#COVID19 Mwongozo wa Serikali ukoje kuhusu kuzika wafu waliofariki kwa Covid-19?

#COVID19 Mwongozo wa Serikali ukoje kuhusu kuzika wafu waliofariki kwa Covid-19?

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Wadau hakuna mahala unaweza kupata updated info kama Jf.

Wadau mwenye info kamili atujuze kwa sasa utaratibu uko vipi kuzika mtu aliyefariki kwa covid-19.

Ifahamike kwa sasa vifo ni vingi sana uraiani na vina ukaribu na matatizo ya kupumua.

Nawakalishe mimi Idugunde
 
Na utakuwa unaushahidi gani kama ni uviko 19?hivi watanzania akili za namna hii tutaziacha lini🙄
 
Na utakuwa unaushahidi gani kama ni uviko 19?hivi watanzania akili za namna hii tutaziacha lini🙄
Huyu jamaa ni tahira.Halafu serikali ipo wazi kabisa kwenye ishu ya Corona kuwa ni jambo ambalo siyo la msingi kwao na hawana time nalo ndiyo maana serikali ndiyo inayoongoza kwa kusababisha mikusanyiko,haina time na wananchi kusababisha mikusanyiko,watu wakifa wanazikana tu kiholela bila ya miongozo,hakuna mass testing,hakuna law enforcement ya wasiochukua tahadhari na kadhalika halafu jamaa anakuja na uzi wa upupu kama huu.

Halafu siku zote serikali ambazo hazina kibali cha wananchi kama Serikali ya Tanzania ambayo imeingia madarakani kwa wizi wa kura siyo responsible government.Kwa hiyo ni jambo la kushangaza sana kuona mtu anailaumu au kuishangaa serikali ya Tanzania kutokujishughulisha na janga la Corona wakati anajua kabisa kuwa ni serikali ambayo haina wajibu kwa wananchi kwa sababu haina kibali cha wananchi.
 
Jamaa kuandika jambo la msingi sana halafu nashangaa watu wanamzodoa. Corona ipo sana, watu wengi wanaumwa na wanakufa. Hata maswali ya eti unauhakika gani kwamba ni corona ni maswali ya kijeuri tu. Subiri ikugonge ndiyo utaamini. Misiba ni shughuli ya mikusanyiko na hivyo ni vyema kwa wakati huu serikali ingetoa miongozo flani.
 
Watanzania ni watu wa ajabu sana
 
Mkuu labda nikuambie tu kama ulikuwa hujui mimi ni muhanga wa hili janga la corona tayari nimeugua karibu mara mbili lakini naamini huko miaka ya nyuma huu ugonjwa uliwahi kuwepo ingawa ulikuwa hauzungumzwi labda tulikuwa tunaujua kwa jina lingine lakini maisha yaliendelea na bado tunaendelea kuishi

Nikikujibu hoja yako ni kwamba nakubaliana na wale wote juu ya uwepo wa huu ugonjwa katika kuungana na mataifa ya wenzetu lkn kitendo cha kutaka kuishi kwa hofu na kuendeleza habari za ugonjwa huu kana kwamba magonjwa mengine hayapo au hayauwi hapo ndipo ninapokinzana na nyinyi[emoji849]mbn hapa katikati kama mtakumbuka maisha yaliendelea kama kawaida na hatukusikia cha maiti kutupwa kama ambayo wenzetu walitutabiria na badala yake maisha yaliendelea sasa embu mniambie hakukuwa na vifo huko majumban na mahospitali?

Njia pekee ni kukuukubali kuwa ugonjwa upo sawa tuuzoeee kwakuendelea kutumia njia zile zile zilizofanikisha awamu ya kwanza na tuuuwishi huu ugonjwa kama tunavyouwishi magonjwa mengine kama ukimwi,kansa etc...

Mwisho japo si kwa umuhimu naomba unijibu ile serikali iliyotuambia chanjo sio nzuri ni biashara tu na serikali ile ilikwenda mbali kwa kutuambia hata zile barakoa zao tuzichunguze maana kuna zingine zimepandikizwa virusi ile ilikuwa ni serikali ya chama gani kam ni hii viongozi wao si ndio hawa wanatumia nguvu kubwa kutuambia chanjo ni bora?
 
Back
Top Bottom