tuone sasa akijiokoa.

Pinda kasema bungeni kwamba mambo mengine watu wasikurupuke!!!! Tena baada ya kusema kwamba Mengi hakukosea!
 
Hapa naanza kupata wasiwasi na uadilifu wa CCM na hawa umoja wa vijana wake kutoka Tabora hivi siku zote hizi ndo kwanza leo wanamjua kama Mengi mbaguzi? kwa kuwa tu katajwa mtu wa na wenzake, siku zile vyombo vyake vya habari vikiwatukana WAPEMBA na kuwaita "magaidi" walikuwa kimyaa.
 
Hawa hapa.....Beni na Msanii (1995)
jkmkapa.jpg
 
Last edited:
Nataka Kumjua baba wa Mafisadi,Nani anawalea mafisadi?

Mie nimeona sasa Mengi ameenda mbali sana,Katumia Vyombo vyake vya habari vibaya sana na mpaka sasa nashindwa kuelewa ni kwanini Jukwaa la Habari limekaa kimya kuhusiana na habari hii.Tukiachia mambo kama haya siku mtu anweza kuamua kuwatangazia UMMA mambo ya ajbu ajabu tu!

Kama anajua Kila "flani" ni mapapa basi atuambie baba yao ni nani?hauwezi kuwa papa kama haujazaliwa na papa,na hauwezi kuishi kwa ujanja tu bila ya kulelewa na PAPA.Kwa maana nyingine aseme tu kuwa Na "flani" ni papa,awaorodheshe!

Inawezekana Mengi anawaju wazazi wa hawa Mapapa,ila kwa suala hili la kuchonga juzi mie nasema mzee amechemka,na maejenga chuki kati ya watu na pia ameleta "Ukaburu"!

Kama asipotaja baba wa Mapapa,anayawealea mapapa mie nitandelea na msimamo wangu kuwa Mengi ameamua kuwachafua kina RA na wenzake!

Tabia ya mtu kutaka Sympathy kwa wanachi imepitwa na wakati,

Yes,Mengi najua unaweza kuwataja wazazi wa hao mapapa.Come on do it Now!

Mkuu heshima mbele

Mimi nafikiri hapa cha kuhoji ni kwanini mengi amewataja hao waliotajwa? Pili naona kama nchi ipo ipo mtu anataja kwamba kuna Mafisadi na wala haulizwi kwa maana ya kutoa ushahidi. Kutoa ushahidi kwa Mengi ndio kutafungua milango ya ufisadi wote. Wananchi hatujajua tuu kwamba Mengi anaweza akawa amefungua njia kwa namna moja ama nyingine kumaliza hili tatizo ambalo wengi tunaona kama ni sugu la UFISADI.

Ila sasa cha msingi lazima watajwa waweze kujitokeza na kutetea usafi wao dhidi ya tuhuma za bwana Mengi unless otherwise Maneno ya Bw Mengi yana ukweli 100%
 
Jamani ehh, msieleze vitu vigumu sana juu ya hawa vijana. Hawa hawajui hata mchezo gani unaendelea. Tungelisema kuwa, bado wanasubiri washushe bendera ya TANU na kuweka ya CCM. Ukiwauliza walikuwa wapi watakuambia walukuwa busy wakichoma tumbaku na kuvuta bangi. Usiku walikuwa wanaongeza nyumba ndogo maana hawa wakirudi kesho huko Sikonge, wanaonwa kama miungu fulani hivi.

Ni sawa na rais wa Africa na Mkewe wanaenda Ulaya kuomba misaada na mke wa Rais wa Africa kavaa pamba kali kumzidi mke wa Rais mtoa misaada...🙂 Ila sisi pia wa Tabora tuna ushamba wetu na njaa yetu vilevile.

Labda la muhimu kujiuliza na kupanga ni JINSI YA KUWAAMSHA NDUGU ZANGU HAWA.
Pole sana mpambanaji,tatizo umaskini unaouona Tabora hauko huko tu ni sehemu nyingi.Kinachosumbua kwa watanzania wengi ni fikra tegemezi hawawezi kusimamia hoja zao wenyewe.Ni bahati mbaya Rais wa kwanza alikuwa msomi na akili nyingi na alioongoza kwa mda mrefu.Hivyo fikra za watanzania wengi ukishakuwa kiongozi wao fikra zao zinawatuma kuwa una uwezo wa kufikiri kuliko wao na kuangukia kila wakati kusubiri maagizo ya watawala wao.
Juhudi ya kuanzisha wazo na walisimamie wenyewe hawana,Mwalimu aliwadekeza kufikiri kwa niaba yao.Nashukuru sana Mwanakijiji anahangaika kuwatoa kutoka huko kwamba mungu aliwapa mwalimu tu na hatoi mara mbili.Nakumbuka hotuba ya kihistoria aliyotoa Mbeya siku ya mei mosi watawala wetu hawataki kuirudia.Na wamehakikisha electronic media hairudii hotuba ile wakihofia wananchi wasielewe namna ya kutafuta viongozi bora.
 
Tamko la Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Tabora

Ndg wanahabari,
Waheshimiwa ndugu waandishi tunashukuru sana kwa kujitokeza siku ya leo kuja kutusikiliza, tunaomba muendelee na moyo huo kutumikia jamii kwa kutoa habari za uhakika zenye tija na taifa letu.Mungu awabariki sana kwa hilo.

Tungependa kwanza kutumia fursa hii kuwapa pole wakazi wa Jiji la Dar es salaam, hasa maeneo ya Mbagala na Maeneo yote kwa Ujumla kwa tukio la jana la milipuko ya mabomu, na kuwapa pole majeruhi wote walioathirika na tukio hilo, na pia kuwapa pole familia zote waliofiwa na ndg zao kutokana na tukio hilo, mungu azilaze pema peponi roho zao, na tunawaombea majeruhi wapone haraka.

Tuliopo hapa mbele yenu ni Mwenyekiti UVCCM Mkoa, Mjumbe wa Baraza kuu Taifa na wenyeviti wa UVCCM wa wilaya zote za mkoa wa tabora, maana yake wilaya ya tabora mjini, Nzega, Sikonge, Igunga, Urambo,na Uyui. Pia tunaye katibu wa Uhamasishaji Uvccm wa Mkoa wa Tabora. Tumekuja hapa Dar-es-Salaam tangu juzi kwa ajili ya kufuatilia maandalizi ya fundraising kwa ajili ya miradi ya vijana wa mkoa wa Tabora, na tunaomba tuwahakikishie vijana wenzetu kwamba mipango inaendelea vizuri sana, na inshaalah mungu akijalia, maandalizi yatakuwa yamekamilika wakati tunarejea Tabora.

Aidha tumeamua kuongelea kauli ya Mfanyabiashara wa IPP, Ndugu Reginald Mengi aliitisha vyombo vyake vya habari na kuanza kutukana na kuhukumu watanzania wenzake, ni kauli ambazo hazivumiliki kwa mtu aliyestaarabika kutuhumu watu kwa maslahi binafsi na anyoyafahamu mwenyewe bila kufata misingi ya sheria.

Kauli hizo licha ya kuleta harufu ya ubaguzi wa rangi pia inakuza chuki ya raia dhidi ya wenzao kwa mtazamo kuwa umasikini wao unakuzwa na kundi la watu kwa manufaa yao. Aidha linatoa taswira kuwa serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake kwa kiwango cha kuwaruhusu baadhi ya watu kuharibu nchi, jambo ambalo lina lengo la kuigombanisha serikali na wananchi wake.

Bila kujali utawala wa sheria na haki ya msingi ya binadamu, tunaamini kila mtanzania anayo haki sawa kabisa. Tunapenda kuishukuru na kuipongeza sana Serikali kupitia Waziri wa Utawala Bora na Waziri wa Habari kwa kukemea kitendo hicho na kuendelea kusisitiza Taifa lenye utawala wa Sheria.

Kilichotusukuma sisi leo kama Vijana wa CCM wa mkoa wa Tabora ni jinsi ambavyo Ndugu Mengi alimtaja mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM - Mhe Rostam Aziz, ambaye vilevile ni Mbunge wa Igunga. Wadhifa nyigine ambazo amewahi kushika ni pamoja na Mweka Hazina wa CCM Taifa, pia kwa sasa ni Mjumbe wa NEC kupitia mkoa wetu wa Tabora na Kamanda wa UVCCM wilaya ya Igunga, maana yake ni KADA kwelikweli wa CCM na nyumbani kwao ni Mkoa wa Tabora, tukaona hili haliwezi kupita bila sisi kama vijana kuja kutetea Chama chetu. Kazi kubwa ya Umoja wa Vijana ni kutetea uhai wa CCM na Viongozi wake pale tunapo amini kuwa wanasimamia maslahi ya Taifa.

Hivi karibuni kumetokea hali ya mabadiliko ktk mfumo/tabia yetu ya kutoa mawazo kama wananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Ikiwa ni haki ya mtu kutoa mawazo, ni haki iliyoainishwa katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini haki hiyo inapotumiwa vibaya kwa maslahi binafsi, na kwa nia ya kuwachafua wengine haki hii hugeuka kuwa vurugu na vurugu hizi zinaweza kupelekea hata machafuko kwa kupandikiza chuki miongoni mwa jamii yetu.

Ndg wanahabari, baada ya utangulizi hapo juu, sisi kama viongozi wa UVCCM wa wilaya zote na mkoa wa Tabora na kwa niaba ya UVCCM (M) Tabora, tunaomba kusema yafuatayo:

1. Tunalaani kauli kuwa Mh Rostam Aziz, kama kiongozi wetu na kamanda wa Umoja wa Vijana wilaya ya Igunga kudhalilishwa hadharani na mtu bila kuleta ushahidi wowote, tunamtaka Mzee Reginald Mengi atuombe radhi wana CCM wa mkoa wa tabora kwa kumtuhumu kiongozi wetu ambaye wananchi wake wana imani naye sanjali na wana Tabora, na amechaguliwa kidemokrasia na wananchi wengi tu. Tukiacha kauli yake bila kukemea maana yake tumekubaliana, jambo ambalo siyo kweli na kazi zake katika mkoa wa Tabora na wilaya ya igunga ni ushahidi tosha.

2. Tunalaani matamshi ya Ndugu Reginald Mengi dhidi ya Raia wenzake, na tunahoji nafasi ya ndugu Mengi kwenye jamii mpaka achukuwe nafasi ya kutuhumu, kuchunguza na kuhukumu. Raia yoyote wa Tanzania mwenye nia njema anaruhusiwa kisheria kupeleka ushahidi au kushitaki na kufungua kesi dhidi ya yeyote anayehujumu Taifa, kama kweli anayosema kwanini asiende mahakamani kuwafungulia kesi watu hawa na kuishtaki kwa maslahi ya Nchi. Tunaomba serikali kama ambavyo Mhe Mkuchika amesema, kuchunguza kauli za Ndugu Mengi na kumchukulia hatua kali zakisheria ili watu waheshimu utawala wa sheria nchini.

3. Tunahoji nafasi yake ni nini kwenye CCM? Na kwanini anatumia majukwaa ya CCM kutukana viongozi kama anavyojisikia,na kutamka kuwa wateule wa Rais ni wezi. Ndugu Mengi anayo historia ya kulumbana tena kwa kashfa na Mawaziri wengi nchini, tunamtaka aache mara moja na kama anataka siasa aingie kwenye ulingo wa siasa na tutakuna nae kwenye majukwaa ya kisiasa

4. Tunaiomba serikali iangalie upya sheria na matumizi haya mabaya ya vyombo vya habari ambayo yanaweza kuleta mtikisiko mkubwa kwenye nchi, mgawanyiko na serikali iweze kupiga marufuku tabia hii ya Bwana Mengi kutumia umaskini wa watanzania kupandikizia chuki watu wengine.

5. Tumefuatilia kwa karibu mwenendo na Ziara za Ndugu Mengi akiwa na Msafara wa Wabunge huku akitoa Misaada Mbali mbali, na tumepata taarifa kwamba anakuja katika wilaya ya Mkoa wa Tabora, Uvccm Mkoa wa Tabora inatoa Angalizo ikiwa kama misaada yake inaendana na tabia ya kutukana na kuwaundia majina mabaya viongozi wetu wa Chama, tunamuonya kama vijana wa Tabora na kamwe hatutavumilia jambo hili. Wananchi wa Tabora wana matatizo mengi, lakini vilevile wanaheshimu utu na kamwe hatuwezi kukubali matatizo yetu yatumike kudhalilishwa utu wetu na wa viongozi wetu tuliowachagua kidemokrasia.

6. UVCCM tunamuunga mkono MNEC wa Mkoa wa Tabora Mh Rostam Aziz(Mb) na kuwaambia Watanzania kuwa Mkoa wa Tabora tuna imani naye na hatuna shaka juu ya Uzalendo wake kwa Taifa hili tunafahamu anafanya biashara zake halali na hajawahi kushtakiwa na serikali kuwa amekwepa kodi zozote anazotakiwa kulipa na kwa hili uzalendo wake hauna shaka , na kumtaka asivunjike moyo, hizi ni kelele za watu wenye nia mbaya na tunamuahidi tutakuwa naye bega kwa bega katika kipindi hiki na hatutaruhusu kauli chafu dhidi ya kiongozi wetu. Tunathamini sana mchango wake wa muda mrefu kwa Chama Cha Mapinduzi na maendeleo anayohangaika nao kwa wananchi wa jimbo la igunga na mkoa wa tabora kwa ujumla.

7. Uvccm Mkoa wa Tabora, tunatoa angalizo kwa watanzania wenzetu kuwa Tusiruhusu UKABURU kutuingia kwa mtu kuja na hoja ya UBAGUZI ili kuwajengea chuki Watanzania . Tabia hii Baba wa Taifa aliwahi kuikemea na kuifananisha na ukaburu tusiruhusu makaburu kuibuka katika nchi yetu.

8. Uvccm mkoa wa Tabora, tunakemea na tunashauri Chama Cha Mapinduzi kuchukua hatua kurudisha nidhamu ndani ya chama na Serikali kwani CCM ndiyo chama tegemeo. Kwani hivi sasa kuna kashfa, malumbano ambayo hayasaidii nchi na kutoruhusu mijadala ambayo itatuyumbisha kama taifa, tabia ya aina hii si jambo zuri bali ni hatari kwa mustakabali wa nchi yetu.

9. Mwisho tunapenda kuwahakikishia wanahabari na watanzania kwa ujumla Uvccm mkoa wa tabora tunamuunga mkono MNEC wetu na hatuko tayari kuona anadhalilishwa bila kuwa ushahidi wa jambo lolote na imani serikali haitaruhusu tabia ya watu kujitafutia umaarufu kwa Gharama za kuchafua wengine.

10. Uvccm Mkoa tunatoa angalizo kwa Wabunge wa Majimbo yote ya mkoa wa Tabora ,na wa viti maalum kuwa wakasimamie utekelezaji wa Ilani ya CCM kama walivyoahidi kwa wapiga kura, pia tunatoa wito kwa wabunge wa Mkoa wetu wanaoambatana na Misafara ya Bwana Mengi wajiepushe na misafara inayokashifu na kuita majina mabaya viongozi wetu na wao kuwa sehemu ya jambo hilo wakishangilia. Kwa kuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP ana Tabia ya kutumia majukwaa ya CCM na kukashifu watendaji wakuu wa serikali na wakati huo huo kumsifia Rais kwani huwezi kumsifia Rais wakati unakashifu na kuwaita watendaji wake wa chama na Serikali kuwa ni Mafisadi na hawamsaidii Rais kimantiki ni kwamba anakosoa uteuzi wa Rais na kuonyesha kuwa unamapungufu. Vijana hatutakuwa tayari kubeba wabunge 2010 wanaoshiriki katika ziara ambazo zinakichafua chama na serekali kupitia kivuli cha kusaidia wanyonge.

11. Tunasisitiza tunalaani kauli ya Mengi na tunaomba serekali itekeleze alichosema Mh Mkuchika.

AHSANTENI SANA, MUNGU AWABARIKI

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Pathetic! Ni vijibwa tu, kazi kutumika na ulafi mbele
 
Kwa njaa yao vijana hawa wa Tabora naomba niwape laana mbili kuu ambazo ziwafikie na kuwaganda mpaka uchaguzi wa 2010


2. STATIC GLOBAL FINANCIAL CRISIS

Bei ya pamba imeshuka mpaka Tsh 150/Kg, Na iendeleeeeeee hivyo hivyo mpaka watakapokuwa na masikio na adabu wasukuma hawa, labda 2010 watajua kuwa kumbe maharage si chakula cha jela peke yake
icon8.gif

Kadu,

Hii laana haitupati siye Wanyamwezi. Naona uachanganya nsansa na nswalu. Wasukuma ni maana yake Wanyamwezi wa Kaskazini na siye Wanyamwezi wa Tabora wanatuita Wadakama. Wasukuma wanalima Pamba wakati sisi twalima tumbaku kwa wingi. Hivyo labda bei ya tumbaku ikishuka, tumelaaniwa.

Kama utakumbuka kuwa miaka ya 80 ilikuwa kichekesho kujenga kiwanda cha nyuzi Tabora wakati Pamba zatoka Mwanza/Shinyanga.

Mwisho niseme tena, kwa wananchi wa kawaida, hata hawaelewi nini kinaendelea. Ni watu ambao walitakiwa waseme "Hivi lini Sallum Abdallah atakuja Sikonge...?" Usiwaone wamevaa vizuri na vizimu vya mkononi, ushamba wao hadi unatisha.
 
jk - 1995


Mwanahabari una chuki na watu wengine siyo!Tutajie ni wkanini uwaone hawa wazee Mafisadi?acha mambo ya kizushi..Mie nimemuomba Mengi atutajie tu sababu yeye si ndiyo mtu wa kuhukumu watu na kuwapa makosa..

Mpaka sasa sijapata ushahidi wa kutosha kuwa Mkapa na JK ni Mafisadi,Hivyo napingana na Mawazo yako Mpaka nitakopothibitishiwa hivyo mahakamani!

Wanaweza kuwa na mapungufu yao katika utendaji ila bado sijafikia hatua ya kuwapaka Matope kiivyo ila wana matatizo yao na sikatai!
 
Kadu,

Hii laana haitupati siye Wanyamwezi. Naona uachanganya nsansa na nswalu. Wasukuma ni maana yake Wanyamwezi wa Kaskazini na siye Wanyamwezi wa Tabora wanatuita Wadakama. Wasukuma wanalima Pamba wakati sisi twalima tumbaku kwa wingi. Hivyo labda bei ya tumbaku ikishuka, tumelaaniwa.

Kama utakumbuka kuwa miaka ya 80 ilikuwa kichekesho kujenga kiwanda cha nyuzi Tabora wakati Pamba zatoka Mwanza/Shinyanga.

Mwisho niseme tena, kwa wananchi wa kawaida, hata hawaelewi nini kinaendelea. Ni watu ambao walitakiwa waseme "Hivi lini Sallum Abdallah atakuja Sikonge...?" Usiwaone wamevaa vizuri na vizimu vya mkononi, ushamba wao hadi unatisha.
Mkuu Sikonge,

Hao ndio wawakilishi wa Sikonge? Kwi kwi kwi!!!!

Aafadhali Kyela kumbe tunatembeza bakora kwa viongozi wabovu.

Hao vijana wameambiwa tu wakaseme nini, yaani watanzania tumegeuka vikaragosi vya watu wengine. Kuna wa RA, kuna wa Mengi, kuna wa Manji, kuna wa Mtanzania kwi kwi kwi!!!

Mtu mwenye dhiki kweli hawezi kuwa huru. Hawa vijana inatakiwa wasaidiwe waweze kujitegemea na wala sio kutegemea mifuko ya wanasiasa majambazi. Ndio maana viongozi wetu wangependa kuona hawa vijana wanazidi kuwa wajinga na kuendelea kuimba nyimbo zao. Balaa kabisa hii!
 
Tamko la Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Tabora

5. Tumefuatilia kwa karibu mwenendo na Ziara za Ndugu Mengi akiwa na Msafara wa Wabunge huku akitoa Misaada Mbali mbali, na tumepata taarifa kwamba anakuja katika wilaya ya Mkoa wa Tabora, Uvccm Mkoa wa Tabora inatoa Angalizo ikiwa kama misaada yake inaendana na tabia ya kutukana na kuwaundia majina mabaya viongozi wetu wa Chama, tunamuonya kama vijana wa Tabora na kamwe hatutavumilia jambo hili. Wananchi wa Tabora wana matatizo mengi, lakini vilevile wanaheshimu utu na kamwe hatuwezi kukubali matatizo yetu yatumike kudhalilishwa utu wetu na wa viongozi wetu tuliowachagua kidemokrasia.


KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI[/COLOR][/SIZE][/FONT]

Wilaya ya mkoa wa Tabora ni ipi hiyo .... utetezi wa fisadi unawafumba hadi mnaandika pumba tupu.

Phweeewhu ....
 
Ajabu na kweli leo uvccm Tabora wanamtetea Rostam kuhusu ufisadi,jana wazee wa yanga walitoa tamko la kumtetea Manji.jamani haya ni makundi ya watu wenye njaa kali tusipoteze muda wa kujibizana nao.nchi hii ya ajabu sana ukimwona mtu anajinufaisha kupitia nafasi aliyonayo ukisema wanakuona mbaya .oo fulani anatibu dili za watu,jamani hatutafika tusipoambizana ukweli.
 
Back
Top Bottom