My 1month experience in JF

My 1month experience in JF

Nitashauri Mods kutoruhusu PMs kwenye jukwaa la mapenzi, chit chat ,Love connect ..Bali wahusika wote waende mtandao kama Badoo, fb nk.
Mnatuchafulia hali ya hewa kwa kubugudhi wageni humu [emoji23] [emoji23] [emoji23] mpaka wanajuta kwa mwezi mmoja tu...Tafadhali wazee wa PMs mnakuwa mbwa mwitu kwa ngozi ya kondoo kurarua swala wetu.
 
NDUGU YANGU HILI JAMVI LIMEVAMIWA 'IN THE SPIRIT OF FREE SPEECH' KIASI KWAMBA KWA SASA HALINA TOFAUTI NA FB. HIVI SASA NI NADRA SANA KUDADAVUA MAANDIKO MURUA YA NGULI AMBAO NDIYO WALIOTUFANYA SASA TUVUTIWA NA KUINGIA JAMVINI. HIVI SASA NI MAGUFULI! MAGUFULI !MAGUFULI !NA HAKUNA MANTIKI YOYOTE ILE YA WAANDISHI WENGI HUMU NDANI NA HII INANIFANYA NIAMINI KUWA KUTOKANA NA MISONGO YA MAISHA KUNA WENGINE BAADA YA KUTAFUTA SULUHISHO WAO WANATAFUTA WA KUMLAUMU NA HIVI SASA NI MAGUFULI! MAGUFULI!
Inawezekana aisee
 
Habari za Jumapili wanajamvi...
Nimetimiza mwezi mmoja na cku kadhaa toka nijiunge rasmi na JF. Kiukweli nimejifunza mengi, nimekutana na mengi humu ya kukatisha tamaa, kuumiza, kuvunja moyo hata kufikia kujitoa kwa muda [emoji4]

Ila kikubwa nilichojifunza ni kutokuamini kila kilichomo humu, kutokumuamini yeyote humu na zaidi sana usichukulie serious chochote kinachoendelea humu.

Ingia humu soma story ufurahi ama ujifunze jambo basi. PM ni za kupiga story za uongo na kujisifia maisha unayoishi, unachomiliki basi.

Tofauti na JF niliyokuwa ninaiona wakati nikiwa guest member, JF ya watu wenye akili na upeo wa hali juu, watu wenye mawazo na mitizamo ya hali ya juu, [emoji4] kumbe imejaa waongo, wanafiki na waliotayari kuumiza wengine kwa kivuli cha kutojulikana....

Mwisho ninawashukuru sana kwa kunikaribisha na kunifunza humu, naahidi nimejifunza na nitaendelea kujifunza kwamba JF ni dunia ya kusadikika [emoji4] [emoji4]

Have a good weekend and merry early xmass
Mkuu maisha ya jf hayana tofauti na maisha halisi ya jamii yetu, kwa hiyo unachopaswa kutambua in kwamba wewe uishi maisha yako, kwa sababu kila mtu ana umuhimu wake katika jamii husika, kama si muhimu kwako ni muhimu kwa mwingine, so don't ignore anybody. Pia katika real life mtaani unaweza kuchagua rafiki/ company kulingana na mahitajio au matakwa yako, pia humu you can be selective too, inawezekana hoja zangu ukaziona hazifai sawa, Ila Luna mwingine ataona zinafaa, that is how life goes.
 
Mkuu maisha ya jf hayana tofauti na maisha halisi ya jamii yetu, kwa hiyo unachopaswa kutambua in kwamba wewe uishi maisha yako, kwa sababu kila mtu ana umuhimu wake katika jamii husika, kama si muhimu kwako ni muhimu kwa mwingine, so don't ignore anybody. Pia katika real life mtaani unaweza kuchagua rafiki/ company kulingana na mahitajio au matakwa yako, pia humu you can be selective too, inawezekana hoja zangu ukaziona hazifai sawa, Ila Luna mwingine ataona zinafaa, that is how life goes.
Nashukuru sana kwa udadavuzi huu mkuu
 
JF ni dunia ya kusadikika [emoji1] [emoji1] [emoji1]. Pole, bila shaka ushalizwa tayari.
 
JF ni kila kitu. Kama alivyosema mleta uzi, uongo upo, umbea upo, matusi yapo nk lakini pia elimu nzuri tu ipo, misaada ipo, marafiki wapo, stress free corner ndo penyewe, ni wewe tu kuchambua na kupima yepi yanakufaa. Mimi nikichoka kwa shughuli zangu naingia JF kupata kiburudisho
 
Back
Top Bottom