Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Kwema Wakuu,
Katika another episode ya digitali samala kwa watoto, welcome to my channel😂😂 vile najiona kama influencer wa maana
.
Kama mada inavyosema Wakuu, wengi tunadharau watoto hawajui mambo tunayoona ni 'makubwa' kwa umri wao na wengina naona tunaogopa tu kujua ukweli utakaotuonesha wanajua zaidi ya tunavyodhani na labda kwa namna nyingine tumefeli kama wazazi na walezi.
Sasa kama uko una mtoto kajaribu zoezi hili weekend na uje utuletee majibu ya nini umegundua kwa mtoto wako. Umekuwa ukimpa simu yako achezee au umemnunulia simu muulize apps anazopenda kutumia, muulize nini kinatrend kwenye mitandao ya kijamii, kuna ka mtandao ambako unaona si kazuri kwa mtoto toa ka scenario muulize kama alishawahi kukutana nayo, hata mauzui ya ngono ambayo umekuwa ukimkataza (au lah) muulize kwa lugha ambayo itailewa, una TV nyumbani muulize mbali na katuni anapenda kuangalia nini. Series gani inabamba sasa hivi (kulingana na aina ya kifurushi unachotumia), nk. Wale wenye watoto wa kiume wanapenda sana game na nyumbani zimepigwa marufuku, chombeza tu kirafiki, mtoto afunguke ujue huwa anatumia vipi muda wake.
Na wale wakoloni ambao bado mnaishi miaka 47, jumlisha wale wenye watoto wakike ambao mnasema wangu namzuia hiki mpaka afikishe chuo, au kwangu hakuna kuangalia TV ni kisomo tu, kwangu kuangalia TV ni masaa mawili tu tena JMosi pekee, fanya zoezi hili tafadhali uje utuambie umefahamu nini?
MUHIMU: Wakati mtoto anafunguka USIKUNJE SURA, yaani jilipue tu kuwa siku hiyo unataka kumjua ziadi mwanao kwenye upande mwingine. Smile na umfanye/mhimize afunguke zaidi.
Ukishapata picha mwanao anafahamu nini, isiwe ndio mwanzo wa kurudi kwenye ukoloni wako au kumzuia kwenye kila kitu, hii iwe mwanzo wa kumuongoza mwanao kwenye matumizi mazuri ya digitali na kujilinda kwa ujumla. Ajue kwa lolote litakalotokea wazazi/mzazi wangu atanilinda.
Hii isiwe kitu cha mara moja, fanya hivi mara kwa mara kuendelea kuweka ukaribu na mtoto na kutafuta njia za kumsadia kadri mambo yanavyojitokeza.
Tuko hapa nasubiri shuhuda wakati wengine wengine tunaendela kuchangia mada na kushea experiences.
Katika another episode ya digitali samala kwa watoto, welcome to my channel😂😂 vile najiona kama influencer wa maana
.Kama mada inavyosema Wakuu, wengi tunadharau watoto hawajui mambo tunayoona ni 'makubwa' kwa umri wao na wengina naona tunaogopa tu kujua ukweli utakaotuonesha wanajua zaidi ya tunavyodhani na labda kwa namna nyingine tumefeli kama wazazi na walezi.