Makonde plateu
JF-Expert Member
- Nov 19, 2022
- 1,443
- 3,480
Copy and Paste kama ilivyokutwa;
"Moyo wangu unavuja damu kuhusu binti yangu wa kwanza Maria Izidory Petro ambaye alikuwa anasoma Chuo, Institute of Tax Administration kilichoko Dar es Salaam akichukua Shahada ya Kodi. Alipata changamoto ya kiafya ghafla kwa ambacho kilidaiwa kuwa sumu kwa mujibu wa madaktari tarehe 26 na kufariki 27 Septemba 2024 katika Hospitali ya Rufaa Kitete, baada ya kupelekwa na mwanaume nisiyemjua."
"Mwanaume huyo alipomfikisha hospitali, alilipa pesa ya awali hospitali na kumwachia mdogo wa marehemu elfu 40 ya dharula. Mdogo wa marehemu aliitwa na mwanaume baada ya dada yake kupata shida hiyo. Watu waliokuja nyumbani baada ya mazishi ni wafanyakazi wenzake tu kwa kadiri ya maelezo yao."
"Wakati tatizo linampata tayari mwanaume huyo alikuwa akiishi naye kwa siri, inasemekana ni mwanajeshi wa kambi ya Mabama Tabora, alimchukua bila ya mimi kuwa na taarifa. Nina wasiwasi kifo cha mwanangu si cha kawaida."
"Ninaomba kupaziwa sauti ili haki itendeke. Baba ninakuomba nina maumivu makali."
Izidory Petro Chinyo,
Mzazi.
20 Novemba 2024.