Mwongozo ukoje kuhusu kupima HIV/AIDS?

PAZIA 3

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
1,102
Reaction score
1,919
Nashindwa kuelewa,saivi kuna utaratibu wa kupimwa HIV kabla hata hujaenda maabara,nasikiasikia tu kuwa ni mwongozo wa serikali,je hii ni kweli,au ni huku tu nilipo mimi?
 
Nashindwa kuelewa,saivi kuna utaratibu wa kupimwa HIV kabla hata hujaenda maabara,nasikiasikia tu kuwa ni mwongozo wa serikali,je hii ni kweli,au ni huku tu nilipo mimi?
Sasa zaidi ya maabara, vipimo vinatolewa wapi?

Sema saivi kila anayehudhuria hospitali za umma lazima aulizwe status yake ya maambukizi then anashawishiwa kupima tangu anapomuona daktari ili akikubali vile akienda maabara tu wamuunganishie.
 
Sasa zaidi ya maabara, vipimo vinatolewa wapi?

Sema saivi kila anayehudhuria hospitali za umma lazima aulizwe status yake ya maambukizi then anashawishiwa kupima tangu anapomuona daktari ili akikubali vile akienda maabara tu wamuunganishie.
Ninachokizungumza sijasimuliwa,yaan ukitoka mapokezi,ukienda kwa docta kuelezea,kabla hajakwandikia kwenda maabara,anachukua damu,na reagents za HIV test anazo hapohapo mezani,wala hakuandai,ukitoka maabara anakwambia,afya yako nzuri,au la ,kisha anasoma majibu ya maabara
 
Ila kwa utaratibu huo,nahisi,kunahatari ya watu kukimbilia pharmacy na kununua dawa,lazma serikali iwe wazi,iwajuze wananchi kuwa,kwasasa kupima HIV ni compasary,ili wajiandae kisaikolojia
 
Again serikali yetu kama ni hivi haya ni makosa,kupima HIV ni hiyari ila its a right thing to do,na elewa kuwa vipima HIV UNAWEZA KUNUNUA KWENYE PHAMANCY,unajipima mwenyewe kama vipimo vya mimba kwa KE,ILA kabla hujafanya hivi please jiandae kisaikolojia,na sioni sharia yeyote inayomlazimisha mtu kupima HIV,mambo mengine tuamke ndugu zangu watanzania,elewa haki yako ,wajibu wako kisheria.
 
Sasa zaidi ya maabara, vipimo vinatolewa wapi?

Sema saivi kila anayehudhuria hospitali za umma lazima aulizwe status yake ya maambukizi then anashawishiwa kupima tangu anapomuona daktari ili akikubali vile akienda maabara tu wamuunganishie.
PITC(health provider initiative test councelling)big up.
 
alipaswa kukushauri kabla ya kufanya/kuchukua vipimo. nawe kwanini uliliruhusu kufanyiwa hivyo nakuja hapa jukwaani umefanya makosa.(siku nyingine sio kupima maambukizi pekee hata kama kupima malaria panahitaji ridhaa yako utaki utopimwa.
 
Ni kweli ni Sera ya shirika la Afya duniani (WHO) kwa sasa, na imekuwa adopted na taifa letu pia. WHO ina malengo kuwa kufikia mwaka 2020 ,90% ya watu wawe wanafahamu hali yao ya maambukizi ya VVU, na kati ya hao 90% wawe wameshaanza matibabu ya ARV, na kati ya hao 90% dawa ziwasaidie kuimarisha kinga zao za mwili. Wameanzisha program ya "PROVIDER-INITIATED TESTING AND COUNSELLING", miaka kadhaa iliyopita ,yaani unapofika tu kituo cha afya, mtoa huduma yeyote aliyekuwa licenced (DAKTARI,MUUGUZI,MTEKNOLOJIA WA MAABARA N.K) anatakiwa akushauri kuhusu faida za kujua hali yako ya maambukizi, akueleze faida zake,aandae namna ya kukusaidia kwa majibu yatakayotokea baada ya kupima,ukikubaliana basi atakupima na utaambiwa hali yako ya maambukizi ndani ya dakika 10 hadi 20 na hii inaweza kufanyika sehemu yeyote kama wodini, chumba cha kumuona Daktari nk., Kama majibu yataonyesha ni mwathirika utaanza darasa la dawa (ADHERENCE SESSION), utafanyiwa vipimo vya figo na ini na kwa mujibu ya mwogozo mpya wa WHO ndani ya wiki mbili utaanza matumizi ya ARV bila kujali kiwango chako cha CD4, wala Clinical stage. Kama majibu yataonyesha hauna maambukizi, utashauriwa urudi baada ya miezi mitatu kuhakikisha hali ya maambukizi na utapewa elimu namna ya kujizuia usipate maambukizi
NB:Mtoa huduma hatakiwi kukupima kwa siri au bila wewe kukubaliana (consent), ni kinyume na maadili ya taaluma.
 
Sio kwamba wanakupima Malaria?Kuna siku nlimpeleka mtt wa Sister hospitali ilikuwa Usiku, kufika mapokezi yule mdada akampimia hapo hapo na kile kipimo kinafanana kama cha HIV,mm sikujua tulivyotoka nkamwambia heeee kwann wanakulazimisha kukupima Ukimwi,akanambia hapana mamy ni Malaria hyo
 
Sidhani kama ni sahihi kupima HIV bila ruhusa ya muhusika!
 
 
Nadhani kuna haja ya wizara kuweka wazi swala hili,imenibidi nimtafute rafiki yangu ambae ni docta pia amenidhibitishia hilo,kuwa ni mwongozo mpya wa wizara, wakati mwingine eti wanatumia CBC/FBC ili wajue wapi pa kuanzia,lengo ni kujuwa kiwango cha white blood cells,duh,kwa utaratibu huu,takimwi itaongezeka kutoka 225, hadi 500, wanaoambukizwa kwa siku moja
 
Hiyo approach tu ndo imeenda kushoto kido coz informed concert kwenye Huduma za afya ni lazima. Wengine tunajijua hari zetu so ukipima afu ukakuta nipo +ve bila concert ni kosa. Ila kwa sasa kila client anayevisit hospital lazima aulizwe status yake na ashawishiwe kupima, akigoma basi
 
Wamebuni mbinu mpya ya kuongeza wateja wa dawa zao...!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…