Pre GE2025 Mwl. Japhet Maganga: Wakurugenzi waendelee kusimamia Uchaguzi Mkuu mwaka 2025

Pre GE2025 Mwl. Japhet Maganga: Wakurugenzi waendelee kusimamia Uchaguzi Mkuu mwaka 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Katibu mkuu wa CWT atakuwa amewakilisha mawazo ya maelfu ya waalimu nchini kuhusu jambo hili la mchakato wa uchaguzi mkuu usimamiwe na wakurugenzi wa halmashauri wa wilaya.

Wakurugenzi hawa wa wilaya ambao ni makada wa chama cha Mapinduzi wanaoteuliwa / kutenguliwa / kuhamishwa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ambaye ni mgombea urais.
 
VYAMA VYA SIASA VISIVYO PUNGUA 6 NA WASHIRIKI BINAFSI 376, TAASISI NA MASHIRIKA MBALIMBALI WAFIKA DODOMA KUTOA MAONI

View: https://m.youtube.com/watch?v=n_smd697UXI

Ifuatayo ni Ripoti kwa urefu kutoka Dodoma kuhusu miswaada iliyotolewa maoni mbele ya Kamati Ya Kudumu Ya Bunge ya utawala, sheria na katiba ambapo kamati ya kudumu ilisikiliza na kupokea maoni ya wadau na wananchi tarehe 6 January 2024. Zoezi hilo ni la siku nne mfululizo lililoanza leo January 6 2024. Hii ni fursa adimu imetolewa isiyopatikana kirahisi ameseme Dkt. Joseph Kizito Mhagama ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Bunge.

0M7A5062-681x387.jpg
Picha: mwenyekiti Dkt. Joseph Mhagama ameketi (katikati) na kushoto Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Florent Kyombo na Katibu wa kamati hiyo, Ndg. Frank Nkya.

Leo tarehe 6 Januari, 2024 Bungeni Jijini Dodoma. Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama (mbunge CCM) akiongoza kikao cha kamati hiyo kilichopokea maoni ya wadau kuhusu miswada minne ya Sheria iliyosomwa Bungeni kwa mara ya kwanza wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge.

Miswada hiyo ni : Mswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2023
; Mswada wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wa Mwaka 2023; Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.5) wa Mwaka 2023 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.5) Bill, 2023]; na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa wa Mwaka 2023 [The Political Affairs Laws (Amendment) Bill, 2023].
0M7A5154-1024x815.jpg

Mbunge wa Jimbo la Nyang’hwale, Mhe. Hussein Nassor Amar akichangia jambo wakati wa utoaji wa maoni kwa wadau kuhusu miswada minne ya Sheria .

0M7A5308-1024x683.jpg

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Mhe. Zitto Kabwe akitoa maoni leo tarehe 6 Januari, 2024 Bungeni Jijini Dodoma.

0M7A5497-1024x683.jpg

Leo tarehe 6 Januari, 2024 Bungeni Jijini Dodoma Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakifuatilia maoni ya wadau kuhusu miswada minne ya Sheria .

0M7A5678-1024x683.jpg

Wadau Mbalimbali wakifuatilia utoaji wa maoni kuhusu miswada minne, leo tarehe 6 Januari, 2024 Bungeni Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
 
08 January 2024
Movement ya Wananchi Watanzania watoa maoni

View: https://m.youtube.com/watch?v=rm8wI2pHQ4s
Miswada hiyo ni : Mswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2023; Mswada wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wa Mwaka 2023; Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.5) wa Mwaka 2023 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.5) Bill, 2023]; na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa wa Mwaka 2023 [The Political Affairs Laws (Amendment) Bill, 2023]

Movementi hiyo haifungamani na chama chochote cha kisiasa pia ipo kwa ajili ya kuondoa dhana kuwa kuna kundi la wachache wenye hati miliki kuhusu wapi kutolewe maoni, kina nani wana haki ya kuongoe kwa kustakabali wa nchi yetu sote inayoitwa Tanzania. Leo movementi hiyo meza kuu wapo
akiwemo mama Celestine Simba, Dr. Slaa, wakili Mwabukusi, Mdude .....
.
 
MAONI MBELE YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE MASUALA YA UTAWALA, SHERIA NA KATIBA

6 January 2024
Katibu Mkuu chama cha walimu (CWT) Mwl. Japhet Maganga ashauri ma- DED waendelee kusimamia Uchaguzi Mkuu mwaka 2025

View: https://m.youtube.com/watch?v=I3RC9WBcx0w
Source : mwananchi digital

Mwalimu Japhet Maganga na wadau wengine wa Usawa wa Kijisia, vyama vidogo vya siasa, asasi kadhaa za kiraia, makundi ya vijana n.k wanazungumza kutoka Bungeni Jijini Dodoma leo Jumamosi, Januari 6, 2024 wakati ambapo Kamati ya Kudumu ya Bunge inayosimamia masuala ya Utawala, Sheria na Katiba inaendelea kupokea maoni ya wadau mbalimbali kuhusu miswada ya sheria mbalimbali ikiwemo inayohusu uchaguzi.

Wadau mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa Chama cha walimu Tanzania (CWT) Mwalimu Japhet Maganga ambaye ameshauri Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuendelea kuwatumia Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2025, huku uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 ukiendelea kusimamiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na wadau wengine wakitoa maoni yao.

Wadau wanaopendekeza wasisitiza wakurugenzi wa halmashauri za wilaya ma-DED kuendelea kusimamia uchaguzi, wasema ma-DED ndiyo wanaelewa hali halisi katika jiografia wilayani, tamaduni za wakazi wa maeneo pia wana rasilimali fedha na mamia ya waalimu ambao hutumika kufanikisha mchakato mzima wa uchaguzi mkuu.

Wadau hawa wanazungumza kutoka Bungeni Jijini Dodoma leo Jumamosi, Januari 6, 2024 wakati ambapo Bunge linaendelea kupokea maoni ya wadau mbalimbali kuhusu miswada ya sheria mbalimbali ikiwemo inayohusu uchaguzi.

Naye mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya utawala, sheria na katiba, mheshimiwa Dkt. Joseph Kizito Mhagama (Mbunge CCM) aliwapa miongozo ya jinsi ya wadau kuwasilisha maoni yao.

Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Kudumu ya bunge amewaomba wadau hao 367 kuwa wavumilivu kusikiliza hoja za makundi mbalimbali hata kama vinakinzana kwani zoezi hilo la kusikiliza maoni ni kwa ajili ya kuboresha, kuweka mapya au kuondoa baadhi ya mambo yaliyowakilishwa ktk miswada muhimu.

Nia ni kupata kitu kitachosaidia kamati ya bunge na bunge kufanya maamuzi yamayozingatia umma mpana wa Tanzania unataka mabadiliko gani ktk miswada kadhaa ikiyowakilishwa bungeni.

Huyu mwalimu kumbe hana akili timamu sawa na walimu wenzake
 
Huyu mwalimu kumbe hana akili timamu sawa na walimu wenzake

Wanananchi na makundi mengine tayari mmeona yaliyojiri mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika Dar es Salaam pia wale ambao wanaendelea kufika kutoa maoni mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge masuala ya utawala, sheria na katiba maoni yao ni yepi.

Hivyo ni wajibu wa kila mtanzania kuendelea kutoa maoni popote alipo, katika jukwaa lolote ili wasisike nini wanataka ili wasitekwe nyara na makundi mawili yaani Baraza la Vyama vya Siasa na yale makundi yaliyokwenda Dodoma kutoa maoni kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge.
 
Basi sawa
 
Kama hoja ni kujua jiografia ya maeneo basi Wenyeviti wa vyama katika maeneo husika ndiyo wasimamie maana wengi Huwa wanakuwa wazawa wa maeneo husika tofauti na DED na timu yake amabao ni wa kuja kwa mapenzi ya Mwenyeheri na Mpakwa mafuta Samia Suluhu Hasan.
Huyo Maganga aache upuuzi,kila taasisi ifanye kazi kwa mujibu wa sheria,NEC kazi yao ni kuendesha zoezi la uchaguzi na DED kazi yake ni kusimamia shughuli za maendeleo katika Wilaya.Kila mtu ashinde mechi yake!
Tuzingatie utawala bora mbona hiyo cwt ina matawi mikoani na wilayani,Tume ya utumishi wa walimu,Tume ya utumishi wa umma iko every corner of this country,sembuse hii ya uchaguzi ambayo ni muhimu mno. je wao mazingira ya kijografia wanayafanyaje? hoja dhaifu mno kuzingatiwa.
 
09 JANUARY 2024
MAONI YA CCM MBELE YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE - YAOMBA MABADILIKO YAFUATAYO KATIKA MUSWADA

View: https://m.youtube.com/watch?v=jX_cKdVqHtY
Maoni hayo yametolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM Taifa (UWT) Mary Chatanda leo Jumenne, Januari 9, 2023 jijini Dodoma ambapo wadau mbalimbali wanaendelea kutoa maoni yao kuhusu sheria mbalimbali ikiwemo sheria tatu zinazohusu masuala ya uchaguzi.

Chama cha Mapinduzi CCM kimepongeza mabadiliko ya sheria za uchaguzi na hatua iliyochukuliwa na Bunge ya kukusanya maoni ya watu mbalimbali kwenye miswada ya sheria ikiwemo miswada mitatu inayohusu masuala ya uchaguzi huku kikishauri mambo 7 ikiwemo kuhusu kutokuwepo kwa ulazima kwa sheria kuwataja waziwazi wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi.
 
KANISA KATOLIKI LAFIKA MBELE YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE MASUALA YA UTAWALA, SHERIA NA KATIBA

View: https://m.youtube.com/watch?v=L8OSm7yc2N4
Kanisa Katoliki Tanzania kupitia Askofu Jude Thadaeus Ruwa'ichi OFMCap, yawasilisha maoni yake juu ya miswada ya sheria ya uchaguzi na sheria ya Tume ya Uchaguzi mbele ya kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulika na masuala ya utawala, sheria na katiba.

Katika mambo 21 ambayo Kanisa Katoliki la Tanzania limependekeza kufanyiwa maboresho au kuondolewa kabisa, ni yanahusu uhuru wa wafanyakazi wa tume, uteuzi wa mwenyekiti na makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, haki ya kuhoji matokeo n.k n.k
 
Joseph Selasini na Doyo Hassan Doyo - wasifia miswada ni mizuri, tuwape nafasi wakurugenzi

View: https://m.youtube.com/watch?v=laxvm3-rwz4

Mwanasiasa mkongwe Joseph Selasini, na Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance For Democratic Change (ADC) Doyo Hassan Doyo wasema - Mambo ni mazuri, suala ni utashi na maDED wapewe nafasi kusimamia uchaguzi 2025..

Joseph Selasini awaomba baadhi ya wanasiasa wanaoponda miswada hii wajifikirie, maana siyo Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete wala John Joseph Magufuli walithubutu kujitosa kuleta marekebisho ya sheria hizi muhim, ila Rais mwenzao Dr. Samia Hassan ameonesha utashi na nia kwa kuwasikiliza watanzania hadi miswada kuundwa na pia kuchambuliwa mbele ya Kamati ya Bunge, hii ni hatua kubwa ...
 
MAONI MBELE YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE MASUALA YA UTAWALA, SHERIA NA KATIBA

6 January 2024
Katibu Mkuu chama cha walimu (CWT) Mwl. Japhet Maganga ashauri ma- DED waendelee kusimamia Uchaguzi Mkuu mwaka 2025

Mwalimu Japhet Maganga na wadau wengine wa Usawa wa Kijisia, vyama vidogo vya siasa, asasi kadhaa za kiraia, makundi ya vijana n.k wanazungumza kutoka Bungeni Jijini Dodoma leo Jumamosi, Januari 6, 2024 wakati ambapo Kamati ya Kudumu ya Bunge inayosimamia masuala ya Utawala, Sheria na Katiba inaendelea kupokea maoni ya wadau mbalimbali kuhusu miswada ya sheria mbalimbali ikiwemo inayohusu uchaguzi.

Wadau mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa Chama cha walimu Tanzania (CWT) Mwalimu Japhet Maganga ambaye ameshauri Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuendelea kuwatumia Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2025, huku uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 ukiendelea kusimamiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na wadau wengine wakitoa maoni yao.

Wadau wanaopendekeza wasisitiza wakurugenzi wa halmashauri za wilaya ma-DED kuendelea kusimamia uchaguzi, wasema ma-DED ndiyo wanaelewa hali halisi katika jiografia wilayani, tamaduni za wakazi wa maeneo pia wana rasilimali fedha na mamia ya waalimu ambao hutumika kufanikisha mchakato mzima wa uchaguzi mkuu.

Wadau hawa wanazungumza kutoka Bungeni Jijini Dodoma leo Jumamosi, Januari 6, 2024 wakati ambapo Bunge linaendelea kupokea maoni ya wadau mbalimbali kuhusu miswada ya sheria mbalimbali ikiwemo inayohusu uchaguzi.

Naye mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya utawala, sheria na katiba, mheshimiwa Dkt. Joseph Kizito Mhagama (Mbunge CCM) aliwapa miongozo ya jinsi ya wadau kuwasilisha maoni yao.

Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Kudumu ya bunge amewaomba wadau hao 367 kuwa wavumilivu kusikiliza hoja za makundi mbalimbali hata kama vinakinzana kwani zoezi hilo la kusikiliza maoni ni kwa ajili ya kuboresha, kuweka mapya au kuondoa baadhi ya mambo yaliyowakilishwa ktk miswada muhimu.

Nia ni kupata kitu kitachosaidia kamati ya bunge na bunge kufanya maamuzi yamayozingatia umma mpana wa Tanzania unataka mabadiliko gani ktk miswada kadhaa ikiyowakilishwa bungeni.

sasa mtu mwenyewe ni mwalimu, kunafikiri angeongea nini? ndio maana huwa tuansema waalimu ni mafeliaz ndio maana wamekuwa waalimu. hata hivyo tunawashukuru kwa kutugawia walichotugawia wakati wakihangaika na maisha baada ya kufeli mitihani ya kuendelea na course bora zaidi.
 
10 January 2024

Askofu Konki: Rais amejali sana ushirikishwaji kwenye utawala wake hasa kwenye miswada hii ya sheria

View: https://m.youtube.com/watch?v=7FS-ySRQcfY
Askofu Mkuu wa Kanisa la Elim Pentekoste Tanzania, Peter Konki akizungumza wakati akitoa maoni yake kwenye miswada mbalimbali ya sheria ikiwemo miswada inayohusu masuala ya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom