My happy ending story


Dada shosti, nashukuru sana kwa jinsi ulivyo jitahidi kujua na kutambua tatizo ulilo nalo na kulizungumza. Ni hatua kumbwa kuelekea uponyaji.

Kama sijasahau nafikiri ulichangia pia katika thread ya ugomvi wa wazazi watoto tujiweke wapi, na ulisema ugonvi ulikuwepo kati ya baba na mama ndio umesababisha makovu ndani ya moyo wako kiasi cha kumwogopa kila mwanaume unaye mwona.

Watu husema ukiumwa na nyoka , ukiona unyasi utakimbia pia. Lakini kila tatizo huwa njia ya kutokea.

1.Kuolewa ni haki yako ya msingi kwa hiyo matatizo ya baba na mama hayana kibali cha kukuzuia haki yako ya masingi.

2. Unahitaji emotiona/psychological healing kwani hofu uliyonayo hukuzaliwa nayo nddo maana nimekwambia uwaone wahusika /wataalam. Na uhakika utapona na utakuwa shosti yule wa mwanzo.

3. Si wewe tu mwenye tatizo kama hilo wapi wengi walio jeruhuwa na mambo mablimbali ya maisha lakini walipo chukua hatua wamepona na sasa wanayafurahia maisha yao kama kawaida.

4.Unatakiwa ufanye bidii ya kuwa karibu na wanaume, zungumza nao, chat nao, tembea nao hadi uone huna hofu tena mbele yao.

5. Zungumza kuhusu tatizo lako hata ukiwa na wasichana wenzio, na amini hofu uliyo nayo itapotea.

6. Tafuta websites zinazo toa njia ya kupona kutokana na tatizo kama lako, naamini utapata jibu.


Asante.
 
mi ending sina, siku mkitaka begining naweza kupost machache
 
Ni demu anitwa rozi nilimzimika ile kivile/
aliniweka chini sikufurukuta ka msukule/
alinifanya niamini niitarajie harusi
lakini alicho nitenda/ ni bora ninge ugua virusi.....
 
Tunaomba mwisho wa huo mwanzo wako!!!

haha, basi ngoja nikupe brief

kuna mtu wakati anaanza mazungumzo ya mapenzi na mimi alipata medical case akafanyiwa surgery ambayo iliyotishia reproductive health yake alilazwa hospitali muda mrefu na alikuwa amechanganyikiwa sana. mimi nlikuwa safarini, niliporudi tu moja kwa moja kutoka airport nilifika hospitali kumuona na mabegi yangu kwenye gari. kudhihirisha alivyonipenda mbele ya ndugu zangu na zake, alinitaka niombe chochote kutoka kwake naye atanipa. mi nilimuomba anifanyie mambo mawili tu, moja asahau tatizo lake na pili atoke hospitali na kurudi nyumbani.

kila mtu alinishangaa na wengine walinilaumu kwa masharti yale kwaani waliona kama namshawishi atotroke matibabu. yeye aliniambi hataweza na hajaruhusiwa na dk lakini atajitahidi kumuomba dk amruhusu kutoka hospitali. nilimuahidi kuwa kesho yake nitakuja kumchukua, kwa hiyo ajiandae na amfahamishe dr kuwa amepona kesho anarudi nyumbani. alijitahidi akaanza kwanza kumwambia nesi mmoja aliyekuwa anamhudumia na nesi alimueleza dk, dk alikataa na kesho yake alipopita kukagua wagonjwa, alimkumbushia. mimi nilifika kama saa 5 asubuhi nikaambiwa amechukuliwa na dk kwa uchunguzi zaidi, baada ya kama dk 45 hivi, alirudi na kutuambia ameruhusiwa kutoka hospitali!

ndugu zake walicharuka, wengine wakasema nataka kumuua ndugu yao, walimfuata dk kumuonya kuhusu kumruhusu ndugu yao kirahisirahisi vile hasa baada ya ushawishi wangu, dk alishangaa kusikia kuna mtu ameshawishi ile ruhusa kwani alikuwa hata hajawahi kuniona. baadaye nilimfuata chemba nikamueleza kuwa mimi ndiye ninayelaumiwa. akaniambia kuwa amempima kwa kina na ameridhka na amemruhusu na kuwa matibabu mengine atakuwa anafuatilia akitokea nyumbani. kweli tuliondoka na ndio ulikuwa mwanzo wa yule ndugu kupona hadi leo.

kwa kweli familia yao inanipenda sana hadi leo na baba yake alinipa zawadi kubwa sana amabayo napenda niiache siri kwa leo
 
mimi yangu itajaza kurasa ila ndio sababu ya kutokuwa na mwenza mpaka leo,nikimwangalia mwanaume machoni namwona yuleyule aliyenitenda

Tafadhali twanmbie hata kama ni kurasa mia, jitahidi.
 
Ni demu anitwa rozi nilimzimika ile kivile/
aliniweka chini sikufurukuta ka msukule/
alinifanya niamini niitarajie harusi
lakini alicho nitenda/ ni bora ninge ugua virusi.....

Ebu twambie uhalisi, unaweza ponya maisha ya mtu.
 
haha, basi ngoja nikupe brief



kwa kweli familia yao inanipenda sana hadi leo na baba yake alinipa zawadi kubwa sana amabayo napenda niiache siri kwa leo

Hi kali, nimeipenda. N a kila la kkeri judi.
 
4.Unatakiwa ufanye bidii ya kuwa karibu na wanaume, zungumza nao, chat nao, tembea nao hadi uone huna hofu tena mbele yao.
SASA HAPA NDIO TATIZO KILA NIKIWA NAE NIKIMWANGALIA MACHONI NAONA KAMA MACHO YAKE KUNA KITU YANANIAMBIA,NAANZA KUMCHUKIA NDANI KWA NDANI MPAKA MWISHO CHUKI INATOKEZA HADHARANI
 


pole, japo nafikiri hujamwelewa. Maana ya kuchukua hatua ni kufanya kitu cha ziada. Maana yake hata kama hiyo hali inakujia inatakiwa ujifunze kuishinda. Kama sivyo ina maana unaifurahia na kamwe hutapata tiba.
 
Lakini darling si tulikubaliana hutawaeleza watu hii stori. aargh umeniudhi sana..........ila nimekusamehe kwa sababu bado nakupenda.
 
Lakini darling si tulikubaliana hutawaeleza watu hii stori. aargh umeniudhi sana..........ila nimekusamehe kwa sababu bado nakupenda.

haha thanks dear. lakini si nashare na wapendwa wetu ili mwenye kupata cha kujifunza nae ajifunze?
 
Ni demu anitwa rozi nilimzimika ile kivile/
aliniweka chini sikufurukuta ka msukule/
alinifanya niamini niitarajie harusi
lakini alicho nitenda/ ni bora ninge ugua virusi.....

Haaa ndugu yangu usiseme hivyo, yani binadam mwenzio akuumize kiasi cha kuomba magonjwa mabaya hivyo no. Bora alivyo kutenda na umezoea kumbuka ungeugua ungeweza kufa au ungekua unaishi kwa matumaini kitu ambacho usingekisahau maisha yako yote na hata familia yako. Kama kitu ni chako haiwezi badilika nakama si chako muda utafika kitaondoka. Life has to go on with or without.
 
Nikikumbuka sad ending yangu, machozi hunitoka na niliapa kutopenda tena mpaka pale mama yangu mzazi aliponiuliza usipowapenda wanawake nani atakuwa mama wa watoto wako au na watoto nao umewachukia?

Mwanangu kwa kutengeneza story nimekuvulia kofia....
 

Shosti,


Watu hutenda makosa kwa sababu wao si mungu, si malaika!


Every one has a moment of madness. Kama baada ya kosa anaomba msamaha ,umsamehe tu, ndio, dunia ,ndio maisha.

Usiwe perfectionist!


Kama aliyekuumiza huwa anarudia kosa hilo hilo, basi umwepuke.


Kusamehe ni moja kati ya sifa ngumu kuwanayo kwa wengi, ukiwa nayo means you belong to a special group.


Watu ni visasi, visasi tu.
 
Mimi yakwangu hata wiki haina,hapa nafikiria kuwashirikisha wana JF hivi karibuni,bado napata matatizo ya namna ya kuiweka humu ila nikiwa tayari nitafanya hivyo.
 
Mimi nina ya mshkaji wangu, alikuwa anampenda kweli binti na akawa amepanga kumfanyia surprise ya kumvisha pete ya uchumba. Yaani jamaa alikuwa ameshadhamiria kumwoa binti. Siku ya siku ikafika jamaa kajiandaa na surprise yake tupo tunamngojea binti aje, basi ile kufika yupo na rafiki yake kumbe binti naye ndo alikuwa amepanga kumwaga jamaa siku hiyo....

Jamaa akaitwa pembeni, binti akamwambia Bwana samahani ila inabidi nikueleze; kuna Bwana nimempata na naona kuwa tunaendana naye zaidi na ameomba kunioa na mimi nimemkubalia, ila naomba tuendelee kuwa marafiki na tuwe tunasaidiana kama kaka na dada. Jamaa karibia azimie, kama jitihada za makusudi hazikufanyika....

Baada ya hapo Binti akaolewa na Bwana chaguo lake na rafiki yangu Mungu si Athumani akapata mke (tena yule rafiki yake binti aliyekuja naye siku ile) jamaa amebahatika kupata mapacha wawili na Binti naye Mungu kamjalia kabinti na muda si mrefu anategemea kupata kitoto kingine cha kiume. Mpaka leo wanaendelea na maisha vizuri kabisa na ni family friends na binti amemtambulisha jamaa kwa mumewe kama kaka yake na wanaheshimiana na kushirikiana utafikiri watoto mapacha vile. Kinachonifurahisha zaidi, jamaa ndiye mshauri mkuu kwenye ndoa yao, na Binti halikadhalika amebeba jukumu la kuishauri familia ya jamaa yangu kwa maana anawajua wote vizuri.
 
kama ni kweli hongera zao waangalie wasije chakachua maji na mafuta huo ukaribu upo salama kabisa au funika kombe mwanaharamu apite

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…