uzeebusara
JF-Expert Member
- Apr 15, 2013
- 657
- 514
Habari zenu wana jukwaa
Naomba msaada au mwongozo wa namna iliyobora ya kupata faili la mgonjwa wangu kutoka hospitali.
Ipo hivi, nina mgonjwa ambaye alikuwa anapata tiba specifically masuala ya uzazi kwenye hospitali binafsi. Lakini baada ya kuona vipimo na tiba mbalimbali kutokuwa na mafanikio baada ya muda mrefu, tuliona tucheki hospitali nyingine. Sasa tumepata ushauri badala ya kuanza vipimo upya ni vema tungeenda na faili linaloonyeaha historia nzima ya matibabu ya mgonjwa. Hii hospitali binafsi ya awali imekuwa na changamoto katika kutoa faili kwani toka awali tulikuwa tunaruhusiwa kadi tu ya kuwa tunapata tiba pale. Hatukuwa tunapata nafasi hata ya kununua dawa maduka mengine na kama unavyojua dawa za masuala ya uzazi gharama lkn pale gharama zilikuwa juu sana ila ilibidi kukubaliana na masharti yale.
Kwa sasa nataka kupata hili faili kwenda nalo hospitali nyingine, na sera ya hospitali hii ya awali wanaugumu sana wa kutoa faili ya mgonjwa. Naomba kujua haya
1. Je ni sahihi kuzuia faili la matibabu ya mgonjwa?
2. Kama si sahihi, nitumie njia gani kupata faili ambalo ni haki ya mgonjwa wangu
TAMBUA: Hatudaiwi hata sh mia (100/=) na hii hospitali
Natanguliza shukrani za dhati kama suala langu litapewa mwongozo sahihi