Mzee Akilimali: Yanga haiwezi kukodishwa kama masufuria

Mzee Akilimali: Yanga haiwezi kukodishwa kama masufuria

Mzee Akilimali amedai Yanga ni klabu kubwa na haiwezi kukodishwa kama masufuria ya kwenye shughuli kwa ajili ya kufaidisha mtu mmoja


===============
Habari Zaidi
===============

Siku kadhaa kabla ya kufanyika mkutano wa Yanga, Kamati ya Mwafaka ya Wazee wa Yanga imezungumza na waandishi wa habari kuhusu mfumo ambao mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji anataka autumie katika kuingia mkataba wa miaka 10 kuimiliki nembo ya klabu.

Katibu wa Kamati ya Mwafaka ya Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimalia amesema ambacho Manji anakifanya kinaweza kusababisha timu hiy ikaingia katika vurugu ambazo hazikuwepo kwa muda mrefu kwa sababu njia ambayo anatumia inawagawa wanachama na mashabiki kwa wengine kuutaka mfumo na wengine kuukataa.

“Hatutaki kurudi kule tulipokuwepo katika mgogoro wa miaka saba, mwaka 2003 ndiyo tukapata usuluhisho na kukubaliana kuwa litumike jina ambalo lilikubaliwa na waasisi wetu, tukakubaliana kuwa kuwe na Yanga SC na Yanga Cooperation,

“Yanga kampuni ilifishwa na kukawa na utaratibu kuwa kuwe na hisa, Yanga SC kuwe na hisa 51 na wanachama wawe na asilimia 49, na tulizunguka mikoa mingi ili kufuta mgogoro uliokuwepo na kuomba ridhaa ya wanachama wa klabu kukubali hisa,” alisema Akilimali na kuongeza.

“Tulipata mwenyekiti mpaka anatoka timu ilikuwa na Mil. 200, tukampata bwana Nchunga yeye akajiuzulu baada ya miaka miwili, tukamchagua Bwana Manji akaongoza kwa miaka miwili, kwasababu tu ya upenzi ikabidi tuikanyage katika akaongeza muda, ili tujipange na yeye ajipange ili tutafute kuongozi wa baada yake, na tukafikia hatua ya kumchagua kwa mara nyingine,

“Haijafika hata miezi nane imeibuka swala la deni la Bilioni 11 na laki sita, jambo ambalo limetushtusha sana wanayanga, limekuja tamko la mwenyekiti kuleta hoja kuwa akodishwe Yanga na lebo yake kwa muda wa miaka 10, kwasisi wote tunasema Yanga ni kubwa sana, Yanga haiwezi kukodishwa kama masufuria ya kwenda shughulini. Kupitia mimi na wazee wa kamati tumesema hatukubaliani na hilo”

Nae aliyekuwa Mwenyekiti wa Matawi ya Yanga, Mohammed Msumi amesema kutokana na Manji kuwa na mahitaji makubwa na klabu ni vyema akakaa pembeni na kuanzisha timu yake mwenyewe na kuacha Yanga iendeshwe na mfumo ambao umezoeleka.

“Kwanini anataka hili jambo haraka haraka na wakati alisema Yanga inajiendesha kwa hasara, mfanyaniashara gani anakaa sehemu ya aina hiyo, kama hawezi kufata utaratbu anaweza kuanzisha timu nyingine sio kuitaka yanga na kutumia mamlaka kwa mabavu ili tu aipate Yanga,” alisema Msumi.

Chanzo: Dewji Blog

Eti kamati ya mwafaka...kamati hii imetoka wapi kwenye katiba ya yanga.
Huyu mzee atakuwa kapigwa chini kwenye "benchi la ufundi"
ha haha
 
Labda nijibu swali kwa swali
Nitajie kiongozi wa Yanga kabla ya Manji ambaye amefanya kitu wewe unacho hisi unakikumbuka mpaka leo.

Ukifanikiwa kumtaja ntarudi, ukishindwa kumtaja maana yake hakuna kiongoz wa yanga alowagi fanya chochote


Umesahau kua sasa hivi deni la yanga ni bilion kumi na moja(11) wakati Madega anakabidhi ofisi timu haikua na deni sasa hivi inadaiwa bilioni kumi na moja. Na alisema akikabidhiwa timu itamchukua miaka minne kulipa deni.
 
Kabla ya maamuzi sahihi jipe muda sio kukurupuka msije mkamujuta na kutafuta mchawi tathmini kura wazo kwa umakini upande upi uko sawa
 
Yanga a.k.a vyura sio masifuria ya sherehe mkuu, bangachori aanzishe timu yake
Huyo mwenye njaa zake kwa nini yeye asianzishe timu yake. Wenye timu kama wameamua who cares?
Wamatopeni wanauza nyumba ili wakaishi guest house. Wenyewe kama wameamua nani ngulumbili wa kuzuia?
 
Timu inakodishwa kama wahayamalaya wa uwanja wa fisi
 
Kama Manji ana nia nzuri na Yanga bhax aisaidie timu bila kujikodishia, Haina haja ya kujikodishia timu baada kwa miaka kumi, Akiwa mwenyekiti kwa miaka kumi ni sawa lkn sio kujikodishia timu. Huyo muhindi alikuwa na plan zake cku nyingi, Cha kwanza kilikuwa ni kuwin mioyo ya wana Yanga hlfu kufanya na kukipata anachotaka kutoka Yanga(Maslahi yke binafsi)
 
Hao wazee waje kwenye mkutano tarehe 23 kama wana hoja .na huyu MZEE akilimali alishafukuzwa uanachama na sasa anatafuta nini sasa?

Ni nani aliyemfukuza uanachama mzee Akilimali????.....Pengine hamuijui historia ya YANGA...Klabu hii siyo ya kufukuzafukuza ovyo wanachama...wanachama ndio ambao hujiweka kando na siyo kufukuzwa....Halafu kwanini YANGA ikodishwe???? Huyo Manji ameshindwa nini kuitumia nembo au logo hiyo akiwa yeye ni Mwenyekiti????Ni kwanini anataka kampuni yake aliyoianzisha ndiyo itumie logo hiyo??? Kukodisha timu kuna faida gani??? Je, faida hizo haziwezi kupatikana bila kukodisha???
 
Manji amefanikisha timu kuwa mabingwa wa ligi kuu mara 3 ndani ya miaka mi 4, tumeshinda kombe la FA.
Tumefika robo fainali ya kombe la CAF afrika
Hatujafungwa na Simba kwa miaka miwili sasa.
At least na kipindi cha uongozi wake klabu imetulia hamna fujo fujo.
Manji anaweza kuwa ana matatizo yake ila huwezi sema hajafanya kitu, kafanya ila hajafanya kwa asilimia 100, na haja fanya kile ambacho wewe ulitaka afanye.
Hayo ni kweli na gharama ya ubingwa huo ni hayo mabilioni anayowadai!Unadhani kununua match mchezo?
 
Back
Top Bottom