MWONGOZO: Kupata faili la mgonjwa

MWONGOZO: Kupata faili la mgonjwa

uzeebusara

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2013
Posts
657
Reaction score
514
Habari zenu wana jukwaa
Naomba msaada au mwongozo wa namna iliyobora ya kupata faili la mgonjwa wangu kutoka hospitali.
Ipo hivi, nina mgonjwa ambaye alikuwa anapata tiba specifically masuala ya uzazi kwenye hospitali binafsi. Lakini baada ya kuona vipimo na tiba mbalimbali kutokuwa na mafanikio baada ya muda mrefu, tuliona tucheki hospitali nyingine. Sasa tumepata ushauri badala ya kuanza vipimo upya ni vema tungeenda na faili linaloonyeaha historia nzima ya matibabu ya mgonjwa. Hii hospitali binafsi ya awali imekuwa na changamoto katika kutoa faili kwani toka awali tulikuwa tunaruhusiwa kadi tu ya kuwa tunapata tiba pale. Hatukuwa tunapata nafasi hata ya kununua dawa maduka mengine na kama unavyojua dawa za masuala ya uzazi gharama lkn pale gharama zilikuwa juu sana ila ilibidi kukubaliana na masharti yale.
Kwa sasa nataka kupata hili faili kwenda nalo hospitali nyingine, na sera ya hospitali hii ya awali wanaugumu sana wa kutoa faili ya mgonjwa. Naomba kujua haya
1. Je ni sahihi kuzuia faili la matibabu ya mgonjwa?
2. Kama si sahihi, nitumie njia gani kupata faili ambalo ni haki ya mgonjwa wangu

TAMBUA: Hatudaiwi hata sh mia (100/=) na hii hospitali
Natanguliza shukrani za dhati kama suala langu litapewa mwongozo sahihi
 
File ni mali ya Hospitali!
Kama mlifanya vipimo hivo ndo mnaweza kuomba majibu yake kwa mfano wa Softcopy e.g Hospitali kubwa hapa Dar wanakupa majibu yako ya Xray au CT scan katika CD.

Na kama labda mlifanya Ultrasound mnaweza pewa nakala ya report ya Sonographer.

Hivo hivo kama mlifanya vipimo vya damu mnaweza kuviomba...Hizo ni haki zako!

Lakini Documentations za Daktari alichokua anakitubu na maamuzi alokua akichukua inabaki kuwa mali ya taasisi husika!

Kupewa file la mgonjwa ni sawa na hospitali kujishtaki yenyewe mahakamani maana kwanza umeachia siri za mgonjwa ila pia hilo file linaweza tumika kuishitaki hospitali iwapo uta notsi kitu ambacho hakikua sawa katika matibabu ya mgonjwa wako...Hapa unaweza muajiri hata Daktari mwenye njaa akatafuta weakness kwenye hilo na mkalitumia kuwashitaki mahakamani!

Kamwe piga ua garagaza hautokaa upewe file la mgonjwa na hospitali iliyo smart iwe ya Serikali au ya Private.
 
Nimekuelewa Mkuu
Nashukuru, sasa kupata majibu ya hivyo vipimo mbalimbali ndiyo imekua ngumu mno. Maana nilihitaji kupata nakala hizo kn kipimo kimoja tu ndiyo kilisalia cha CT SCAN ambacho wao pale hawana na walikiri hawana na recommendation ya yuke daktari bingwa akasema tujaribu hospitali zenye huduma hii.
Ntaomba naka hizo, na si faili lote. Asante sana
 
Kiutaratibu file la mgonjwa halitoki nje, ukiona mgonjwa amepata file lake basi ujue ni kwa magumashi, kwa wafanyakaz wasio na maadili. Unachoweza kuomba ni Taarifa ya matibabu(Medical Report).
Asante Mkuu, ntaomba nakala ya taarifa ya matibabu. Kisha nitaleta mrejesho, japi wkt ule tunaendelea na tiba ilikuwa ngumu kutoa kwa sababu kuna wakati pale bei ya dawa ilikua juu mnoo ukilinganisha na pharmacy kubwa 2 nazijua zipo Posta na makutano ya Kkoo na Tandamti (majina kapuni) lkn alikuwa wanakataa kutoa wakisema dawa lazima tutumie zinazouzwa pale pale tu
 
Back
Top Bottom