Huyu mwalimu kumbe hana akili timamu sawa na walimu wenzakeMAONI MBELE YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE MASUALA YA UTAWALA, SHERIA NA KATIBA
6 January 2024
Katibu Mkuu chama cha walimu (CWT) Mwl. Japhet Maganga ashauri ma- DED waendelee kusimamia Uchaguzi Mkuu mwaka 2025
View: https://m.youtube.com/watch?v=I3RC9WBcx0wSource : mwananchi digital
Mwalimu Japhet Maganga na wadau wengine wa Usawa wa Kijisia, vyama vidogo vya siasa, asasi kadhaa za kiraia, makundi ya vijana n.k wanazungumza kutoka Bungeni Jijini Dodoma leo Jumamosi, Januari 6, 2024 wakati ambapo Kamati ya Kudumu ya Bunge inayosimamia masuala ya Utawala, Sheria na Katiba inaendelea kupokea maoni ya wadau mbalimbali kuhusu miswada ya sheria mbalimbali ikiwemo inayohusu uchaguzi.
Wadau mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa Chama cha walimu Tanzania (CWT) Mwalimu Japhet Maganga ambaye ameshauri Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuendelea kuwatumia Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2025, huku uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 ukiendelea kusimamiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na wadau wengine wakitoa maoni yao.
Wadau wanaopendekeza wasisitiza wakurugenzi wa halmashauri za wilaya ma-DED kuendelea kusimamia uchaguzi, wasema ma-DED ndiyo wanaelewa hali halisi katika jiografia wilayani, tamaduni za wakazi wa maeneo pia wana rasilimali fedha na mamia ya waalimu ambao hutumika kufanikisha mchakato mzima wa uchaguzi mkuu.
Wadau hawa wanazungumza kutoka Bungeni Jijini Dodoma leo Jumamosi, Januari 6, 2024 wakati ambapo Bunge linaendelea kupokea maoni ya wadau mbalimbali kuhusu miswada ya sheria mbalimbali ikiwemo inayohusu uchaguzi.
Naye mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya utawala, sheria na katiba, mheshimiwa Dkt. Joseph Kizito Mhagama (Mbunge CCM) aliwapa miongozo ya jinsi ya wadau kuwasilisha maoni yao.
Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Kudumu ya bunge amewaomba wadau hao 367 kuwa wavumilivu kusikiliza hoja za makundi mbalimbali hata kama vinakinzana kwani zoezi hilo la kusikiliza maoni ni kwa ajili ya kuboresha, kuweka mapya au kuondoa baadhi ya mambo yaliyowakilishwa ktk miswada muhimu.
Nia ni kupata kitu kitachosaidia kamati ya bunge na bunge kufanya maamuzi yamayozingatia umma mpana wa Tanzania unataka mabadiliko gani ktk miswada kadhaa ikiyowakilishwa bungeni.
Huyu mwalimu kumbe hana akili timamu sawa na walimu wenzake
Basi sawaWanananchi na makundi mengine tayari mmeona yaliyojiri mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika Dar es Salaam pia wale ambao wanaendelea kufika kutoa maoni mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge masuala ya utawala, sheria na katiba maoni yao ni yepi.
Hivyo ni wajibu wa kila mtanzania kuendelea kutoa maoni popote alipo, katika jukwaa lolote ili wasisike nini wanataka ili wasitekwe nyara na makundi mawili yaani Baraza la Vyama vya Siasa na yale makundi yaliyokwenda Dodoma kutoa maoni kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge.
Ualimu Pasipo Elimu (U.P.E)Tangu ualimu urasimishwe kuwa ni kwa wale waliofeli sekondari na kutokuwa na ufaulu wa kuingia vyuo vikuu au vya kati, hapo ndipo tukaanza kupata walimu wasio na upeo mkubwa wa kufikiri.
Tuzingatie utawala bora mbona hiyo cwt ina matawi mikoani na wilayani,Tume ya utumishi wa walimu,Tume ya utumishi wa umma iko every corner of this country,sembuse hii ya uchaguzi ambayo ni muhimu mno. je wao mazingira ya kijografia wanayafanyaje? hoja dhaifu mno kuzingatiwa.Kama hoja ni kujua jiografia ya maeneo basi Wenyeviti wa vyama katika maeneo husika ndiyo wasimamie maana wengi Huwa wanakuwa wazawa wa maeneo husika tofauti na DED na timu yake amabao ni wa kuja kwa mapenzi ya Mwenyeheri na Mpakwa mafuta Samia Suluhu Hasan.
Huyo Maganga aache upuuzi,kila taasisi ifanye kazi kwa mujibu wa sheria,NEC kazi yao ni kuendesha zoezi la uchaguzi na DED kazi yake ni kusimamia shughuli za maendeleo katika Wilaya.Kila mtu ashinde mechi yake!
sasa mtu mwenyewe ni mwalimu, kunafikiri angeongea nini? ndio maana huwa tuansema waalimu ni mafeliaz ndio maana wamekuwa waalimu. hata hivyo tunawashukuru kwa kutugawia walichotugawia wakati wakihangaika na maisha baada ya kufeli mitihani ya kuendelea na course bora zaidi.MAONI MBELE YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE MASUALA YA UTAWALA, SHERIA NA KATIBA