Mzee Ayo afariki dunia baada ya kutapeliwa pesa mtandaoni. Umuhimu wa NIDA na alama za vidole kwenye usajili wa kadi za simu ni upi?

Mzee Ayo afariki dunia baada ya kutapeliwa pesa mtandaoni. Umuhimu wa NIDA na alama za vidole kwenye usajili wa kadi za simu ni upi?

Tatizo linaanzia kwa wale wanaosajilia laini watu wengine na wale wanaosajiliwa laini wakipoteza simu hawawaambii wale waliowasajilia ili wakazifunge hizo laini matokeo yake hizo laini zinaangukia mikononi mwa matapeli na kuanza kutapeli watu,wito wangu kwa TCRA na makampuni ya simu waendelee kutoa elimu ili wananchi waone umuhimu wa kuripoti pale wanapopoteza simu ili laini zao zifungwe mara moja vinginevyo ikitokea laini imetumika kwenye uhalifu kama wa utapeli wahusika waliotumia vitambulisho vyao kusajili laini hizo wawajibike labda watu watatia akili.
 
Huu
Ametapeliwaje????
Maana sijafungua hiyo video

Ova
Huu utapeli nimewahi kukutana nao,jamaa wanakutumia meseji kuwa umepokea pesa kiasi kadhaa alafu wanakupigia uwarudishie.
 
Habari wana JF

Wakati swala la kusajili kadi za simu kwa kitambulisho cha nida na alama za vidole unaingia nchini tulipewa umuhimu mbalimbali wa jambo ilo ikiwemo swala la usalama na kudhibiti utapeli kwa njia ya mtandao.

Nimeleta hoja hii kwani ni miaka sasa tangu swala la kujisajili kwa kutumia nida na alama za vidole uanze lakini bado tatizo la utapeli kwa njia ya mtandao umekuwa unaendelea kukua kwa kasi sana. Najiuliza mfumo huu wa usajili umekwama wapi kuwakamata matapeli awa ambao wanawaumiza baadhi ya watanzania na ata kusababisha umauti kwa wengine

Je hizo kadi za simu zinazotuma jumbe mbalimbali za utapeli zinasajiliwa kwa namna gani tofauti na hii iliyoelekezwa na serikali? Na kama zinasajiliwa kwa alama za vidole na nida kwanini watu awa wamekuwa hawakamatwi wakati utambulisho wao unafahamika.

Wapo wanaosema vinatumika vitambulisho vya wananchi wengine bila wao kujua, lakini kama ni kweli iko hivyo kwanini hii mitandao ya simu haiwajibishwi kwa kuwa wao wanawafahamu vijana wao waliowapa vibali vya kusajili mtaani. Kwani line inayosajiliwa mtaani haina taarifa za wakala aliemsajili?

Ninaomba kufahamu kwanini utaratibu huu wa usajili haujafanikiwa kwa kiwango kikubwa kutatua changamoto hii ya utapeli, lakini pia kushauri nini kifanyike.

Uzembe huu unagusa watu watatu:

yeye marehemu kushindwa kutanzua trick ndogo sana ya ku confirm salio, mtoto wake wa kike kutomhoji kwa kina baba yake pamoja na mhudumu wa miamala ya pesa kutuma pesa bila kuhakiki account ya mteja.

Apumzike kwa amani.
 
Mfumo wa kusajili line kwa Tanzania bado ni mbovu sana.

1-Kwanza wanatakiwa wafute mtindo wa kusajili line mitaani,,

2-Watu wote waende makao makuu husika kwenye ofisi z mitandao ya simu.

3- ukisajili line lazima muhusika apigwe picha iwe kwenye record za mtandao husika.
Hivi ndivyo wafanyavyo wenzetu wanaojitambuwa.

Huo upuuzi wa kusajili line mara 2 au zaidi utakoma.
Pia ni rahisi kumjuwa tapeli kwa sura yake pindi atakapofanya utapeli.
 
USIJE UKASHANGAA LAINI ILIYO SAJILIWA KWA ALAMA ZAKO ZA VIDOLE INATUMIWA NA TAPELI MDA HUU

SASA UNAPO SEMA KWANINI WAHALIFU HAO HAWAKAMATWI KWA KUFUATA ALAMA ZA VIDOLE USIJE SHANGAA WAKIANZA KAMATA WATANZANIA WENGI AMBAO SIO WAHALIFU NDIO WATAONEKANA WAHALIFU UKIWEMO WEWE.

MAANA YANGU NI KWAMBA WANAO SAJILI LAINI WENGI WAO NDIO HAO MATAPELI AU WANAHUSIKA KUWAUZIA MATAPELI LAINI HIZO ZA UTAPELI.

UTANIULIZA LAINI WANAPATAJE WANAPO SAJILI LAINI UNAKUTA ANAKUAMBIA MTANDAO UNASUMBUA HEBU WEKA DOLE GUMBA TENA HAPO NDIPO WANAPO WAFOTOLESHA WATU LAINI NYINGI BILA WAO KUJUA

MWISHO KABISA MFUMO KWA SASA TAYARI UPO CORRUPTED

(NI MIMI NINAE INGOJA YERUSALEMU MPYA YA KRISTO YESU )
Mimi niliwahi kucheki NIDA yangu imesajili namba ngapi,nikakuta ina namba 7,wakati mimi natambua namba 4 tuu.
 
Hiyo msg mnashindwa kuigundua
Kama famba au ndy inakukuta akili ishachemka,mambo ya kupanic

Ova
Hapana mimi hawakunipata ila kwa kuwa nilikuwa na muda walituma meseji wakanipigia nikawa nawasiliana na jamaa akawa ananielekeza nimrudishie pesa Mteja ametuma kimakosa,na kwa kuwa nilimwambia nina balance ndogo akaniambia niende kwa Wakala nimpe hiyo namba atume pesa,nilirekodi mazungumzo yote nikawa nasikiliza nacheka tu mwenyewe.Ila ndio hivyo wakimpata asiyeshtukia wanampiga.Ila kama huyu Wakala angeomba hela kwa Mzee kabla kutuma angemuokoa sana Mzee, sema ndio hivyo naye akatuma tu.
 
Habari wana JF

Wakati swala la kusajili kadi za simu kwa kitambulisho cha nida na alama za vidole unaingia nchini tulipewa umuhimu mbalimbali wa jambo ilo ikiwemo swala la usalama na kudhibiti utapeli kwa njia ya mtandao.

Nimeleta hoja hii kwani ni miaka sasa tangu swala la kujisajili kwa kutumia nida na alama za vidole uanze lakini bado tatizo la utapeli kwa njia ya mtandao umekuwa unaendelea kukua kwa kasi sana. Najiuliza mfumo huu wa usajili umekwama wapi kuwakamata matapeli awa ambao wanawaumiza baadhi ya watanzania na ata kusababisha umauti kwa wengine

Je hizo kadi za simu zinazotuma jumbe mbalimbali za utapeli zinasajiliwa kwa namna gani tofauti na hii iliyoelekezwa na serikali? Na kama zinasajiliwa kwa alama za vidole na nida kwanini watu awa wamekuwa hawakamatwi wakati utambulisho wao unafahamika.

Wapo wanaosema vinatumika vitambulisho vya wananchi wengine bila wao kujua, lakini kama ni kweli iko hivyo kwanini hii mitandao ya simu haiwajibishwi kwa kuwa wao wanawafahamu vijana wao waliowapa vibali vya kusajili mtaani. Kwani line inayosajiliwa mtaani haina taarifa za wakala aliemsajili?

Ninaomba kufahamu kwanini utaratibu huu wa usajili haujafanikiwa kwa kiwango kikubwa kutatua changamoto hii ya utapeli, lakini pia kushauri nini kifanyike.

Tunadanganywa sana nchi mbona mm nimetumiwa nitumie kwa namba hii sasa hivi?na pia kila baada ya siku napata ujumbe huo.kwa kweli kifo cha mzee Ayo kimenisikitisha sana
 
Back
Top Bottom