Analyse Babako nampenda sana.
Napenda sana anavotumia experiential learning kwenye maisha yenu/yako.
Sijasahau habari ya mashamba ya tangawizi.
Kuhusu my Hero mi ni baba yangu pia.
Babangu aliwahi kuniruhusu nikapigane na mvulana.
Alinipiga nikalia, nikarudi nyumbani ninalia.
Akaniuliza kwann unalia, nkasema nimepigwa na fulani!
Akaniambia kwann kila siku unapigwa na unarudi nyumbani unalia, simama!
Nikasimama, akaniambia this time around utapigana.
Nkasema naogopa, yule ni mvulana.
Akaniambia sawa, ila na wewe ni msichana.
Tofauti pekee iliyopo kati ya msichana na mvulana ni the fact kuwa mmoja anavaa kaptura na mwingine anavaa sketi.
Kuanzia leo utakaa kaptura.
Na utaenda kupigana.
Nikavalishwa kaptura, nkarudishwa eneo la tukio.
Akageuza kuniacha (tulikuwa tunakaa maghorofani) kumbe alilaa juu kama balcony hivi anatutizama.
Nkaenda nkaanzisha revenge, nkamchapa bana yule mvulana.
Aseeeeh.
Sijawahi sahau that energy ndani yangu.
Na sijawahi kusahau maneno ya babangu.
Na yamenivusha mahali kwingi mno.
My father my Hero.