MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Dah! Leo nimekumbuka mbali sana aisee.
Nakumbuka miaka kadhaa iliyopita nikiwa na yule msichana niliyempenda kuliko KITIMOTO ROSTI NA NDIZI MBILI (Pilipili usiweke), tulienda first date pale Dubai. Mida ya saa 5 asbh hivi tukakwea pipa Emirates hadi huko Dubai na kufika kama saa 12 jioni.
Tukafikia palepale Dubai mjini chumba namba 108, Khayirat Hotel. Nakumbuka tulifanya shopping na kuinjoi sana mitaa ya Deira.
Baada ya siku 3 tukaona twende kule jangwani (Desert safari), ikaja Land Cruiser V8 hadi hotelini kutuchukua, Ile ndo nafungua mlango wa V8 nipande nikasikia Ngo! Ngo! Ngo! Mtoto wa jirani Mama Peruu ananigongea na kuniambia "Anko maji yaliyokuwa yamekatika yameanza kutoka nipe ndoo nikakuchotee"
Ndoto yangu ikaishia hapohapo.