Kaka malila habari za siku.
Mi nimefurahi sana na hii kitu na ninakumbuka ulivyoniambia siku ile tulipoonana. wale samaki vipi kaka mabwawa tayari?
umefanya ile taratibu ya kusajili ile miti kule Mufindi?
Halafu kaka ukipata mda nenda pale ofisi za UN dsm kitengo cha mazingira wape habari juu ya jitihada zako za kupanda miti kaka kuna pesa palekwa ajili ya project kama hizi.
Tutaonana nikirudi maana niko hadelanda oslo norway kwa hawa waheshimiwa wa ile kampuni yetu. narud tar 26 mwezi huu.
Mungu akutangulie!! hivi mbuzi unawafugia pale mkuranga sio?
Nilifanikiwa kupata mbegu ya mbuzi wanaozaa pacha,nikaona hii ndio mbegu nzuri, mara ya kwanza alizaa pacha nikafurahi sana,mara ya pili amepiga watatu triplets nikamshukuru Mungu, leo nimekwenda kwa yule mzee aliyeniuzia kumpa feedback nikiwa mabega juu kwa kupata triplets, nikashangaa yeye mbuzi wake amezaa watoto watano kwa mkupuo mmoja.
Tamaa mbaya,lakini nimemwomba aniuzie vile vitoto vyote vitano,nasubiri jibu.
Wakuu njooni tufuge. Inalipa,ukienda maonyesho ya wakulima au saba saba ndio utajua nini kinaendelea ktk ulimwengu wa mifugo.
Kaka Malila nikupate wapi nami uniuzie hao mbuzi, hata wawili nami nipate kianzio?
'one fo ze rooooooodddd'!!!!kama upo dar nenda pale mandela rd just after tazara area ,kuna wizara husika watakupa ushauri mzuri wa mbegu bora ya ng'ombe wa maziwa,na pia how to's za kufuga,ila fahamu kufugia cows in dar ni gharama sana na inachukua muda wako mkubwa,kwani majani ni ya kununua ,bora ufugie mkoa wa pwani,eg kibaha,chalinze ,or mkuranga, siyo mbali sana na dar and u can transport maziwa yako kila siku kuliko kufugia dar na kuwa na headache ya malicho ya hao wanyama
kama kuna wanaopenda kufuga wanyama hasa mbuzi ( wa maziwa,nyama),njooni tuunganishe nguvu tufanye mambo.inawezekana kabisa tukafuga kwa mafanikio sana. Kila kitu kipo ndani ya uwezo wetu.
I believe together we can go.
mkuu malila. .., nimefuatilia badizzo Arusha kama ulivyo hitaji itatumwa soon na hii itakuwa free for use to any jf member who wishes to use it. ... starting from you
tupo pamoja jf
<br />Jina la kisayansi la mitiki ni lipi wadau?
mkuu malila. .., nimefuatilia badizzo Arusha kama ulivyo hitaji itatumwa soon na hii itakuwa free for use to any jf member who wishes to use it. ... starting from you
tupo pamoja jf
Kaka, kwa ufupi.
Ng'ombe wanaofaa ukanda wa joto ni wale wasio na rangi nyeusi. pili uchague aina kulingana na outcome unataka nini mwisho wa siku (beef,diary, dual).
Kuna aina wanaitwa Ayrshire wanaweza kustahimili maisha ya pwani(coastal belt) na magonjwa yake. unatakuwa upate kizazi cha pili na cha tatu ikienda cha nne au pure breed uekwama kuna ugonjwa unaitwa ECF (east cost Fever) lazima ukutoe.
Uzuri wa breed hii unaweza kwenda mpaka 15Lts na butter fat content ikiwa 3.
The best ni breed inaitwa jersey kikubwa anahitaji eneo dogo,chakula kidogo pia anaweza kustawi pwani.kanuni ileile usiende kizazi cha nne.
hawa ni maziwa yenye thamani kubwa ila volume ndogo, kwa wahuni tuna wa kross jike la ayshire na dume la jersey matokeo yake hatta kwa 2M sikuuzii ila akiwa jike.
Kuna breed nyingine wanaitwa kitukama simentor(Dual) hawa ni maziwa na nyama, wastani wa lita 8, chakula kibao ila sometimes wana ishu ya kubeba mimba baada ya mzao wa kwanza(hapo uwe mvumilivu una weza chukua mwaka kumpandisha).
Breed zingine mapambo ya kimasai, karibu shamba
Mkuu malila, nimefuatilia badizzo Arusha kama ulivyo hitaji itatumwa soon na hii itakuwa free for use to any jf member who wishes to use it. ... starting from you
tupo pamoja jf
Mkuu salama,Kweli nimeamini " OLD IS GOLD" Huu uzi bado una manufaa makubwa. Malila Tunaomba utupe mrejesho wa mambo yafuatayo:
Asante sana kaka, kila nisomapo michango yangu huwa nina farijika sana. Na sababu ni kwamba hii platform ya bwana Max inatuwezesha kupata information zenye thamani kubwa bila taabu yeyote.
- Mbuzi wa maziwa pamoja na uzao wake, unaendeleaje? tuliopo Dar tutapataje hiyo mbegu?
- Bwawa la samaki na lenyewe vp?
- Safari ya kule morogoro imefikia wapi ili tuanze kujiandaa mapema?