Tabutupu
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 13,206
- 18,549
- Thread starter
- #21
nashukuru Tabutupuila sidhani kama nnaamini asilimia mia hao washauri kwa kuwa kama binaadam nadhani nitawaeleza sehemu ya tatizo tu,nafikiri wa kujisaidia zaidi ni mimi mwenyewe,sielewi kwa nini kila nikisoma Signature yako nasikia msisimko fulani naomba usiibadilishe tafadhali,huwezi jua unalisha nini baadhi ya mioyo ya watu
Dada shosti, nashukuru sana kwa jinsi ulivyo jitahidi kujua na kutambua tatizo ulilo nalo na kulizungumza. Ni hatua kumbwa kuelekea uponyaji.
Kama sijasahau nafikiri ulichangia pia katika thread ya ugomvi wa wazazi watoto tujiweke wapi, na ulisema ugonvi ulikuwepo kati ya baba na mama ndio umesababisha makovu ndani ya moyo wako kiasi cha kumwogopa kila mwanaume unaye mwona.
Watu husema ukiumwa na nyoka , ukiona unyasi utakimbia pia. Lakini kila tatizo huwa njia ya kutokea.
1.Kuolewa ni haki yako ya msingi kwa hiyo matatizo ya baba na mama hayana kibali cha kukuzuia haki yako ya masingi.
2. Unahitaji emotiona/psychological healing kwani hofu uliyonayo hukuzaliwa nayo nddo maana nimekwambia uwaone wahusika /wataalam. Na uhakika utapona na utakuwa shosti yule wa mwanzo.
3. Si wewe tu mwenye tatizo kama hilo wapi wengi walio jeruhuwa na mambo mablimbali ya maisha lakini walipo chukua hatua wamepona na sasa wanayafurahia maisha yao kama kawaida.
4.Unatakiwa ufanye bidii ya kuwa karibu na wanaume, zungumza nao, chat nao, tembea nao hadi uone huna hofu tena mbele yao.
5. Zungumza kuhusu tatizo lako hata ukiwa na wasichana wenzio, na amini hofu uliyo nayo itapotea.
6. Tafuta websites zinazo toa njia ya kupona kutokana na tatizo kama lako, naamini utapata jibu.
Asante.