mokala1989
JF-Expert Member
- May 4, 2013
- 2,236
- 728
Asante, mimi sijatokea SUA, ila SUA huwa napita kwa watalaam kuchota ujuzi.
Kila la heri mkuu!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante, mimi sijatokea SUA, ila SUA huwa napita kwa watalaam kuchota ujuzi.
Wenzangu bado wako Kitonga comfort Hotel wanakula, mimi niko mlimani namalizia kupanda mlima, niko na dogo mmoja tunamalizia mlima kitonga. Wenzetu wakimaliza kula watatukuta Ilula kama tutaamua kusimama, ila tumekubaliana na dogo, break ya kwanza Tunduma. Pale tutapumzika kisha tuvuke mpaka.
Karibu sana, safari ni ndefu, ina miiba na kiu, njaa kali ipo.Ila ukifika Tunduma kila kitu bwelele.
Kama kuna wanaopenda kufuga wanyama hasa Mbuzi ( wa maziwa,nyama),njooni tuunganishe nguvu tufanye mambo.Inawezekana kabisa tukafuga kwa mafanikio sana. Kila kitu kipo ndani ya uwezo wetu.
I believe together we can go.
Kutokana na ungezeko la watu kuongezeka kwa kasi na wengi kutokuwa na ajira.Je usalama wa mbuzi hao 50 utaufanikisha vipi kutokana na majambazi wa sasa?
Dah, wewe unahofia Majambazi? kama kila mtu angekuwa anaogopa leo hii hata uvumbuzi usingekuwepo, achilia mbali Ujambazi kuna watu wamekufa wakati wanatest uvumbuzi wao, nisha wahi kuweka list ya wavumbuzi walio kufa wakati wanatest kazi yao.
Ukiogopa hakika huwezi fanya chochote kile katika maisha yako
Kwa mara nyingine tena, leo nimeona haja ya kuanzisha mada nyingine na tujadiliane kwa pamoja juu ya ufugaji wa mbuzi baada ya kujadili kwa muda mrefu ile mada ya ufugaji wa kuku.
Ufugaji wa mbuzi hapa Tanzania ni fursa adhimu ambayo Watanzania wengi hawajaiona. Ni ufugaji ambao wenyewe kama mfugaji atazingatia kanuni na misingi ya ufugaji Bora, ni rahisi sana mfugaji kujiondoa kutoka kwenye umasikini na kuwa tajiri. Kitu cha msingi na muhimu ni kwamba,mfugaji lazima awe na eneo pamoja na mtaji wa kuanzia.
Mbuzi wanatakiwa kufugwa shambani. Shamba ambalo mbuzi wanatakiwa wafugwe linapaswa liwe na sehemu ambayo mbuzi wanaweza kwenda kuchungwa na pia kuwe na chanzo cha maji. Mbuzi kitabia hupenda kulala juu hivyo mabanda yao yanapojengwa lazima yainuliwe juu. Mabanda ya mbuzi si ghari,kwani hujengwa simple.
Mbuzi kwa mwaka wao huzaa mara mbili na ukipata ile mbegu ya wanaozaa mapacha faida yake huwa ni kubwa zaidi, itategemea na mtaji wa mfugaji, lakini kama mfugaji ataweza kuanza na mradi wa mbuzi 50 inakuwa vizuri zaidi. Ukiwanunua mbuzi 50@ tsh.50,000/= utapata Milioni 2 na nusu, madume 2 kila moja likanunuliwa kwa tsh 75000/= kwa madume mawili itagharimu tsh laki moja na nusu. Usafirishaji wa mbuzi hauzidi laki tatu na nusu. Kwa hiyo itajikuta ukiwa na milion 5 utaweza kuanza na mradi wa ufugaji wa mbuzi majike 50 na madume mawili,pamoja na kuwajengea sehemu ya ya kulala.
Kama nilivyoainisha hapo awali, mbuzi kwa mwaka wao huzaa mara 2, hivyo kama kila mbuzi atazaa hebu chukulia kila mbuzi atazaa mbuzi mmoja tu, ingawa kuna wengine watazaa mapacha hasa ukipata ile mbegu ya mbuzi wanaozaa mapacha, mwishoni mwa mwaka utakuwa na idadi ya mbuzi 100 wapya waliozaliwa na ukujumlisha na mtaji ule wa mbuzi 50 utakuwa na jumla ya mbuzi 150, hii ni ndani ya mwaka mmoja, pata picha utakuwa na mbuzi Idadi gani baada ya miaka 3 hasa ukizingatia kuwa wale watoto wa mbuzi watakapofikia miezi 8 utaanza kuwapandisha nao watazaa nk. Ili kufikia malengo, inashauriwa kuwa mbuzi wa mtaji wanaonunuliwa lazima wawe na umri mmoja ili kusudi waweze kupata mimba kwa wakati mmoja na waweze kuzaa kwa wakati mmoja pia.
Magonjwa ya mbuzi mengi yanafahamika na ni rahisi kudhibitika,hivyo mbuzi si rahisi kufa hovyo.
Toka mbuzi anapata mimba mpaka anazaa,hutumia muda wa wiki miezi mitano yaani siku 150.
Kwa sababu hili pia ni eneo langu nilililolisomea, nawaruhusu kwa wale wote wenye Interest na uanzishaji wa Mradi huu wa ufugaji wa mbuzi kuuliza swali lolote lihusulo ufugaji bora wa mbuzi nami nitajibu.Lengo likiwa ni lile lile la kusaidiana kama Watanzania ili kuondokana na hili lindi la umasikini.
Karibu kwa majadara.
Malamsha,ahsante mkuu kwa mada nzuri ila hapo kuzaa mara 2 kwa mwaka nina mashaka kidogo sababu kama anabeba mimba miezi 5 je, mwezi mmoja baada ya kuzaa atabeba nyingine? Hapo nina mashaka kidogo naomba maelezo kidogo mkuu.
Hawa mbuzi ni mbuzi bora walioboreshwa, wanapatikana dodoma. Ni matokeo ya cross breed iliyofanyika kati ya mbuzi wa kienyeji wa dodoma na exotic breed.Hivyo wengi wa uzao wao huzaa mapacha. Mbuzi hawa huuzwa tsh elfu 50, wakiwa na umri wa miezi 5.Wanapatikana wapi hao wanaozaa mapacha?
TP Mazembe,Kutokana na ungezeko la watu kuongezeka kwa kasi na wengi kutokuwa na ajira.Je usalama wa mbuzi hao 50 utaufanikisha vipi kutokana na majambazi wa sasa?
Chasha,Unazungumzia mbuzi wa Maziwa/wa kisasa au, kuna mtalaamu mmoja aliwahi kunaimbia hawa mbuzi waga wanakufa katika mazingira ya kutatanisha je ni kweli?
Mwenye mradi wa mbuzi pia anapaswa kuwa na shamba ambalo atalitumia kwa ajili ya kufugia mbuzi wake. Mbuzi wakifugwa shambani wanakuwa kwenye usalama zaidi ukilinganisha na wale wanaofugwa mjini. Shambani pia kunakuwa na nyasi za kutosha ambazo huwafanya wale na washibe hivyo kuimarisha afya yao.
Nimependa maelezo yako Zantsan ila nilikuwa ninatamani kufahamu hao mbuzi wanaozaa pacha wanapatikana wapi na bei zao zipoje..