- Thread starter
- #61
Nilifanikiwa kupata mbegu ya mbuzi wanaozaa pacha,nikaona hii ndio mbegu nzuri, mara ya kwanza alizaa pacha nikafurahi sana,mara ya pili amepiga watatu triplets nikamshukuru Mungu, leo nimekwenda kwa yule mzee aliyeniuzia kumpa feedback nikiwa mabega juu kwa kupata triplets, nikashangaa yeye mbuzi wake amezaa watoto watano kwa mkupuo mmoja.
Tamaa mbaya, lakini nimemwomba aniuzie vile vitoto vyote vitano, nasubiri jibu.
Wakuu njooni tufuge. Inalipa, ukienda maonyesho ya wakulima au saba saba ndio utajua nini kinaendelea ktk ulimwengu wa mifugo.