My Brown Sugar

My Brown Sugar

Ilianza kama utani lakini sikujua kama itatokea siku nita fall in love na wewe,wala sikuwahi kuwaza kwamba utakuja kuziteka hisia zangu

Wakati mwingine huwa napotezea lkn ukweli unabaki pale pale kwamba hakika moyo wangu umekupenda,,naweza kuyadanganya mawazo yangu lkn si moyo wangu

Hatujawi kuonana lkn hisia zangu na moyo wangu unaniambia kuwa wewe ndio mtu pekee ambaye ni sahihi kwangu,,haijalishi kama nina mahusiano huku nje ya jf lkn linapokuja swala la kuwa ndani ya jf basi wewe ndio mtu pekee ambaye hupenda kuona comment zako na id yako

Sitojali kama una mahusiano nje ya jf,,kikubwa ukiwa ndani ya jf basi ningependa niwe ulimwengu wako,niwe furaha yako na niwe liwazo lako

Sitojali kama tutakuja kuonana au laa,,,kikubwa ni mimi kukupenda wewe tu,,,huwa nafurahi pale ninapo kuona online

Haijalishi ucheshi kiasi gani ninao kwa watu wengine wenye jinsia kama yako lkn deep down najua ni wewe pekee ambaye moyo wangu umekutunuku,,na kibaya zaidi siwezi kuudanganya moyo wangu juu ya upendo wangu kwako

Kwa wadau wengine wanaweza kushangaa inakuwaje nampenda mtu ambaye sijamuona,,jibu ni moja tu nahisi kuna chemistry kubwa juu yako na kuna bond kubwa kati yetu

Ninachoamini siku zote moyo unaona mbali sana kuliko macho yetu haya,,na moyo unahisi yale ambayo kwa mtazamo wa kawaida hatuwezi kuyaona

Haijalishi kama unahisi kama vile ninavyo hisi mimi,,kikubwa ni vile ninavyo hisi mimi juu yako,,najisikia raha kukupenda wewe na kukuwaza wewe

Kama kuna kipindi katika maandishi yangu nilitokea kukuuzi wewe kwa namna yoyote na kuumiza hisia zako naomba kukwambia am so sorry kipenz

Hope utaelewa kwa mapungufu yoyote ambayo yamejitokeza,,,haijalishi utachukua muda gani kuyatafakari maneno yangu,,kikubwa nitakuwa tayar kuwa na subira siku zote

Ninacho hitaji is to love you my brown sugar!

Ni hayo tu!
hivi mnakuwaje mnapata na wachumba humu noma sana mkuu, Hongera sana, Mimi zombi sijui
 
hivi mnakuwaje mnapata na wachumba humu noma sana mkuu, Hongera sana, Mimi zombi sijui
Inawezekana hata kwako pia mbona, kupitia comments na maongezi ya hapa na pale huku majukwaani,mnajikuta mnaenda sawa mwisho wa siku mnakuwa close
 
Back
Top Bottom