Huu ubaguzi na kulazimisha Imani kwa Zanzibar ulianza zamani sana, Imani ya mwengine unaingilia uhuru wa mwengine, watu wanafungishwa kwa lazima watake wasitake, iliwahi kutokezea kuna kipindi watu walikua wanafatwa hadi ndani wamejifungia wanakula wanakamatwa. Kipindi hichi cha Ramadhani kwa watu walinzi wa usalama wa raia ni dili kwao, maana wanavamia watu kisingizio wanakula wanawekwa ndani kutoka ni chapaa.
Kisa cha wamasai, ni ubaguzi dhahiri shahiri, wamekua Zanzibar kwa miongo mingi sana sasa na wamekua niwalinzi waaminifu kwa mahoteli visiwani, haijawi hata siku moja kutokea fujo, hawataki kuwaambia ukweli waliwafanya kitu gani hawa wamasai hadi wakawapiga watu fimbo, kwa ufupi walichokozwa, ila reaction ya waserekali ikawa ni kubwa kuliko mfano.
Unaweza kushangaa Zanzibar, walevi (wanywaji) wanaonekana hawafai zaidi ya mabaradhuli, wanatembea huru kabisa na hakuna hata mmoja anakemea, utasikia wakisema aaaaaa ndo sio rizki huyoooo, uliza yule afande yuko wapi? ( huru na hana hatia).
Imani thabiti ni kishinda vile vibavyoweza kuvunja Imani na sio kulazimisha wengine watii imani yako.