JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani (WHO), Mtoto anapaswa kuanza kunyonyeshwa saa moja baada ya kuzaliwa hii husaidia maziwa ya mama kuweza kutengenezwa kwakuwa mtoto anapowekwa kwenye kifua cha mama huchochea Hormones zinazozalisha maziwa.
Pia husaidia mtoto kupata choo cha mwanzo ambacho huondoa maumivu ya tumbo kwa mtoto
Mtoto anatakiwa kunyonyeshwa maziwa ya Mama pekee kwa kipindi cha miezi 6 na baada ya hapo ndipo ataongezewa vyakula vya ziada kwakuwa wakati huo maziwa ya mama hupunguza virutubisho.
Mtoto ataendelea kunyonyeshwa mpaka kufikia miezi 24 au miaka miwili hii husaidia kumkinga mtoto na magonjwa kama utapiamlo