DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Aliyekuwa Katibu wa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, ambaye ni Mwalimu na Mwandishi mahiri wa Makala , Mwl. Makungu Mussa Sweya, jana 2/7/2025 alichukua na kurejesha fomu ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Bariadi Vijijini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mwl. Makungu Ms amesema amefanya maamuzi haya akitambua uwepo wa upinzani mkali ndani ya jimbo hilo toka kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Reli (Masanja Kadogosa) ambaye pia amechukua fomu kugombea jimbo hilo.
Jimbo la Bariadi Vijijini ni jimbo jipya zao lililopatikana baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Bariadi, na kupatikana majimbo mawili ya Bariadi Vijijini na Bariadi Mjini.
Jimbo hilo kabla ya kugawanywa lilikuwa chini ya Andrea Kundo (Naibu Waziri wa Maji) ambaye kwa sasa ameamua kugombea Jimbo la Bariadi Mjini.
Mwl. Makungu Ms, kijana mwenye itikadi ya utu na usawa na misimamo mikali dhidi ya ubadhirifu wa mali za umma na ugumu wa maisha ya Mtanzania, ambaye falsafa zake zimekuwa zikionekana wazi katika makala zake mbalimbali, amepata uungwaji mkono mkubwa sana toka katika kundi la vijana walio na maisha ya kawaida (wapwa) ambao ni wengi katika Jamii ya Wanabariadi.
Kauli mbiu ya vijana hawa kuwa "Aliyeshiba hamjui mwenye njaa", inaonekana kuungwa mkono na watu wengi wa hali za maisha ya kawaida ili kutuma ujumbe kwa wale wanaodhani kuwa kugawa fedha za rushwa kwa wajumbe ndiyo njia pekee ya kujihakikishia ushindi ili hali wakishapita na kuwa wabunge wanaondoka hawakumbuki tena hali duni za watu wenye njaa.
Aliyeshiba hamjui mwenye njaa, na hivyo ambao hawajashiba wameungana pamoja kumuweka mwenzao.
Macho yetu tunayaangazia katika Jimbo la Bariadi Vijijini kwa umakini mkubwa mpaka mwisho wa mchakato huu wa uteuzi wa wagombea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).