Usilete kujifanya kujua wakati unapoambiwa ukweli; ungekuwa mwalimu mwenye busara unatakiwa kupokea critiques kwa moyo mkunjufu na kuzifanyia kazi, lakini wewe unaleta ubishi. Nitakurudisha shule ya particle mechanics kama ifuatavyo
(a) Katika elementary mechanics kuna reference tatu (x,y,z), lakini orientation angles zake yaani theta_x, theta_y na theta_z inaweza kuwa na value yoyote. Kwa hiyo x-y-z axes hazina fixed directions. Katika advanced mechanics, kuna an infinite number of axes, na huwa zinakuwa defined kama R^n where n can be any integer. Kwa hiyo madai yako kuwa kuna reference mbili ni kuonyesha ufinyu wako katika somo hilo. Ingawa najua kuwa swali lako lilikuwa constrained katika plane ya karatasi ambayo ni 2-D, bado hujaspecify orientation ya axes zako, na wala maswali yenyewe hayakusema hivyo, ndiyo maana nikakuonya kuwa unakaribisha majibu mengi ambayo utashindwa kuyakana. Kama mwalimu mzuri unapotoa mtihani jitahid kuwa specific kusudi uwe na uhakika wa kupata jibu moja uniformly.
(b) Kudai kuwa mwanafunzi wa form two atafanya assumption ya g ndiko kunawakosesha elimu pana watoto wetu kwani nyie mnawafundisha kukariri kuwa g ni 10m/s^2 wakati siyo kweli. Value halisi ya g ni (GMe/R_e^2) wakati G ni universal gravitational constant, M_e ni mass of earth and R_e ni distance from the center of earth. Kwa vile R_e inabadilika kulingana na kina kutoka usawa wa bahari na vile vile kulingana na latitude (kwa vile dunia ni oval), huwezi kumkaririsha mtoto kuwa g=10 m/s^2 ukadai kuwa unajua. Experiment ikifanyikia Njombe kwenye nyanda za juu, haiwezi kuleta matokeo sawa na yale ya Dar es Salaam kwenye usawa wa bahari. Ni kawaida kwenye mitihani kuweka statement kuwa assume the value of g to be 9.81m/s^ au 10m/s^2; ulitakiwa ufanye hivyo ili kuzuia ambiguity kwenye mtihani wako.
(c) Baada ya somo hilo fupi, nitakuonyesha kuwa maswali yako mengi yana makosa hata kama mtu ungeamini kuwa value ya g=10m/s^2. Kwa mfano swali la 3 unatakiwa upate 8tan(theta)-tan^2(theta)-4=0, siyo kama wewe ulivyoweka. Na vile vile swali la 7, the modulus of elasticity siyo force; kwa hiyo huwezi kuipima katika Newtons, badala yake inapimwa kwa N/m. Katika swali hilo hilo la 7, unatakiwa upate v^2=64+20x-48x^2 siyo kama wewe ulivyoweka. Lugha iliyotumika katika maswali yako mengi ina ambiguities nyingi ambazo hutakiwi kuzionyesha kwa watahiniwa wako, ukizingatia kuwa wana time constraints, kwa hiyo hawawezi kupoteza muda wao wakifikiria swali lina maana gani wakati wanatakwaiwa wajibu swali lao kabla muda wa mtihani haujaisha.
Samahani kwa kuandika kwa kirefu hivyo; umenichokonoa mwenyewe. Unfortunately inaonekana kama vile huu ni mtihani uliowahi kutolewa kwa wanafunzi wetu katika shule mojawapo nchini, na inawezekana kuna wanafunzi walioambiwa kuwa wamafeli wakati maswali yenyewe yana mapungufu namna hiyo.