Mzee Ayo afariki dunia baada ya kutapeliwa pesa mtandaoni. Umuhimu wa NIDA na alama za vidole kwenye usajili wa kadi za simu ni upi?

Mzee Ayo afariki dunia baada ya kutapeliwa pesa mtandaoni. Umuhimu wa NIDA na alama za vidole kwenye usajili wa kadi za simu ni upi?

Mkenda01

New Member
Joined
Dec 12, 2013
Posts
1
Reaction score
10
Habari wana JF

Wakati swala la kusajili kadi za simu kwa kitambulisho cha nida na alama za vidole unaingia nchini tulipewa umuhimu mbalimbali wa jambo ilo ikiwemo swala la usalama na kudhibiti utapeli kwa njia ya mtandao.

Nimeleta hoja hii kwani ni miaka sasa tangu swala la kujisajili kwa kutumia nida na alama za vidole uanze lakini bado tatizo la utapeli kwa njia ya mtandao umekuwa unaendelea kukua kwa kasi sana. Najiuliza mfumo huu wa usajili umekwama wapi kuwakamata matapeli awa ambao wanawaumiza baadhi ya watanzania na ata kusababisha umauti kwa wengine

Je hizo kadi za simu zinazotuma jumbe mbalimbali za utapeli zinasajiliwa kwa namna gani tofauti na hii iliyoelekezwa na serikali? Na kama zinasajiliwa kwa alama za vidole na nida kwanini watu awa wamekuwa hawakamatwi wakati utambulisho wao unafahamika.

Wapo wanaosema vinatumika vitambulisho vya wananchi wengine bila wao kujua, lakini kama ni kweli iko hivyo kwanini hii mitandao ya simu haiwajibishwi kwa kuwa wao wanawafahamu vijana wao waliowapa vibali vya kusajili mtaani. Kwani line inayosajiliwa mtaani haina taarifa za wakala aliemsajili?

Ninaomba kufahamu kwanini utaratibu huu wa usajili haujafanikiwa kwa kiwango kikubwa kutatua changamoto hii ya utapeli, lakini pia kushauri nini kifanyike.

 
USIJE UKASHANGAA LAINI ILIYO SAJILIWA KWA ALAMA ZAKO ZA VIDOLE INATUMIWA NA TAPELI MDA HUU

SASA UNAPO SEMA KWANINI WAHALIFU HAO HAWAKAMATWI KWA KUFUATA ALAMA ZA VIDOLE USIJE SHANGAA WAKIANZA KAMATA WATANZANIA WENGI AMBAO SIO WAHALIFU NDIO WATAONEKANA WAHALIFU UKIWEMO WEWE.

MAANA YANGU NI KWAMBA WANAO SAJILI LAINI WENGI WAO NDIO HAO MATAPELI AU WANAHUSIKA KUWAUZIA MATAPELI LAINI HIZO ZA UTAPELI.

UTANIULIZA LAINI WANAPATAJE WANAPO SAJILI LAINI UNAKUTA ANAKUAMBIA MTANDAO UNASUMBUA HEBU WEKA DOLE GUMBA TENA HAPO NDIPO WANAPO WAFOTOLESHA WATU LAINI NYINGI BILA WAO KUJUA

MWISHO KABISA MFUMO KWA SASA TAYARI UPO CORRUPTED

(NI MIMI NINAE INGOJA YERUSALEMU MPYA YA KRISTO YESU )
 
Back
Top Bottom