Kama ukiweza, na jinsi nilishauri kwenye andiko langu hapo mwanzo, tengeeza system ambayo ni framework agnostic, maana kwamba business logics hazitegemei framework, tumia concept ya Domain Driven Dvelopment (DDD), na pia SOLID itakuchukua muda kuielewa ila ikikukaa, utashukuru sana.
DDD inakuewezesha uhamishe shughuli yako kutoka kwa Laravel kuja kwa Yii au framework yoyote bila mahangaiko, inakuwezesha kufanya upgrade ya framework yako bila kuvuruga business logics zako maana umezintenganisha na kuzilinda.
Pia inakuewezesha kubadilisha DBMS kama vile MYSQL kwenda hata MS SQL au Postgres bila shida, system yako inabaki wima licha ya misukosuko ya frameworks na vita vyao.
Kuna kipindi nilipoteza mradi wa hela ndefu kwenye taasisi moja ya kiserikali, yaani nimepiga mzigo ulioshikamana na kutegemea framework fulani, kisha taasisi ikaajiri vijana kutokea chuo ambao walikua wameiva Laravel, wakapiga siasa humo ndani kwamba system yangu iko based on old technology ambayo kwa maoni yao na ushauri kwa mabosi wa taasisi ni kuwa kwa vile sio Laravel, basi ni old technology.
Siasa kama hizi hauwezi kuziweza maana madogo kama hao huwa wamewekwa humo kwa connections za wakubwa, chochote wanachokisema kinachukuliwa kuwa kweli na ndio basi, ukizingatia wakurugenzi kwenye hizi taasisi hawajui mambo ya teknolojia.
Nililazimika kupoteza mradi, ila kama enzi hizo ningekua nimejilinda na concept ya DDD, mbona ningehamisha kwenda kwa Laravel na kuendelea kutafuna hela