My wife to be ananuka mdomo,naogopa kumwambia!!

Hata mimi sijaona ubaya wa hii thread. Mimi nadhani hapa unaweza andika chochote na bado usimdhalilishe mtu yeyote kwa kuwa hujataja jina. Angekuwa anaongea na washkaji kijiweni hapo sawa tungesema amemdhalilisha msichana wake.

Naona tunaanza kutishana yani tuanze ku calculate kabla ya kuandika kwani imekuwa face book. Hunijuhi, sikujuhi ndio maana this is a place where we can dare to talk openely.

Wanaonuka midomo ni wengi hivyo hii thread inaweza wasaidia wengi tu. Tupunguze kuwa monitors; mtu ukiona thread haina maana ipotezee.

Kwani hili jukwaa ni la wakongwe tu ama kila mtu anaweza changia no mata ni new member au mkongwe aceni watu watu watoe ideas zao bwana.

Wala hamna mtu aliyegomba kuwa wageni wasichangie. Ni kwamba tu inashtusha kidogo kuona mwanachama mpya kama wewe uliyejiunga tarehe 21, mwezi wa 8, 2011 kuanza kucomment kuhusu mambo ya zamani na wanachama wa zamani. Mgeni gani anayejua mambo ya zamani ya hapa?

Asanteni kwa michango and mawazo yenu wadau! I know ntayafanyia kazi

Hujuhi kuwa kuna watu ni wakongwe but still ni new members. Mimi mfano nimeijua JF since 2006 or 7 but have joined as a member recently. Kwa hiyo kujua ya zamani sio issue ni ufuatiliaji tu. Usiangalie joining date na ku conclude kuwa huyu member hajuhi ya zamani.

Ndicho hicho tunachosema kwamba wengine wanaonekana wageni kumbe hata si wageni. Ni majina yao tu ndo yaliyomageni. Multiple IDs....

Hako ni ka ugonjwa kadogo sana. Just mchukue mwambiye akusindikize kwa Dr wa kinywa. Halafu wewe sasa tibiwa halafu mshauri naye acheki mdomo wake atapewa dawa na kupewa ushari mzuri tu tena utakula denda kila siku

Kurudi kwenye mada; Najua kuna watu wana harufu mbaya mdomoni na most of them I think wanajua kuwa wana hilo tatizo. Mfano kulikuwa na binti tulikuwa tunasoma nae college alikuwa na hilo tatizo tena lake nadhani lilikuwa ni extreme kwani kila mtu alikuwa anajua.

Huyu dada ni msafi na alikuwa anatumia mouth wash (si unajua mabafu ya kushare tulikuwa tunamuona anavyo jitahidi). Na wazazi wake ni wale ambao uwezo wao ni naweza kusema ni mkubwa hence kama ni mambo ya hospitali wangeweza ku afford hospital yeyote.

She made me conclude kuwa hilo tatizo labda halina dawa ni maumbile. Vile vile huyo mdada alikuwa na harufu kali ya jasho (kikwapa). Alikuwa anatumia most expensive perfumes.

Lakini ndio zilikuwa zinafanya harufu iwe mbaya zaidi. Ila kama wadau wanavyosema hapo juu jaribu kwenda kwa dentist yawezekana wengine hawaendi hospital na wanaishia kukata tamaa. Mimi nilikuwa ignorant nilijua kunuka mdomo na kikwapa ni ugonjwa wa kudumu yaani ni maumbile.

..............Hata wewe pia unanuka mdomo lakini anashindwa kukuambia.............

1. Nunua line ya simu.

2. Weka kwenye simu yako.

3. Mtumie ujumbe mfupi wa maneno.

4. Itupe hiyo line.

duuu hii lazima atamshitukia jamaa ndiyo ametuma hiyo sms.

Dah hapo mnaambukizana magonjwa ,mwambie aache kula chips maharage na maziwa mgando,mwanamke usafi bana
Katika vitu vinavyoondoa harufu mdomoni ni MAZIWA MDANDO,hapo umeteleza au haufahamu.
Vitu vya kuangalia kwenye tatizo la kunuka mdomo:
1.je usafi unafanyika kwa usahihi mara 2-3 kwa siku ?
2.ulimi husafishwa ? yaani pamoja na kusugua pia tumia upande wa kushikia ku-scrap.
3.kuna meno yaliooza ?
4.una ugonjwa wa fizi/kinywa ?

kama yote hapa juu yako sawa sukutua na maji ya ufukuto yaliyochanganywa na chumvi/mdalasini(cinammon),na kunywa mtindi mara kadhaa kwa siku.

kama umechagua waridi upende na miiba yake. Otherwise unapaswa kuchagua kilicho bora. Ukishindwa kumwambia atibiwe basi na ww u mgonjwa kama yeye au zaidi. A man should bold enough to face challenges. Ki ukweli nikiambiwa nioe umpya leo haki ya nani nitakagua hadi kucha ,sembuse mdomo?

Mchane live mwana,mpe kubwa usirembe,manake ukikaa kimya haisaidii,pengine yeye hajijui,we ndo mtu wake wa karibu wa kumweleza hilo.

Hapa kuna mtu kaniambia dawa ya kienyeji ya kuua harufu either ya mdomo au kikwapa ni kutumia maji yaliyolowekewa sufuria ya ugali, haya kazi kwako

Hapa kuna mtu kaniambia dawa ya kienyeji ya kuua harufu either ya mdomo au kikwapa ni kutumia maji yaliyolowekewa sufuria ya ugali, haya kazi kwako
hii ni dawa ya kienyeji kwa ajili ya kikwapa.

Huyu jamaa ni mpumbavu!mzaririshaji!mshamba!ungekuwa kweli unampenda na ndo mtarajiwa wako usingesema hayo yote!bali ungesema jamani nini dawa ya tatizofulani?usimpotezee dada wawatu mdawake fataki we!

jaza mint chewing gum home kwako uwe unampa mara kwa mara yan kama unafanya utani vile unampa na wewe unakula, hiyo ya ugali niliisikia anasukutua mdomoni

Jitahidi umuambie, maana kama ni kweli ni aibu mbele ya watu wengine wataposema mtarajiwa wako.

Wote mnaoponda hii thread sio waelewa.

Sijaona udhalilishaji hapa zaidi ya jamaa kutaka ushauri.

Tena ameeleza vizur tu kuwa mwez wake akiambiwa anaona amedharauliwa je atumie njia gani kumwambia bila kuleta ugomvi baina yao?

Akaomba kama kuna dawa mmwambie na jinsi gani atatue hili tatizo, sasa udhalilishaji uko wapi hapa?

Yani kusema tatizo lilipo ni udhalilishaji? Achen hizo bana mbona kuna thread zinaenda mbali zaidi ya hapa?!

Mkuu nakushauri kama ifuatavyo.
Mchukue dem wako mkae umwambie kwa jinsi gani unampenda na hutak kumpoteza.
Then mwambie kwamba mapenz ya kweli ya yale ya kuambiana ukweli kwa lengo la kuboresha mahusiano yenu.
Hivyo umeamua kumwambia tatizo alilonalo ili mjue jinsi gani mnalitatua.
Akikuuliza ni tatizo gani basi hapo unamwambia kwa upole kabisa. Then onyeesha jitihada za kutaka kumsaidia ktk tatizo hilo mf. Mshauri muende dental clinic n.k
hapo demu atakuelewa kwamba hujamdharau ila ni hali halisi.

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…