Mwl. Nyerere: Kuna Askari Yupo Tayari Kuua au Kuuawa Kwa Sababu Tu Analipwa Pesa

Mwl. Nyerere: Kuna Askari Yupo Tayari Kuua au Kuuawa Kwa Sababu Tu Analipwa Pesa

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mwl. Nyerere alisema kuwa duniani kuna majeshi ya mamluki ambao hupigana kwa ajili ya fedha pekee. Alitolea mfano baadhi ya mamluki waliowahi kuwepo Congo, akieleza kuwa mtu wa aina hiyo hufanya kazi kwa malipo tu bila kuwa na uzalendo kwa taifa lolote.

Akisema kwamba, mamluki anaweza kwenda upande wowote wa vita ilimradi alipwe fedha. Nchi mbili zikiwa vitani, anaweza kwenda kwa upande mmoja na kuwaambia wamlipo ili awapiganie. Kwa hiyo hana upande maalum wala heshima ya taifa; anachojali ni pesa tu.

Mwl. Nyerere alisisitiza kuwa askari wa aina hiyo yupo tayari kuua au hata kuuawa kwa sababu ya fedha. Tofauti na askari wa kawaida ambaye huwa tayari kupigana, kuua au kufa kwa ajili ya heshima, usalama na maslahi ya nchi yake.

Kuna majeshi duniani ya mathelane walikuwa wapo Congo, mathelane ni mtu anayefanya kazi kwa malipo yani kwa pesa, sababu yake yakufanya hivyo ni pesa tu. Ukimuuliza kwanini unafanya hivyo anasema nalipwa na ajali nani anayemlipa.

Inawezekana nchi mbili adui zinapigana hii na hii anaweza kwenda kwa hii akasema mtanialika wakikubali kumlipa atawapigania yani yeye hana upande anajuwa pesa tu Askari wahivyo wanajuwa pesa tu ni malaya malaya tu

Yupo tayari kuuwa au kuchukua hatari ya kuuwawa kwa sababu ya pesa tu. Ila Askari wa kawaida yupo tayari kufa au kuuwa kwa sababu ya heshima ya nchi yake Amesema Mwl Nyerere

Labda kwa wanajeshi huko haiwezekani, ila kwa wanaume wa kawaida inawezekana kabisa

Tena bora hata wanaokufa kwa ajili ya pesa na sio wale wanaokufa kisa wawahi wakapewe mabikra 72 huko peponi
 
Back
Top Bottom