Paramagamba
Member
- May 12, 2017
- 85
- 129
Nadhani alikuja na Lori ili afanye usafi ndani mwangu kwa sababu sijawahi kuona maishani mwangu usafi wa namna hii. Wizi gani huu unaiba mpaka vyeti vya shule? Mwizi gani huyu anaiba mpaka business card? Nimerudi toka kazini ile nafungua tu mlango nakutana na sakafu inanizomea.
Hakuna kitu hata kimoja juu ya sakafu kuanzia Sebuleni, Jikoni mpaka vyumbani. Hata kama ni kukomoana sio kwa kiwango hiki, yani ameacha sabuni tu bafuni sasa ninafanyaje mjini si ni bora tu nirudi kijijini sasa.
Umeniibia mali zangu zote nilizozitafuta kwa jasho maisha yangu yote haitoshi umeamua kuniibia mpaka na vyeti vyangu vyote kuanzia elimu ya msingi mpaka chuo kikuu, ameiba hati ya kiwanja, kampuni na mikataba yangu mingi tu ameondoka nayo, huyu ni mwizi wa aina gani jamani?
Nilisusa wiki nzima nalala usiku bila kufunga milango ya nyumba aje amalizie na hizi sabuni alizoziacha bafuni. Yani kanirudisha nyuma miaka 20. Sikubali. Nimeamua kuwekeza kwa ajili yake. Nitamshughulikia ipasavyo perpendicular.
Nimeamua rasmi kumtangazia vita kali na nipo tayari kwa lolote. Ninaomba mwenye mawazo zaidi ni namna gani nitaweza kumshughulikia huyu mwizi ipasavyo aweze sio tu kurejesha vyeti vyangu bali pia ashike adabu akatoe ushuhuda na kwa wezi wengine ulimwenguni.
Mawazo yenu ni muhimu ndugu zangu.