Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Wengi tungependa kuishi na kulelewa na wazazi wetu waliotuzaa lakini maisha yana changamoto nyingi. Kuna wanaozaliwa na wazazi wanapoteza maisha, wengine ni matokeo ya kubakwa, wengine ni mimba za ujanani wakati wazazi wote hawana dira za maisha.
Wengi wetu pale unapomuelewa mtu na kuanza kumfikiria kwa maisha ya baadae ndipo unamueleza kuhusu watoto ulio nao. Maana hizi gym na make up siku hizi mama wa watoto wanne anaonekana bado kigori kabisa.
Shida inakuja kwa watoto kuanza kumkubali baba au mama mpya. Inawezekana ulishawapa utaratibu wa kuendesha maisha yao ya kila siku mfano mdogo tu ni nyama, ukirudi uji kuta imekwisha unatafuta mboga ya kesho, mama mpya anakuja na serikali mpya kuwa kilo ya nyama lazima ikate siku mbili.
Hakuna mzazi anayependa watoto wake wapate shida lakini na watoto waelewe mtu mzima kuishi bila mwenza ni changamoto. Wapeni ushirikiano. Juzi rafiki yangu ameitwa mke bandia mke halali alikua mama yetu. Sasa kama mama yenu ni mke halali yuko wapi sasa hivi?