My Favorite Stacks for Web, Mobile, Desktop &DAPP App development

Napenda kusoma vitabu kuliko kuangalia video ikiwa una kitabu kinachozungumzia DDD naomba share Hapa bro
 
Napenda kusoma vitabu kuliko kuangalia video ikiwa una kitabu kinachozungumzia DDD naomba share Hapa bro

Nitashare humu kitabu ila baadaye kidogo, sema DDD ni kitu cha kutafuta Google fasta.
Kuna hii link jamaa ameweka mfano wa DDD anayoitumia kwa Laravel na Symphony, anaihamisha kwenye frameworks bila kupoteza chochote How to create a framework-agnostic application in PHP
 
Walikupa nafasi ya kutetea teknolojia husika? Kwa sababu hakuna uwezekano wa kuandika framework Agnostic code. Unachoweza kufanya ni ku encapsulate functionalities kwenye units na kwa kanuni kama Polymorphism. Mfano

Code:
interface PaymentInterface{
    public function pay(int $amount, string $description): bool ;
}

Code:
class LaravelImpl extends PaymentInterface
{
    public function pay(int $amount, string $description): bool
    {
        //Laravel tied implementation
    }
}

$paymentGateway = new new LaravelImpl();
$paymentGateway->pay(100, 'Malipo ya kalamu');

Akija mtu anafikiri labda Symfony ndio new Technology na Laravel ni old then anabadilisha implementation anaweka yake

Code:
class SymfonyImpl extends PaymentInterface
{
    public function pay(int $amount, string $description): bool
    {
        //Symfony tied implementation
    }
}

$paymentGateway = new new SymfonyImpl();
$paymentGateway->pay(100, 'Malipo ya kalamu');


Siasa kama hizi hauwezi kuziweza maana madogo kama hao huwa wamewekwa humo kwa connections za wakubwa, chochote wanachokisema kinachukuliwa kuwa kweli na ndio basi, ukizingatia wakurugenzi kwenye hizi taasisi hawajui mambo ya teknolojia.
Ukikutana na mazingira kama haya huwa ni mabaya sana. Nakuelewa. Huwa nikikutana nayo huwa natafuta tu exit plan, hata kama ni mradi wa Billions. Maana najua mwisho wake ni kuharibu badala ya kujenga!
Nililazimika kupoteza mradi,
Badge of honor!
ila kama enzi hizo ningekua nimejilinda na concept ya DDD, mbona ningehamisha kwenda kwa Laravel na kuendelea kutafuna hela
DDD et al ni kuongeza complications unnecessarily. Kuandika code ukiwaza kuna siku zitahamia technolojia nyingine ni worst way of doing it. Andika code as if zitatumika milele kwenye hiyo platform but so clear kiasi kwamba porting kwenda kwenye another technology isiwe issue.
 

Samahani nimekua busy, sijapata nafasi ya kujibu vizuri, bila shaka utakua haujatulia uelewe hii dhana kabla ya kuiponda, ni kitu kimenichukua muda mrefu sana na kutafiti kwa kina na kufanya lots of practical expriments kabla kuipokea, manufaa yake sio limited kwenye framework independence pekee yake, ni shughuli muhimu sana kama ukiwa open minded uisome na kuielewa, hususan kama umewahi kujkuta kwenye complex multination enterprise project, aina ya systems ambazo zina-husisha multiple technologies.

Ningependa sana tuwe na nyuzi kama hizi ambazo tunajadili mbinu na mifumo tunayotumia kwenye kufanikisha shughuli, na tusiishie tu kwenye kujadili frameworks, ila tujadili full software development lifecycle, huwa unaanzaje kwenye feasibility mpaka mwisho, technlogies zote unazotumia kwenye DevOps yako ni zipi, na changamoto na manufaa yake.

Kuna vijana wengi watajifunza mengi humu.
 
On my journey to fullstack
 
Mwenye Google Play Console nanunua bei kuanzia laki 5 , iwe na angalau mwaka mmoja, na app hata moja ndani, ikiwa na keystore itakua poa zaidi, nicheki 0718474600 kama unayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…