Songambele
JF-Expert Member
- Nov 20, 2007
- 4,726
- 2,607
Dhamira ya Serikali JMT ya kuboresha mazingira ya kufanya Biashara Tanzania bado ni ndoto ya alinacha. Ukiwasikia viongozi wa kitaifa wanahubiri unaweza ukaona nchi ya ahadi iko karibu kuifikia lakini watendaji katika taasisi za Umma bado wamelala fofofo na wanaamini watanzania bado ni wale wa miaka ya 90.
Waziri wa Ujenzi juzi kati alisafisha watendaji wa mizani ikiwemo na Mzani wa Vigwaza, Lakini wamerudi tena upya kwa matendo yao ya kubambikia watu uzito na kutoza faini za kukomoana kwa madereva wa magari ya Mizigo. Mh. Abdallah Ulega tunakustua tena unahujumiwa na vijana wako wa Vigwaza Mizani. wanatengeneza foleni za makusudi, wanazidisha uzito na wanatoza faini za kukomoana. Tunajua nyie mmeshika mpini lakini mkumbuke yaliyotokea Oktoba 29 wananchi walikimbilia miundombinu sababu ya Tabia za watendaji wenu kulazimisha Rushwa.
Watendaji wenu kwanza wanatugombanisha na wateja wetu kwa kushindwa kuwafikia kwa wakati, Pili wanatuongezea gharama za uendeshaji kwa kutumia mafuta mengi bila sababu za msingi na wanatutoza faini za kutukomoa wakisingizia sheria mlizotunga ndio zinasema hivyo. Nchi zingine za SADC unaruhusiwa kupima zaidi kama hukuridhika na ikiwezekana kupanga mzigo.
Wanakataa gari isipime mara mbili kama dereva hakulizika na kupima kwao, Wakala wa Mizani nae ni ndugu wa Damu na amelala fofofo mpaka asikie wanasiasa wanasema. Sie tunawapa taarifa hii kuelezea machungu mnayotupatia kama hamtaki kusikia msijetulaumu tukijichukulia sheria mkononi. Hii nchi ni ya kwetu sote sio ya watumishi wa serikali na viongozi wao tu tunayohaki ya kufurahia matunda ya Uhuru sote.