semenya Binafsi nimeshukuru na kufurahi na changamoto yako, lakini naomba kukuliza wewe mwenyewe ungekuwa kwenye kamati ya kuscreen watu wa kuwapa Nobel Prize ungeweza kumteteaje mwalimu JKN kuwa apewe na anastahili hiyo award/prize? Maana katika bandiko lako unasema kafanya mengi kwa bara la Africa mengi yepi? Nobel Prze zilianzishwa na mtu ambaye alilaani vita JKN alipigana vita na Uganda, vita ambayo hata hapa JF tumequestion mantiki yake. Sababu alizosema tulikuwa nazo za kwenda uganda leo hii wengi wetu hatuzioni?? wangapi walikufa Uganda? kwa kufa kiasi hicho cha watu tayari anakuwa disquliafied kupata NOBEL.
Ukiangalia hotuba zake, tafuta hata You tube zipo utaioona hotuba moja anayosema kuwa aliombwa apatanishwe na Idd Amin lakini kwa maneno yake mwenyewe anasema aliwauliza watu wanaosema kuwa aache kumpiga Idd Amini kuwa walikuwa wapi??? Sasa Mkuu Nobel Prize haaziendi kwa Jicho kwa jicho, zinaenda kwa ukipigwa shavu la kushoto geuza la kulia.
Desmond Tutu siku moja alipokuwa anatembea mtaanzai aliona Mob wanamtandika kijana alienda akamwangukia juu akamfunika watu wakaanza kumpa kibano yeye mpaka alipookolewa na dola. Nelson Mandela alipoteza uraia wake kwa kuchoma Passport, kuna watu wameadnika Historia kubwa sana kama akina Steve Biko, Chris Hann, Bob Moses lakini bado hawajatambuliwa.
JKN alihamisha watu kutoka kwenye vijiji vyao kwa nguvu, watu wengi walipigwa na migambo, walichomewa nyumba zao, walipoteza mifugo, waliliwa na simba, acha waliokufa kwa maralia, Taifodi, vipindupindu kwenye maeneo waliyowekwa yasioyofaa kwa maisha ya Binadamu.
JKN alitaifisha mali za watu kwa azimio lake la arusha (hii ni sawa na anachofanya comrade Mugabe-Jongwe)
Pitia vigezo vya Nobel alafu toa mchanganuo cha alichofanya JKN kuweza kutunukiwa hiyo Prize. Ni Mtazamo Tu
Mbongela, Mtizamo wako mbovu, umefulia kimawazo na kimantiki. Mwezi mzima Watanzania na watu wengine duniani; nasema duniani kwa sababu kuna maadhimisho na Makongamano ya Kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo cha Mwalimu yanafanyika Kimataifa nje ya nchi yetu kumu-enzi kwa yale aliyoyafanya. Sasa wewe ndugu yangu unayejaribu kutuletea utumbo huu ni dhahiri kwamba huna ulijualo kuhusu Mwalimu ama una chuki binafsi tu kwa sababu huenda uliguswa wewe ama nduguzo katika hayo uliyoyaeleza.
Tukija kwenye vita vya Uganda ambavyo unadai Mwalimu alipigana bila sababu. You are totally mistaken. Katika hiyo hotuba unayoizungumzia, Mwalimu alisema Umoja wa Mataifa na hata Umoja wa nchi Huru za Afrika hawakufanya lolote hata kukemea tu pale Idd Amin alipotangaza dhamira yake ya kutaka kumega kipande cha Tanzania na alipotishia kuipiga Tanzania hadi Dar es Salaam.
Unataka kutuambia kwamba wewe ulitaka Idd Amin aingie kuteka maeneo ya Tanzania na Mwalimu Nyerere akiwa Rais wa nchi Tanzania akae kimya tu kama mwanamke anayesubiri kupigwa makofi na mume mlevi? Chief Mkwawa alipigana na Wajerumani na Wahehe wengi walikufa katika vita hivyo. Wataka kutuambia kwamba kwa kuwa watu wengi walikufa katika vita na Wajerumani basi vita hivyo vilikuwa havina mantiki na Mkwawa asingestahili kupata tuzo lolote kwa kuwa watu walikufa?
Kwa hiyo, Desmond Tutu ni zaidi ya Mwalimu kwa sababu alimlalia na kumuokoa mtu mmoja tu! Usisahau kwamba Mwalimu alikuwa Rais wa nchi kumtaka aanze kulalia wanaopigwa mitaani ni utupu wa mawazo. Pia usituletee habari ya kugeuza shavu katika masuala ya uongozi na ulindaji wa maslahi ya nchi, haviendani. Pia, Mwalimu kama Rais wa nchi yake Tanzania alikuwa sawa kabisa na ambavyo Obama alivyo leo Rais wa nchi ya Marekani. Tofauti za kuona Rais wa Marekani ni zaidi kwa hiyo anastahili tuzo za aina hiyo na si Rais wa nchi ndogo kama Tanzania zinaletwa na fikra potofu tu. Nakubaliana na wanaosema kwamba tuzo hizo zina agenda za kisiasa ndani yake. Vita vya ukombozi Kusini mwa Afrika, jemadari wake mkuu alikuwa Mwalimu Nyerere. Kama watoaji wa Nobel Peace Prize wangelikuwa hawana ajenda zingine hili tu lingemfanya astahili kupata hiyo tuzo kuliko huyo aliyelalia mtu!
Kuhusu Vijiji vya Ujamaa, ni kweli wapo watu waliohamishwa kwa nguvu n.k. lakini watu wenye akili tunajua kwamba hayo hayakuwa malengo wala maelekezo ya Mwalimu. Mwalimu tunayemfahamu asingaliweza kamwe kuagiza watu wahamishwe kwa nguvu ama wapigwe na kuchomewa nyumba zao. Kama ambavyo leo tunaimba wimbo wa watendaji ama wasaidiai wabovu ambao wanamuangusha Rais Kikwete katika dhamira yake ya maisha bora kwa kila Mtanzania, hivyo ndivyo ilivyokuwa katika utekelezaji wa sera ya Vijiji vya Ujamaa. Nia na madhumuni yalikuwa safi kabisa. Lengo lilikuwa ni kuwaweka wananchi waishi sehemu moja ili Serikali iweze kuwafikishia huduma za jamii kwa urahisi na wao waweze kufanya kazi zao kwa kushirikiana ili wajiletee maendeleo yao haraka. Siku hizi tunazungumzia habari za wananchi kujikwamua kiuchumi kwa kuungana kwenye vikundi k.m. Saccos, Vikoba, Msaragamba, n.k. Hayo yote yalikwishaanzishwa na Mwalimu katika sera yake ya Vijiji vya Ujamaa ni majina tu yanabadilishwa lakini lengo ni lile lile la wanyonge kuungana na kushirikiana katika mambo yao ya kujitafutia maendeleo kwa manufaa yao wenyewe.
Azimio la Arusha linakumbukwa na litaendelea kukumbukwa, kwa nini? Kwa sababu lilikuwa linatetea maslahi na mustakabali wa wanyonge walio wengi dhidi ya wachache waliokuwa wameanza kujipanga kutaka kutumia uwezo na madaraka waliyopewa kujinufaisha wenyewe na kuwasahau waliowapa madaraka yale. Ndani ya Azimio la Arusha kuna mwongozo wa maadili mema na miiko ya uongozi ambayo wanayo hata Marekani na nchi zingine ambazo tunatakiwa tuzisujudu.
Jamani, yeyote anayejaribu kumkandia Mwalimu ama kumpaka matope ni wazi anaonekana mgonjwa wa akili mbele ya jamii ya Kitanzania inayomuheshimu na kum-enzi Mwalimu kwa mengi mema aliyoyatenda ambayo kila Mtanzania amewahi kuguswa nayo kwa namna moja ama nyingine. Mbogela, acha bwana Mwalimu kalala kwa amani Mbinguni na Duniani ana WATETEZI!