Mzao wa Tippu Tip uko wapi?

Mzao wa Tippu Tip uko wapi?

Ndio na hii ni km wiki ya tatu na hata sasa nimefanya hivyo
 
Ikumbukwe kwamba wakati wa Biashara ya Utumwa ni Waafrika wenzetu ndiyo waliokuwa wanakamata ndugu zetu kama Watumwa na kuwauzia Waarabu na Wazungu mmoja wao ni mtu maarufu Mchotara Tippu Tip ambaye alikuwa ni Mchotara wa Kiarabu na Kikwetu!
Mama yake Tippu Tip alikuwa ni Mbantu mweusi kama mimi na ni Mzaliwa wa Dar yetu kipindi hicho haikuitwa Dar wakati Baba yake ni alikuwa ni Mwarabu wa kuapia kutoka Oman, huyu ndiyo alikuwa kinara wa kutuuuza Waafrika, sasa swali langu ni Je, mzao wake Tipp Tip uko wapi?
Kwa maana Tipp Tip alioa wake wengi na watoto wengi sana tu hivyo ina maana kizazi chake kipo na kwa kuwa alikuwa ni tajiri, utajiri alioupata kwa njia haramu ya kuuza Watumwa basi aliurithisha kwa vizazi vyake vilivyofuatia, sasa viko wapi vizazi vyake?


Muuza watumwa Maarufu Afrika Mchotara Tippu tip!

images



Kazi ya Tippu Tip!

Islams+african+slaves.jpg




Kwanza huyo mtu kwenye picha anaitwa Hamad bin Muḥammad bin Jum'ah bin Rajab bin Muḥammad bin Sa‘īd al-Murjabī;,ni Mswahili- mzanzibari na si chotara ! Amezaliwa na Baba ambae ni Mswahli wa Zanzibar na Mama ambae amechanganya Muscut na Bara. Mamurjebi wamatapakaa duniani, wapo Zanzibar,Kenya, London, Denmark nk. Wajuu zake walitengeneza hata tamthilia na kurushwa na BBC Swahili

Alikuwa maisha yake amepoteza kwa kusafiri kwa miguu kutoka pwano mpaka afrika ya kati. Hivyo si kweli kama alikuwa na wake wengi. Safari moja kutoka Zanzibar na kurudi inamchukua hata miaka miwili!

Biashara yake kubwa ilikuwa meno ya tembo kuliko watumwa amabayo ilikuwa inalipa zaidi na haina hasara.
Biashara ya utumwa ni ngumu kwa vile kupata soko zuri , mtumwa lazima awe na afya njema.

Kuna wakati watumwa hulazimika kukaa kambini kungoja watononoke ili bei iwe juu

Baba yake Hamad alikuwa Gavana wa Tabora na alioa pia katika ukoo wa Chifu Fundikira
 
Mkuu Barbarosa sehemu ya ukoo wa huyu jamaa wapo sehemu moja Tabora inaitwa "Kwihala".Ni nje kidogo ya mji wa Tabora,njia ya kwenda Sikonge karibu na Seminary Kuu ya Kipalapala ya Kanisa Katoliki iliyojengwa toka miaka ya 1880's.

Huku Kwihala ndio ulikuwa mji wa zamani wa Tabora,kabla ya watu kusogea kuifuata reli ya Kati ya kwenda Kigoma,Mwanza na Mpanda.Lkn mji haswaa ndio huku Kwihara ambapo unamkuta Mzee Nassoro Mwarabu ambaye ni ukoo wa Tippu Tipu.

Na ukifika pale Tabora,hawa Waarabu Ukoo wa Tippu Tipu wanafahamika kama "Waarabu wa Kwihala".Pembeni ya hiki kijiji chao,kuna Makumbusho ya Kale,ambapo unakuta historia ya kina Livingstone,Henry Stanley,Wamisionary wa Holy Ghost Fathers ambao kwa mara ya kwanza wanafika Unyanyembe walipokelewa na hawa Waarabu wa Kwihala.

Eneo hili kuna miembe mingi sana,kuna maembe aina ya boribo na embe dodo.Miembe hii ni miembe "pori" maana haina mmiliki zaidi ya mtu yoyote kuchuma na kula.Miembe hii ilipandwa miaka ya 1880's ikiwa na lengo ya kutumika kama kiashiria cha njia ya kutoka Unyanyembe mpaka Ujiji-Kigoma kutokea Kalambo.

Wapagazi na Waarabu kila walipopita,ili wasisahau njia wakati wa kurudi walipanda miembe,ili wakati wa kurudi waitumie kama "Routes" za kufika.Na kumbuka safari wakati huo ilikuwa inachukua miezi hadi miaka.Ndio maana hata mkoloni toka Tabora mpaka Ujiji,alijenga reli akifuata miembe iliyopandwa na Mwarabu wa Kwihala ambapo ilikuwa sehemu ya makazi ya mke wa Tippu Tipu.

Asante kwa historia nzuri
 
Asante kada Wakudadavuwa ndio maana niliandika "pori" nikiwa na maana si pori haswaa,bali ilipandwa miaka mingi kiasi imekuwa kama msitu na hakuna mwenye nayo.

Eneo lote hilo likiitwa "Kazeh" likianzia eneo ilipo Hospital kongwe ya Karunde,unapita BOMANI ambapo sasa ndio makao makuu ya Jeshi Bregedia ya Kanda ya Magharibi,unashuka lilipo gereza la Tabora Mjini,Halafu shule za Sekondari za Tabora Schools zilizojengwa na Mjerumani...Moja ikiitwa Berlin(Tabora Boys) na nyingine ikiitwa Warsaw (Tabora Girls) kuna shule ya Msingi Kazeh Hill na baadae ukishuka kidogo unakutana na Seminary ya Kipalapala na Mashariki ya Seminary ni uwanja wa ndege wa Tabora ambao wakati wa vita ya kwanza na ya pili ulitumika sana kwa ndege kutua.

Kumbuka Tabora ndio ilikuwa "Administrative Centre" ya Mjerumani,baada ya yeye kufika na kukuta Arabs Traders wameikamata Unyanyembe na kufanya biashara nzuri kati ya pwani na Bara ya Tanganyika mpaka Congo na Zambia.Hapa ndipo Mjeruman akaamua kujenga reli na kufanya kitovu kikuu cha usafiri.Ndio maana karakana kuu ya reli ilikuwa Tabora(Wakati huo reli ndio njia kuu ya usafiri).Mtu hawezi kwenda Mwanza,Kigoma,Mpanda bila kupita Unyanyembe.

Tippu Tipu na vizazi vyake wakaishi hapo Kwihala....wakiwa ndio "conteoller" wa biashara zooote za kutoka pwani kwenda bara,na kinyume chake.Pitia hapa kidogo

Historical information.
Kwihala is a historical site; a center where Slaves were assembled from the Congo, Burundi, Rwanda, and Western Tanganyika (now Tanzania). It was a stop-over as arrangements were made to take the slaves to Bagamoyo and Zanzibar on the way to Europe and other parts of the world.
It is in this area where Stanley met Dr David Livingstone as he was trying to find out the origin of the Nile. Dr David Livingstone was on the way to Ujiji along the shore of Lake Tanganyika in the 1800s.
Dr Livingstone lived in a hut previously inhabited by an Arab slave trader, which was constructed at Kwihala in the 1800s. Since Tabora (originally called Kazeh) is not a tourist destination few know about this historical location."


Mzee Mohamed Said atatusaidia,maana licha ya kuwa ni mzaliwa wa K'koo,lkn huyu ni "mtoto" wa Ujiji...
Nashukuru Muungwana umenipa kumbukumbu nzuri sana ya Tabora nilisoma pale miaka ya sitini Elimu ya Primary ikiitwa H.R. karibu na chuo cha Uhazili Mkuu wa shule akiwa Marehemu Mzee Abubakar Mwilima na Mkuu wa Mkoa akiwa Mzee Waziri Juma, Mkuu wa Polisi akiwa Marehemu Hans Pope, wakati huo tukiwa mwanafunzi tuna badilishana magazeti ya Spear,Boom na Fearless Fang na jirani yangu Jaji Mutungi,zilikuwa pia ni enzi za ushindani mkali wa bendi za Tabora Jazz na Kiko Kids na timu bora ya mpira kupata kutokea Tabora ikipaishwa na ndugu wawili Edmund na Sixmund,Nina imani nitafika siku moja.
 
Hivi vizazi vya hawa Waarabu Maarufu wa zamani kama huyu Tippu Tipu ambaye pia aliitwa Mtipura vingalipo na kama yeye pia alikuwepo Ibn Batuta aliye kuwa na masikani yake Pangani Tanga ni bahati mbaya kuwa Wasomi na watafiti wetu wa mambo ya historia hawakujipa nafasi katika kuchimba kutafuta juu ya koo hizi na pia katika Vizazi hivi hawa kupatikana wasomi walio pekua kumbukumbu za Mababu zao hawa na kuweka wazi,huku masomo yetu ya historia yakitulisha ufahamu juu ya kina Karl Peter, Zelewsky,n.k.
 
Nashukuru Muungwana umenipa kumbukumbu nzuri sana ya Tabora nilisoma pale miaka ya sitini Elimu ya Primary ikiitwa H.R. karibu na chuo cha Uhazili Mkuu wa shule akiwa Marehemu Mzee Abubakar Mwilima na Mkuu wa Mkoa akiwa Mzee Waziri Juma, Mkuu wa Polisi akiwa Marehemu Hans Pope, wakati huo tukiwa mwanafunzi tuna badilishana magazeti ya Spear,Boom na Fearless Fang na jirani yangu Jaji Mutungi,zilikuwa pia ni enzi za ushindani mkali wa bendi za Tabora Jazz na Kiko Kids na timu bora ya mpira kupata kutokea Tabora ikipaishwa na ndugu wawili Edmund na Sixmund,Nina imani nitafika siku moja.
Asante kwa kumbukumbu nzuri mkuu...Bila shaka shule hiyo ndio kwa sasa ikiitwa ISIKE PRIMARY School,imejengwa kwa mawe jirani na Uhazili na Central Police na upande wa Magharibi ikiwa ni Jimbo Katoliki la Tabora
 
Asante kwa kumbukumbu nzuri mkuu...Bila shaka shule hiyo ndio kwa sasa ikiitwa ISIKE PRIMARY School,imejengwa kwa mawe jirani na Uhazili na Central Police na upande wa Magharibi ikiwa ni Jimbo Katoliki la Tabora
Wala sita shangaa kwa mabadiliko hayo makubwa maana toka 1969 sijafika tena Tabora nashukuru kwa kuniweka sawa.
 
This is obsurd,waafrika walitiwa urumwani na wazungu, waarabu walokuwa watu wa kati tuu
 
Ohhh Who is inslaving Africans now? And who did it before?
 
Back
Top Bottom