SI KWELI Mwonekano wa uwanja wa ndege terminal 3 JKNIA

SI KWELI Mwonekano wa uwanja wa ndege terminal 3 JKNIA

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Picha hii inasambaa kwenye mitandao ya kijamii ikibainisha kuwa huu ni uwanja wa ndege ya Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere, Dar es Salaam.

Jamii Check tusaidieni kufuatilia hili.

1658214384245.png

Picha inayodaiwa kuonesha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere
 
Tunachokijua
Septemba 9, 2016, picha kadhaa zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa kuonesha sehemu ya uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam.

Sehemu ya meneno yaliyoambatana na picha hizo ni haya:

“Hapa ni mwonekano wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Dar es Salaam, hii imeendelea kuijengea sifa Tanzania, na Serikali inayotawala ambayo inatekeleza ilani ya Chama husika, ikirekebishwa rekebishwa na vyama vya upinzani.

Ilikuwa aibu kubwa kwa nchi kama Tanzania kuwa na airport yenye mwonekano kama ilivyokuwa, Mwaka 2008, nilikutana na mheshimiwa wa mmoja (Foreigner) ambaye anafanya kazi Ubalozini, alikuwa akisemea kuwa airport yetu ni chafu na haina muonekano wa airport.”


Ukweli wa picha hizi
JamiiForums imefuatilia madai haya na kubaini kuwa picha hizi sio za Tanzania, pia hazina uhusiano wowote na mazingira ya uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere.
1_16a08383c41.1977248_3549962273_16a08383c41_medium.jpg

Uwanja wa Ndege wa Muscat (Sio Uwanja wa Mwalimu Nyerere kama inavyodaiwa)
Utafutaji wa Kimtandao unabainisha uwanja huu kuwa wa Kimataifa wa Muscat na unatazamiwa kumalizika mnamo mwaka 2017.

Awamu ya kwanza ya uwanja huo itakamilisha ujenzi wa kaunta 86 za abiria, mikanda 10 ya kupokelea mizigo pamoja na mageti 40 ya kuingia na kutoka.

Aidha, utakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 12 kwa mwaka.

Makala yanayotoa taarifa za uwanja huu yameandikwa pia na Gazeti la Gulf News.

Picha hizi zilichapishwa pia na The Nkoromo Blog, Charaz Blogspot na Mtaa kwa Mtaa zote zikiwa na maelezo yanayodai kuwa ni uwanja wa Kimataifa wa JK Nyerere, jambo ambalo JamiiForums imebaini sio ka kweli.
Back
Top Bottom