Mwl. Nyerere alitaka vyama viwili imara vya siasa vishindane kama tunataka tufanikiwe

Mwl. Nyerere alitaka vyama viwili imara vya siasa vishindane kama tunataka tufanikiwe

Ndoto ya Mwl. Nyerere kukubali vyama vingi vya siasa nchini ni kupata vyama viwili vikubwa vinavyokosoana, kuonyana na kuogopesha kisera katika kuitawala nchi. Hakupenda utitili wa vyama vidogovidogo visivyoweza kuikosoa na kuitikisa CCM katika kuzuia ukabila, umaskini, udini na rushwa.

Vyama vya upinzani na CCM lazima vizingatie maono haya ya Mwalimu kwa mustakabali wetu, watoto na wajukuu wetu; maana leo una madaraka lakini kesho huna, leo uko CCM lakini kesho uko upinzani au huna chama au leo uko upinzani lakini kesho uko CCM.

Ni upuuzi kufanya lisilo na faida au kukataa kufanya jambo lenye faida kwa taifa kwakuwa tu wewe leo uko na madaraka.
Nini kifanyike
 
Hebu fafanua vizuri mkuu. Alifuta vyama vya upinzania au vyama vya ushirika na machifu. Hayo makundi ndio wapinzania au mimi ndio nimechelewa kuzaliwa?
Ulichelewa aseee....lakini hata darasani haukusoma kuwa alifuta vyama vya kisiasa !?
 
Nini kifanyike
Vyama vyote vifutwe kabisa tuanze upyaaaah, nchi iwe chini ya utawala wa Jeshi kwa miaka mitatu, then ufanyike uchaguzi huru na haki aliyeshinda kwenye sanduku la kura ndiye atangazwe mshindi.
 
Vyama vyote vifutwe kabisa tuanze upyaaaah, nchi iwe chini ya utawala wa Jeshi kwa miaka mitatu, then ufanyike uchaguzi huru na haki aliyeshinda kwenye sanduku la kura ndiye atangazwe mshindi.
Je jeshi halitakuwa biased naliona kama ni wazo zuri vile kwa maana njia nyepesi tutakwama kwasababu tutakutana na watu wale wale wanao ahirisha kufikiri kwa nafsi a.k.a kujizima data
 
Vyama vyote vifutwe kabisa tuanze upyaaaah, nchi iwe chini ya utawala wa Jeshi kwa miaka mitatu, then ufanyike uchaguzi huru na haki aliyeshinda kwenye sanduku la kura ndiye atangazwe mshindi.
Wanajeshi ni makada
 
Back
Top Bottom