SoC02 Mwonekano wangu chakula changu

SoC02 Mwonekano wangu chakula changu

Stories of Change - 2022 Competition

Zamugrandson

New Member
Joined
Aug 12, 2022
Posts
1
Reaction score
4
Kulingana na tafiti za kisayansi zinasema, jinsi wanadamu tunavyoonekana ni kwa sababu ya chakula tunachokula kila siku.

Tangu kuwepo kwa dunia mwanadamu amekuwa anategemea chakula ili aweze kuishi. Ulimwengu umeghubikwa na wimbi la shughuli nyingi mchana na usiku ili kutafuta chakula kwa ajili ya familia.

Hata hivyo, kila familia inapambana angalau kupata chakula kilicho bora. Chakula kimelengwa kuimarisha afya za miili yetu. Ni kupitia chakula tunapata virutubisho vyenye kuupatia mwili nguvu za kufanya shughuli zetu zote. Lishe bora ni miongoni mwa kanuni saba za kujenga afya iliyo bora. Seli zetu za mwili hukua vizuri baada ya kupata virutubisho vilivyo sahihi.

Hata hivyo, ulimwengu wa sasa imekuwa kinyume na inavyotarajiwa. Wanadamu wa sasa wanakula kila kitu bila kujali kina madhara gani mwilini. Ikumbukwe kuwa siyo kila chakula kinaweza kufaa kwa ajili ya matumizi ya binadamu. Kila kinacholiwa kinauwezo wa kuingia mwilini lakini kinaweza kuwa hakina sifa ya kuitwa chakula cha binadamu.

Ni sawa na gari, gari linalotumia mafuta ya petrol haliwezi kutembea kwa kutumia maji, japo maji yanauwezo wa kuingizwa kwenye tank la gari hiyo. Ni vitu sahihi tu ndivyo vinapaswa kuingizwa ndani ya miili yetu. Miili yetu ni kama injini ya gari, hivo kutumia vyakula visivyofaa hudhoofisha na kuua seli za mwili na hivyo kuruhusu njia kwa mwili kuvamiwa na magonjwa.

Wito kwa jamii
Jamii inapaswa kuzingatia ulaji wa vyakula sahihi, kushindwa kufanya hivyo tutajenga Taifa na vizazi vya watu walemavu. Tunapaswa kuzingatia matumizi mazuri ya chakula. Wazazi wanapaswa kuhakikisha meza za vyakula zinabeba virutubisho vyote muhimu kwa kiasi kinachotakiwa. Siyo wingi wa chakula kinachotakiwa kuliwa bali ni ubora wa chakula kinachoingizwa mwilini.

Watoto wajengewe desturi ya kuandaa chakula chenye lishe bora kisichoweza kuleta madhara kwa afya ya watumiaji.

Vyakula vinavyoandaliwa viwandani vinapaswa kukaguliwa na kuthibitishwa kwa ubora wa hali ya juu kabla hakijaingizwa kwenye matumizi ya binadamu.

Kumbuka
Mwonekano wako unachangiwa na chakula unachokula, kushindwa kula chakula sahihi kitafanya upate magonjwa kama shinikizo la damu, n.k. ugonjwa wako ni biashara ya watu wengine. Kuwa makini na chaguzi zako za vyakula usije ukawa chanzo cha kipato kwa watu wengine.

Ahsante kwa kufuatilia andiko hili kwa ufupi.
 
Upvote 5
Back
Top Bottom