Mzao wa Tippu Tip uko wapi?

Ndio na hii ni km wiki ya tatu na hata sasa nimefanya hivyo
 
Kwanza huyo mtu kwenye picha anaitwa Hamad bin Muḥammad bin Jum'ah bin Rajab bin Muḥammad bin Sa‘īd al-Murjabī;,ni Mswahili- mzanzibari na si chotara ! Amezaliwa na Baba ambae ni Mswahli wa Zanzibar na Mama ambae amechanganya Muscut na Bara. Mamurjebi wamatapakaa duniani, wapo Zanzibar,Kenya, London, Denmark nk. Wajuu zake walitengeneza hata tamthilia na kurushwa na BBC Swahili

Alikuwa maisha yake amepoteza kwa kusafiri kwa miguu kutoka pwano mpaka afrika ya kati. Hivyo si kweli kama alikuwa na wake wengi. Safari moja kutoka Zanzibar na kurudi inamchukua hata miaka miwili!

Biashara yake kubwa ilikuwa meno ya tembo kuliko watumwa amabayo ilikuwa inalipa zaidi na haina hasara.
Biashara ya utumwa ni ngumu kwa vile kupata soko zuri , mtumwa lazima awe na afya njema.

Kuna wakati watumwa hulazimika kukaa kambini kungoja watononoke ili bei iwe juu

Baba yake Hamad alikuwa Gavana wa Tabora na alioa pia katika ukoo wa Chifu Fundikira
 

Asante kwa historia nzuri
 
Nashukuru Muungwana umenipa kumbukumbu nzuri sana ya Tabora nilisoma pale miaka ya sitini Elimu ya Primary ikiitwa H.R. karibu na chuo cha Uhazili Mkuu wa shule akiwa Marehemu Mzee Abubakar Mwilima na Mkuu wa Mkoa akiwa Mzee Waziri Juma, Mkuu wa Polisi akiwa Marehemu Hans Pope, wakati huo tukiwa mwanafunzi tuna badilishana magazeti ya Spear,Boom na Fearless Fang na jirani yangu Jaji Mutungi,zilikuwa pia ni enzi za ushindani mkali wa bendi za Tabora Jazz na Kiko Kids na timu bora ya mpira kupata kutokea Tabora ikipaishwa na ndugu wawili Edmund na Sixmund,Nina imani nitafika siku moja.
 
Hivi vizazi vya hawa Waarabu Maarufu wa zamani kama huyu Tippu Tipu ambaye pia aliitwa Mtipura vingalipo na kama yeye pia alikuwepo Ibn Batuta aliye kuwa na masikani yake Pangani Tanga ni bahati mbaya kuwa Wasomi na watafiti wetu wa mambo ya historia hawakujipa nafasi katika kuchimba kutafuta juu ya koo hizi na pia katika Vizazi hivi hawa kupatikana wasomi walio pekua kumbukumbu za Mababu zao hawa na kuweka wazi,huku masomo yetu ya historia yakitulisha ufahamu juu ya kina Karl Peter, Zelewsky,n.k.
 
Asante kwa kumbukumbu nzuri mkuu...Bila shaka shule hiyo ndio kwa sasa ikiitwa ISIKE PRIMARY School,imejengwa kwa mawe jirani na Uhazili na Central Police na upande wa Magharibi ikiwa ni Jimbo Katoliki la Tabora
 
Asante kwa kumbukumbu nzuri mkuu...Bila shaka shule hiyo ndio kwa sasa ikiitwa ISIKE PRIMARY School,imejengwa kwa mawe jirani na Uhazili na Central Police na upande wa Magharibi ikiwa ni Jimbo Katoliki la Tabora
Wala sita shangaa kwa mabadiliko hayo makubwa maana toka 1969 sijafika tena Tabora nashukuru kwa kuniweka sawa.
 
This is obsurd,waafrika walitiwa urumwani na wazungu, waarabu walokuwa watu wa kati tuu
 
Ohhh Who is inslaving Africans now? And who did it before?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…