Jamani Jamani Asha D
Mbona leo mnanishambulia shosti wako??
Najua unampenda sana partner wako, lakin kama unampenda kweli utamlinda.
Hivi umemuangalia Lizzy na mambo anayofanya tena kwa vitendo kabisa???
Unajua unapaswa umuangalie kwa JICHO LA 3???
Yeye anatoka na Kloro au Uporoto LIVE tena mbele yangu wanaenda zao nisipokujua, lakin mi nimetulia tuliii
Na cha kushangaza hata wewe unaejiita PARTNER wake hata kukohoa ulishindwa, achilia mbali kumsema kama unavyonifanyia mimi hapa
Au unataka kusema u-parter wenu ni pamoja na kufichiana makosa yenu??
Unajua undani ya thread aliyoanzisha partner wako iitwayo UPOLE???
Natungiwa mpaka thread kwamba nimezidi UPOLE na ameshajisema wazi yeye HAPENDI WAPOLE
Anajua Sipiyuu ni mpole sana, hata nimkute na Uporoto Bar wanapigana mabusu wala simsemi lolote.
Au una ajenda ya siri na patner wako??? Najua una kaka bachelor na sasa naona kila dalili za wewe kunishambulia mbele ya halaiki ili nionekane sifai wala sijui kupenda, na iwe njia rahisi Lizzy aje kwa kaka ako sio???
Usihangaike sana jamani Asha D
Lizzy kwenye thread yake ya UPOLE ameshanisema vya kutosha
Na kama vile haitoshi hapo juu amerudia tena "SIPIYUU ASIYE WANGU TENA"
NA shoga mtu ukaamua kunimaliza kabisa kwa kuniambia ninamfanyia ushe*** partner wako
Mi nipo tayari kumuachia aje kwa kaka ako bila kinyongo.
Nitamuachia ili wawe huru zaidi na kaka ako waponde raha za dunia bila kificho, kwani mwanzoni walijificha kuniogopa
Mie mpole, niliyeumbwa mpole, naongea kiupole sina la kufanya tena. Nitapaki na upole wangu kwani siwezi kuubadlilisha (amenipa Mungu)
Naomba nikuruhusu rasmi kwamba, mwambie kaka ako kwamba sasa hana kizuizi tena kujirusha na Lizzy anaetamka wazi CPU SIO WAKE TENA.
Eeeh Mungu wasamehe wadada hawa, kwani hawajui walitendalo.
Nihurumie mja wako ninaeonewa na wanadamu nipate aliye sawa na ulivyoniumba.