Mwongozo wa ufugaji wa kisasa wa Mbuzi wa nyama na maziwa


nayajua karibu mashamba yote ya ukanda huu wa ziwa na kati...ila nilisikia hawa wanyama wanastawi sana ktk baridi...ndo maana nikauliza!! na kumbuka mbegu bora inabidi uchanganye kidogo(kama ulivnielezea)!!
 
[/QUOTE]
Mkuu Kasopa asante kwa huu uchanganifu! Je unaweza kutufafanulia kuhusu gharama za sh. 500,000/= kwa ujenzi wa banda. Hii ni gharama nafuu sana kwa banda la ng,ombe.

Pamoja!
 
nayajua karibu mashamba yote ya ukanda huu wa ziwa na kati, ila nilisikia hawa wanyama wanastawi sana ktk baridi...ndo maana nikauliza!! na kumbuka mbegu bora inabidi uchanganye kidogo(kama ulivnielezea)!!

Kweli,watu wengi wanaamini hivyo,mwanzoni ilisemekana huwezi kufuga ng`ombe mikoa ya kusini,siku hizi kuna ng`ombe kibao (mfano ni hawa waliotoka Ihefu mbeya,wapo Mhoro Lindi kibao na Wamasai wanauza maziwa pale Somanga/Muhoro kama kazi). Gharama za kutunza ktk ukanda wa joto ni kubwa kuliko ukanda wa baridi. Kwa hiyo wewe tafuta crossbreed na ufuge kwa kufuata maelezo ya watalaamu wetu.

Nakutakia kila lililo jema ktk azma yako hiyo.
 

appreciation for the knowledge!!
 
Wewe hilo neno umelisema simposimpo tu, lakini liko BOLD sana. Coment zingine haziko vizuri.

Mtu anatangaza ana dola milioni moja hapa jukwaani - mimi nadhani huo ni utani, ndio maana nikamtania kwamba ni fisadi. Nikiwa na fedha kiasi hicho kweli sitakitaja hadharani.
 
Mtu anatangaza ana dola milioni moja hapa jukwaani - mimi nadhani huo ni utani, ndio maana nikamtania kwamba ni fisadi. Nikiwa na fedha kiasi hicho kweli sitakitaja hadharani.
Kumbe ulikuwa unatania. This is a business forum! Anatafuta runch, wewe unadhan atapata vp bila kuwatangazia wadau? sioni ubaya wa kuweka bei yake ya mwisho! kwani bilioni ni mafisadi tu ndy wanakuwa nazo? inategemea na ukubwa wa mradi, hiyo ni 10% tu ya gharama nzima ya mradi! Mali utaipata shambani baba! Kuna wamasai manamiliki ng'ombe 20,000.
 

Hapo peusi pa kwanza ilikuwa jibu tosha. Lakini hayo mekundu.
 
Mimi ni mfugaji wa ng'ombe wa Maziwa, kwa sasa ninao ng'ombe 5 wa maziwa. Mpango wangu ni kuwa na shamba lenye ng'ombe wasiopungua 100. Katika kufikia lengo hili napata wazo la kutafuta mkopo na kwa kuanzia nafikiria mkopo wa Millioni 10. Kwa sasa banker wangu ni Backlay's, lakini kwa muda mrefu wamesimamisha mikopo binafsi yenye mashariti nafuu.

Hivyo kama kuna mwanajamii mwenye idea ya wapi (Taasis) naweza kupata mkopo huu. Benki nyingi wana ahadi, lakini utekelezeja wake bado nahisi ni mgumu.
 

Kwanza, ningekushauri kuwa na mchanganuo wa kazi hii ya ufugaji, kwa sababu kama target ni kuwa na ng`ombe zaidi ya 100,unastahili kusajili shamba lako ili upate mikopo ya kuliwezesha kuwa na uzalishaji wenye faida. Na milioni kumi si kidogo kwa kuanzia ila kwa shamba zuri ni kidogo. Jaribu Twiga bancorp. benki hii bado ni mali ya serikali.

Zaidi sana big up mkuu.
 

Nimefanikiwa kusajili shamba (EBENEZER DAIRY FARM) tokea nilipoanza 2008, sasa huu mkopo ninaotafuta ni pamoja na kuweza kununua shamba na kuongeza ng'ombe. Kwani kwa sasa ninafanya ZERO Grazing, lakini idadi ya ng'ombe itakapofikia 10 nitahitaji kuhamia shambani. Kwa sasa nipo Zanzibar na TWIGA BANCORP hawajafungua tawi. Kuhusu mchanganuo wa mradi, hili nitahitaji mtaalamu.
 

Vizuri sana mkuu, nimekiona kibao kinachoelekeza kwenye shamba lako. Juzi nilikuwa katika pitapita zangu za kutafuta mashamba. Nakushauri uwaaproach CRDB au NMB nadhani wanasaidia. Najua CRDB wamewasaidia wengi sana kwenye sekta ya ufugaji (Mkuza Chicks ni mmoja wa watu walioinuliwa sana na CRDB).

Kila la kheri
 

Mkuu komaa mpaka ufanikiwe kupata mkopo, jifanye hujali, hata hizi benki ndogo pitia,unaweza kukutana na meneja mzuri akakutoa.
 

Jaribu stanbic pia nimesikia wameanza kutoa personal loans kwa wafanyakazi, kila laheri mkuu
 
Ninao usghauri mzuri kwako mkuu,unaweza kupata mkopo nafuu kwa riba nafuu kwa kutumia SACCOS. Ingawa saccos nyingi haziaminiki. Ungekuwa hapa Dar es salaam. Ningependekeza baadhi ya Saccos unazoweza kujiunga nazo. Hasa ukizingatia unahitaji shilingi milioni 10 hizi ni fedha ambazo unaweza kupata kwa kutumia SACCOS.Hata hivyo benki pia ni mahala muafaka.USIKATE TAMAA MPAKA KIELEWEKE.
 
Nashukuru Mkuu kwa Ushauri wako, unaweza kupendekeza trusted SACCOS zilizopo DAR ili niweze kuwasiliana nao na kuona uwezekano wa kujiunga.
 

WANA-JF, kwa yeyote aliye na Sample ya Mchanganuo wa Biashara naomba anitumie.
 

Mimi bado sijafanikiwa kununua Shamba huenda umeona Shamba ambalo limesajiliwa kwa jina hilo, lakini Mimi usajili wangu nimefanyia hapa Zanzibar. Katika Mkopo ninao tafuta ni pamoja na kuniwezesha kununua Shamba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…