Mwongozo wa ufugaji wa kisasa wa Mbuzi wa nyama na maziwa


Sasa mleta mada unataka akufundishe mpaka namna ya kulinda mifugo yako?
 

Kwa mbuzi 50 unatakiwa uwe na eneo la ukubwa gani la kuwalishia?
 
Hawa mbuzi ni mbuzi bora walioboreshwa, wanapatikana dodoma. Ni matokeo ya cross breed iliyofanyika kati ya mbuzi wa kienyeji wa dodoma na exotic breed.Hivyo wengi wa uzao wao huzaa mapacha. Mbuzi hawa huuzwa tsh elfu 50, wakiwa na umri wa miezi 5.

Mkuu unaweza kuelekeza Vzr ni DODOMA sehemu gani wanapatikana hao Mbuzi? ikibidi mawasiliano yao! Nadhani utakuwa umesaidia wengi wanaopita humu JUKWAANI cmbaya pia naww ukiweka mawacliano yako km hutajali
 
Kama una mtu uganda wanaoatukans kwa wingi tu ni hela yako tu
 
Kuwa na mabanda ya mbuzi yaliyo inuliwa hakuchangiwi na magonjwa hatari yanayo_wasumbua?
 

Mkuu kweli wewe ni hazina kwangu. Nipo kwenye mandalizi ya mipango ya ufugaji wa kuku na hao mbuzi. Nikiwa tayari nitakusumbua sana mkuu. ingawa kwenye kuku nimeanza mdogomgogo.
 
Mkuu kweli wewe ni hazina kwangu. Nipo kwenye mandalizi ya mipango ya ufugaji wa kuku na hao mbuzi. Nikiwa tayari nitakusumbua sana mkuu. ingawa kwenye kuku nimeanza mdogomgogo.
Ndandidzi,
Usijari mkuu, tuko pamoja chochote utakachokwama au kuhitaji kufahamu kuhusu ufugaji wa kuku na mbuzi nijulishe nitakusaidia.
 
Kuwa na mabanda ya mbuzi yaliyo inuliwa hakuchangiwi na magonjwa hatari yanayo_wasumbua?
Pamoja na kuzuia kuenea kirahisi magonjwa, Ki tabia mbuzi huhitaji kulala kwenye mabanda yaliyoinuliwa juu,hawapendi kulala chini kama ilivyo kwa ng'ombe.Vilevile mbuzi hawapendi mvua,ukiona mvua inakaribia kunyesha ni muhimu mbuzi wakarudishwa haraka bandani kwao.
 
Ni kweli kwamba ukiwa na beberu mwenye asili ya uzao wa mapacha basi hata majike atakaowapanda watazaa mapacha hta kama hawana asili ya kuzaa mapacha?
 
Mkuu mimi nipo kwenye hatua za mwisho ktk maandalizi ya ufugaji. Nimeplan nianze na kuku baadae nguruwe na hata hao mbuzi make ni rahisi sana kuwafuga.

Shida yangu mimi ni kujua ni umbali gani natakiwa kutenganisha mabanda yao hawa mifugo ili kusiwe na muingiliano wa magonjwa iwapo nitawafuga wote katika eneo moja hasa nikiwa na maana ya kuhimili ulinzi na monitoring ya maendeleo yao?
 
Zanstan asante sana kwa kujitoa. Mungu akubariki. Naulizia gharama ya kusafirisha hao mbuzi hamsini ni kutoka Dodoma kwenda wapi? Dar itakuwa kiasi gani? Asante sana
 
Zanstan asante sana kwa kujitoa. Mungu akubariki. Naulizia gharama ya kusafirisha hao mbuzi hamsini ni kutoka Dodoma kwenda wapi? Dar itakuwa kiasi gani? Asante sana

Mama Joe Karibu sana mjasiria Mali, hiyo bei ni kutoka dodoma hadi Dsm
 
Vipi kuhusu kondoo? Je kuna tofauti yoyote kati ufugaji wa Mbuzi na Kondoo? Je, ufugaji wa Kondoo hauna tija kibiashara kama ule wa Mbuzi?

Asante!
 
Vipi kuhusu kondoo? Je kuna tofauti yoyote kati ufugaji wa Mbuzi na Kondoo? Je, ufugaji wa Kondoo hauna tija kibiashara kama ule wa Mbuzi?

Asante!
MahinaVeterani,

Ufugaji wa Kondoo hauna tofauti na ufugaji wa mbuzi na ndio maana jamii nyingi huchanganya pamoja wanyama hawa wakati wa kufugwa kwao. Kondoo na Mbuzi hushabiana kwa mambo mengi sana lakini lililokubwa ni kuwa wote mimba zao huchukua miezi 5 toka kushika mpaka kuzaa.Pia magonjwa anayopata Kondoo ndiyo hayo hayo anayopata Mbuzi.

Kuhusu masoka ni tabu kidogo ukilinganisha na nyama ya mbuzi,kama unavyojua jamii yetu si watu wengi sana wanaopendelea kula nyama ya Kondoo ukilinganisha na nyama ya mbuzi. Mara nyingi masoko ya Kondoo hupatikana kwenye Mahoteli makubwa.
 
Zantsan nashukuru kwa bandiko hili

Nikiangalia mbuzi zaidi ya 200 naona uhitaji wa shamba kubwa sana ambalo si rahisi kupata dar.
Pengine hapo ndio penye gharama kubwa.

Ninakusudia kuanzisha mradi wa kufuga mbuzi tatizo langu ni eneo....
Pia nasikia ukifuga mbuzi maeneo jirani na Dar kuna wezi huwa wanaweza kuvamia na kukomba mbuzi wa kutosha maana kuna soko.

Mashamba yanapatikana mikoani shida inakuja kwamba bei ya mbuzi mikoani iko chini.....ukitaka kuwauza Dar inabidi kuweka gharama ya usafiri.

Kimsingi ninatatizwa sana ingawa mtaji wa kuanzia tayari ninao

Sijui kama una uzoefu wowote kuhusu hofu zangu!!
 
Last edited by a moderator:

RealMan,

Kuhusu wezi ni tatizo ambalo linaweza kudhibitika. Namna gani utadhibiti wezi ni kuwa lazima uajiri mlinzi ambaye atakuwa anakulindia wakati wa usiku, kama unavyojua huu ni mradi na unahusisha pesa nyingi za uwekezaji hivyo ni muhimu wakati unapanga bajeti ya huo mradi wako ukajumuisha gharama za mlinzi.

Kuhusu kufugia mikoani hakuna shida yeyote kwani wakati wa kuuza utakodi canter na utawapakia mbuzi wako tayari kuwapeleka sokoni Dar au kwenye miji mikubwa. Gharama za usafiri ni ndogo sana kwa kila mbuzi na mara nyingi huwa haizidi tshs. 5000/=

Kama utaona kufugia mikoani kutaongeza gharaza za usafiri au labda siyo mzoefu kwenye usafirisha wa wanyama na kwenda kuwauza Dar unaweza ukatafuta shamba Mkuranga au Babagamoyo ambako wafugaji wengi nimewasaidia kuwaanzishia miradi yao ya mbuzi na Kuku huko na kwamba hali ya usalama ni kubwa tu ukilinganisha na maeneo yaliyo jirani zaidi na Dar.
 
Hawa mbuzi ni mbuzi bora walioboreshwa, wanapatikana dodoma. Ni matokeo ya cross breed iliyofanyika kati ya mbuzi wa kienyeji wa dodoma na exotic breed.Hivyo wengi wa uzao wao huzaa mapacha. Mbuzi hawa huuzwa tsh elfu 50, wakiwa na umri wa miezi 5.

Huko Dodoma wamejaa tele kila kona ama unawafuata wapi?

Contacts?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…