Mzee Aboud Jumbe Mbona uko Kimya Sana ?

Mzee Aboud Jumbe Mbona uko Kimya Sana ?

Bramo

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2009
Posts
13,176
Reaction score
10,068
Wakuu JF Amani iwe Nanyi.

Tunapozungumzia katiba Mpya katika kipindi hiki ambacho Serikali 3 haziepukiki.
Binafsi nimekuwa nukijiuliza sana ni kwanini Mzee Aboud Jumbe Yuko Kimya sana.

Hii ni Seheme ya Wasifu wa Mzee Aboud Jumbe Kutoka Wikipedia

Mwinyi Aboud Jumbe (born 14 June 1920)[1] was a politician in Zanzibar. He held several positions, including the second president of Zanzibar, chairman of the Revolutionary Council, Vice-President of the Union, and the vice-chairman of the Chama Cha Mapinduzi (CCM) party.[2]

Jumbe served as president of Zanzibar from 11 April 1972 until 30 January 1984. He succeeded Abeid Karume as president, following Karume's assassination on April 7, 1972. He was initially elected by the Revolutionary Council as a part of the Afro-Shirazi Party (ASP). While he was in office, in 1977, the two ruling parties of Tanzania merged. In particular, the ASP and the Tanganyika African National Union (TANU), merged to create Tanzania's ruling party, the CCM.[3]

In 1979, Jumbe introduced the first post-revolution constitution of Zanzibar. This separated the powers of the Revolutionary Council and the House of Representatives. Furthermore, the new constitution established elections by universal suffrage, instead of being elected by the Revolutionary Council.[3]
Inasemekana kuwa hata wazo la kuunga TANU na ASP Lilikuwa ni la huyu Mzee.
Huyu Mzee inasemekana kuwa alisalitiwa na Maalim Seif pale alipokuja na wazo la Serikali 3.
Si Mpango wangu kujadili issue ya Maalim Seif, Lakini kwa wanaojua Siasa za Tanzania wanajua kuwa hata Maalim Seif Baada ya kupewa Mikoba ya Uwaziri Kiongozi, haikumchukua muda kuyaona na kuyashuhudia yale Mzee Jumbe alikuwa ameyaona, hii ilipelekea hata Maalim kuwekwa kizuizini na kuachiwa wakati almost nchi iko kwenye Mfumo wa vyama vingi na kujiunga na CUF kuendeleza Mapambano.
Sasa kwa kuwa Maalim anasimamia yale Mzee Jumbe aliyoyaona, hivi hatuoni kuwa ni wakati Muafaka sasa wa Mzee Jumbe kutoa Maoni yake.
Naandika post hii nikiwa na imani kuwa Mzee Jumbe yupo buheri wa Afya.

cc Barubaru , zanzibar huru, Mzee Mohamed Said , Bobwe
 
Last edited by a moderator:
Natoa changamoto kwa waandishi wetu.tafadhilini fanyeni juhudi mukamuone huyu mzee.
Jipangeni jopo kubwa mwende mukamsikilize muandae masuali ya kumuuliza ana mengi ya kusema.
Ni vyema kupata picha halisi ya historia kabla hajatutoka.
Hakika waandishi wa tanzania kuweni wabunifu nendeni kwa huyu mzee...mnalo jukumu la kujua upande wake wa habari
 
tatizo toka mwanzo msema kweli alisakamwa, historia bila kuandikwa upya bila upendeleo hakuna kitakacho kaa sawa. tazama kina lukuvi mara kikombe cha babu safi sasa udini wake kanisani inakera.
 
hawataruhusiwa kumuona maana yupo kizuizini tangu utawala wa nyerere.

Natoa changamoto kwa waandishi wetu.tafadhilini fanyeni juhudi mukamuone huyu mzee.
Jipangeni jopo kubwa mwende mukamsikilize muandae masuali ya kumuuliza ana mengi ya kusema.
Ni vyema kupata picha halisi ya historia kabla hajatutoka.
Hakika waandishi wa tanzania kuweni wabunifu nendeni kwa huyu mzee...mnalo jukumu la kujua upande wake wa habari
 
Muacheni Mzee wetu apumzike UKWELI wake umeendelea kumea na sasa matawi yake yanasambaa nchi nzima... soon tutaanza kuyala matunda yake inshaa'llah... Pole sana Mzee wetu, wamekutesa, wamekutilisha upofu, wamekupandikizia maradhi ya kila aina lakini kwa dua zako toba zako unazokazia na saumu za mara kwa mara zimekunusuru na madhila ya mafatani na sasa kazi yako inaangaza kama nuru ya matumaini kwa umma wa Kitanzania walionyanyaswa na kudhulumiwa haki zao mara baada ya uhuru wetu 1961...
 
Hivi wafungwa wanaruhusiwa kutoa maoni yao? Kama vp 2andamane kushinikiza asamehewe na maCCM.
 
Nijuavyo kuwa huyu Mzee ni bedridden huko Mjimwema.
 
JUMBE ni kielelezo kuwa ukweli hauwezi kufichwa chini ya Zulia kwa nyakati zote!YALIYOFICHIKA YATAFICHUKA TU HATA KAMA JUMBE HATOSEMA TENA LOLOTE
KUNA HANDBOOK INAITWA KWAHERI UKOLONI KWAHERI UHURU.NI BORA MKIWAHI MADUKANI MJISOMEEMAMBO YA ZNZ NA TANGANYIKA NA PEMBA NA UNGUJA YALIOTAFITIWA KISAYANSI!
 
Natoa changamoto kwa waandishi wetu.tafadhilini fanyeni juhudi mukamuone huyu mzee.
Jipangeni jopo kubwa mwende mukamsikilize muandae masuali ya kumuuliza ana mengi ya kusema.
Ni vyema kupata picha halisi ya historia kabla hajatutoka.
Hakika waandishi wa tanzania kuweni wabunifu nendeni kwa huyu mzee...mnalo jukumu la kujua upande wake wa
habari

Huyu mzee anakaribia miaka 100 (kazaliwa 1920) na kwa taarifa nilizonazo keshaanza kupoteza kumbukumbu na hayuko kizuizini kama wengine wanavyodai, kwa hiyo ni vyema watu wakasoma kitabu chake cha the Partnership tutapata kujua mbichi na mbivu humo, otherwise hivi sasa anahitaji dua za hatma nje.
 
tunakipataje hiko kitabu?
 
Tamaa ya kurithi urais toka kwa Julius ndo ili mcost huyu mzee.
 
Mzee jumbe hayuko kizuizini, Yuko Mjimwema Kigamboni, unaweza kwenda ila ni Mzee sana anaongea kama cassette inakula mkanda pia anawatambua watu wa familia yake kwa sauti! Anakiti cha matairi huwa wanatumia kumtoa nje na kumrudisha ndani.
 
Wakuu.
Hivi tunaposema yuko kizuizini tuna maana kuwa yuko Gerezan ama ?
Mimi sielewi kabisa aisee
 
Mzee jumbe hayuko kizuizini, Yuko Mjimwema Kigamboni, unaweza kwenda ila ni Mzee sana anaongea kama cassette inakula mkanda pia anawatambua watu wa familia yake kwa sauti! Anakiti cha matairi huwa wanatumia kumtoa nje na kumrudisha ndani.

Shukran Mkuu
 
Back
Top Bottom