Mzee Akilimali achafua hali ya hewa Jangwani amtuhumu Makamu Rais wa Yanga

Mzee Akilimali achafua hali ya hewa Jangwani amtuhumu Makamu Rais wa Yanga

Kama sio siasa wivu na visasi, MANJI apewe timu aimiliki, tofauti na hapo tutegemee kushuka daraja baada ya misimu miwili au mitatu
Ha ha ha! Masikini akipata, mat...hulia sijui nini! Kama simba haikushuka daraja miaka minne iliyopita basi sahau kuhusu Yanga! Yanga siku zote daima mbele nyuma mwiko! Tuombe Mungu atuweke hadi Mei mwakani!
 
Yafuatayo ni sehemu tu ya mazungumzo mafupi kati ya Nahodha wa Yanga SC Nadir Haroub ' Cannavaro wa Pemba ' na aliyekuwa Mwenyekiti na Mfadhili wa Klabu ya Yanga Yusuph Mehboob Manji baada ya kukutana ile juzi pale Kisutu Mahakamani

Nahodha Cannavaro: Shikamoo Tajiri Manji
Manji: Marahaba Cannavaro vipi mzima?

Nahodha Cannavaro: Mzima tu mdomoni Tajiri ila rohoni kuna masononeko ya kufa Mtu
Manji: Kulikoni tena Cannavaro?

Nahodha Cannavaro: Tajiri huwezi amini sasa ni mwezi wa Nne huu Wachezaji wa Yanga tuna ' njaa ' isiyo na mfano
Manji: Sasa Mimi unataka nifanyeje?

Nahodha Cannavaro: Tajiri tunaomba angalau basi utusaidie tu Hela kidogo kwani kiukweli tunaumbuka hapa mjini
Manji: Yaani Cannavaro kipindi chote nina matatizo si wana Yanga SC wote mlinisusa na leo ndiyo mmeibuka

Nahodha Cannavaro: Ni kweli Tajiri nakiri Kosa kwa niaba ya wenzangu kwani tulidanganywa na baadhi ya Wakubwa
Manji: Mmechelewa sana na hakuna Watu ninaowachukia sasa kama Yanga na Wewe nimekuheshimu tu

Nahodha Cannavaro: Kwahiyo Tajiri nikufuate baadae au?
Manji: Kuna unachonidai?

Nahodha Cannavaro: Njaa Tajiri Manji
Manji: Pambaneni na hali zenu na safari hii mtakula hadi Mende na Mijusi siwasaidii ng'o Wanafiki wakubwa nyie

Nahodha Cannavaro: Dah....sawa Tajiri Manji
Manji: Tena uwaambie na wana Yanga wenzio kuwa msipoteze muda nami na mniache tafadhali. Mtakoma mwaka huu.

OMBI / USHAURI

Jamani wana Yanga SC wenzangu kwa hali hii ya ' njaa ' kali iliyopo kwanini tusifumbe tu macho na twende kwa kupiga hata ' magoti ' Ofisini kwa Tajiri na Mfadhili wa Simba Mo Dewji ili aweze kutusaidia kwa Pesa na ikiwezekana basi na sisi pia tumpe Timu yetu kama ambavyo Simba sasa wanaelekea kumkabidhi Timu?

Nasubiri majibu yenu wana Yanga SC wenzangu kwani hii ' njaa ' naona kila sekunde, dakika, saa na siku inazidi tu Jangwani.

[emoji23][emoji23][emoji23]wewe jamaa ni mnafiki wa kiwango cha PhD
 
Mpira pesa, wachezaji hawawezi kucheza bila kulipwa, ndo tatizo la club zetu za kibongo kuwategemea watu, na club kutokuwa na chanzo cha mapato..
 
Wampe team huyo MZEE hata kwa msimu mmoja tuone.
 
Yule Mzee ' machachari ' wa Klabu ya Yanga Ibrahim Akilimali muda si mrefu akizungumza ' mubashara ' kupitia Kipindi cha Sports Headquarters cha Efm ameamua ' kufunguka ' na kutoa ' Siri ' ya Yanga SC kufanya vibaya kwa kusema kwamba Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Ndugu Clement Sanga ndiyo adui namba moja wa Yanga na anaihujumu Yanga.

Aidha Mzee Akilimali amefichua pia ' Siri ' nyingine kwamba ni kweli jana Wachezaji wa Yanga SC waligoma kutokana na ' njaa ' narudia tena ' njaa ' namalizia kwa kusisitiza ' njaa ' ambayo sasa imekomaa kama siyo kuota mizizi hapo Klabuni huku akiwaonea huruma Wachezaji kwa maisha magumu ambayo wanapitia sasa huku wengi wao wakishindia tu Mlo mmoja na wengine wakishindia tu maji.

Mwisho Mzee Akilimali alimlaumu sana Nahodha wa Yanga SC Beki Nadir Haroub ' Cannavaro wa Pemba ' kwamba na Yeye anatumika na Kaimu Mwenyekiti wa Yanga SC Ndugu Clement Sanga katika ' kuihujumu ' Timu yao. Mzee Akilimali amewataka wana Yanga SC wote duniani kusahau kuwa msimu huu Yanga SC itatetea Ubingwa wake huku akiitaka TFF kama wataona inafaa waipe mapema tu Kombe Klabu ya Simba kutokana na kwamba haoni Timu ya Kuizuia katika Kuchukua Ubingwa msimu huu kwa kusema Simba SC imesajili si tu vizuri bali ' Kisayansi ' zaidi kuliko wao Yanga SC ambao wamesajili ' Kiswahili Swahili ' au ki ' hovyo hovyo '.

Jamani wana Yanga SC wenzangu wote duniani huyu Mzee Akilimali siyo kwamba labda ana ' mahaba ' na Simba SC na pengine siyo mwenzetu huyu? Hivi Katiba yetu ya Yanga SC haina ' Kipengele ' cha Kumfukuza Mwanachama ' asiyeeleweka ' kama Mzee Akilimali? Jamani wana Yanga SC wenzangu popote mlipo haraka sana tuandamane ili huyu Mzee ' afukuzwe ' Yanga SC kwani tumeshamchosha.

Nawasilisha.

Jamani tuwe tunarizika na kuwapongeza viongozi na wachezaji wetu ubingwa Mara 3 mfululizo last season coming from back to ubingwa tuache tamaa za kipuuzi na maneno uasikiwa na maana
 
Porojo zoote hizi mwisho wa msimu mnakimbilia FIFA,this time nasikia fifa wamewaonya kuwatajataja hovyo.
 
Yule Mzee ' machachari ' wa Klabu ya Yanga Ibrahim Akilimali muda si mrefu akizungumza ' mubashara ' kupitia Kipindi cha Sports Headquarters cha Efm ameamua ' kufunguka ' na kutoa ' Siri ' ya Yanga SC kufanya vibaya kwa kusema kwamba Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Ndugu Clement Sanga ndiyo adui namba moja wa Yanga na anaihujumu Yanga.

Aidha Mzee Akilimali amefichua pia ' Siri ' nyingine kwamba ni kweli jana Wachezaji wa Yanga SC waligoma kutokana na ' njaa ' narudia tena ' njaa ' namalizia kwa kusisitiza ' njaa ' ambayo sasa imekomaa kama siyo kuota mizizi hapo Klabuni huku akiwaonea huruma Wachezaji kwa maisha magumu ambayo wanapitia sasa huku wengi wao wakishindia tu Mlo mmoja na wengine wakishindia tu maji.

Mwisho Mzee Akilimali alimlaumu sana Nahodha wa Yanga SC Beki Nadir Haroub ' Cannavaro wa Pemba ' kwamba na Yeye anatumika na Kaimu Mwenyekiti wa Yanga SC Ndugu Clement Sanga katika ' kuihujumu ' Timu yao. Mzee Akilimali amewataka wana Yanga SC wote duniani kusahau kuwa msimu huu Yanga SC itatetea Ubingwa wake huku akiitaka TFF kama wataona inafaa waipe mapema tu Kombe Klabu ya Simba kutokana na kwamba haoni Timu ya Kuizuia katika Kuchukua Ubingwa msimu huu kwa kusema Simba SC imesajili si tu vizuri bali ' Kisayansi ' zaidi kuliko wao Yanga SC ambao wamesajili ' Kiswahili Swahili ' au ki ' hovyo hovyo '.

Jamani wana Yanga SC wenzangu wote duniani huyu Mzee Akilimali siyo kwamba labda ana ' mahaba ' na Simba SC na pengine siyo mwenzetu huyu? Hivi Katiba yetu ya Yanga SC haina ' Kipengele ' cha Kumfukuza Mwanachama ' asiyeeleweka ' kama Mzee Akilimali? Jamani wana Yanga SC wenzangu popote mlipo haraka sana tuandamane ili huyu Mzee ' afukuzwe ' Yanga SC kwani tumeshamchosha.

Nawasilisha.
Kama kweli klabu inamatatizo hayo na uongozi pamoja na wanachama walikwisha liona hilo wakaamua kuikodisha[siyo kuuza] na mzee huyu huyu akapinga sasa analalamika nini?
Achangie fedha kama wazee wengine walivyokuwa wanafanya[Marhemu mzee Kondo Kipwata aliwahi kuweka nyumba yake rehani kwa ajili ya klabu na wala hakujitangaza] na aache kelele.
Ninavyosikia tatizo kubwa la bwana sanga ni kubana matumizi yasiyo yalazima hasa kipindi hiki kigumu na huyu mzee alizowea takrima na sasa amebuma. Hii yanga siyo ya mzee huyo wala hana hati miliki kwa klabu hiyo.
 
Huyu namshangaa sana wakitokea wawekezaji waichukue timu anatia figisufigisu fedha hamna bado analaumu haeleweki anachokiitaji shame on him?
 
Kuionyesha Yanga ina njaa juzi WACHEZAJI walishinda Mahakama ya Kisutu kumsubiri Yusuf Manji awape chochote
 
Back
Top Bottom