Hello wana Jf
Mimi ni mgeni humu japo ni mwenyeji nimekuwa nikifatilia JamiiForums kwa muda ila leo nimejiunga rasmi haswa kwasababu ya post hii
Kiufupi mimi ni mwanamke wa miaka 27 mkristu mrefu mweusi(maji ya kunde)elimu yangu ni level ya degree,sina mtoto ni mcheshi kiasi etc
Age imefika sasa naamini ni wakati wa kupata mwenza wa kutulia nae naamini JF ni kama huko mtaani tu labda mume mtarajiwa atakuwa huku.
Si kwamba huko mtaani sijapata wanaume wanaotaka kuanzisha mahusiano sadly wengi bado hawapo tayari kwa ajili ya ndoa so tunapishana hapo,pia kutokana na kazi zangu pengine nakosa muda mzuri wa kusocialize kivile ukitoa clients ninaowahudumia kazini tu.
Mume mtarajiwa ningependa awe na umri kuanzia 33-35 au zaidi,kabila lolote,elimu ngazi yoyote muhimu ni jinsi gani unaaply elimu yako kwenye mambo muhimu ya maisha,ni mtafutaji sikatai kuajiriwa lakini naamini utakuwa na maono zaidi ya kujiajiri,awe mkristu(mahusiano yake na Mungu ni muhimu sana),mkarimu,msikivu na muelewa anaelewa majukumu yake kama mume,mrefu asiwe chini ya cm 170,akiwa Dar itakuwa vizuri zaidi
Relationship sio sehemu ya kupata stress bali ni sehemu ya kufurahia maisha,am matured enough kujua nini nataka na nini jamii inategemea kutoka kwangu same kwa mume mtarajiwa naamini itakuwa hivyo
DM yangu ipo wazi kwa uchambuzi na kujuana zaidi
Only serious men please kama kuoa bado bado hakuna haja ya kupotezeana muda
Asanteni[emoji1374]