TANZIA Mzee Beda Amuli, mbunifu na mchoraji wa majengo, likiwemo Soko la Kariakoo afariki dunia

Alikua anaishi Mbezi mwisho hapa stend mpya, ng'ambo ya Barabara pale kwenye fremu za maduka, ndipo kwa Bedda Amury, mara nyingi alikua anakaa pale anapata kilaji mzee wawatu taratiiibu. Ila amefia huko sinza kwenye nyumba yake nyingine.
Hapana, taarifa yako juu ya kufariki akiwa Sinza si za kweli. Mzee Beda Jonathan Amuli amefariki akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
 
Mkuu ni kweli, huyu Beda Amuli alikuwa ICON ya ujenzi wa nyumba na Architecture nchini.
Bahati mbaya wala hakuenziwa kwa umahiri wake.
Aliajiriwa kwa miaka mitano na kampuni ya kiisraeli kiitwa ZEVET Achitects, kabla ya kuanzisha kampuniyake ya BJ Amuli Architects.
Kwa sisi tuliosoma uhandisi miaka mingi kidogo, huyu alikuwa akifahamika sana na wanafunzi wa ujenzi.
Bahati mbaya vijana wa sasa wengi hawamjui.
Alimaliza degree yake ya Archtecture mwaka 1964, Israel.
Kwa hiyo unaweza kukisia umri wake.
 
Alikua anaishi Mbezi mwisho hapa stend mpya, ng'ambo ya Barabara pale kwenye fremu za maduka, ndipo kwa Bedda Amury, mara nyingi alikua anakaa pale anapata kilaji mzee wawatu taratiiibu. Ila amefia huko sinza kwenye nyumba yake nyingine.
Jina sahihi la marehemu ni "Beda Jonathan Amuli".
 
Tulikutana na mwanae Stiv mjanja mjanja sana
Ulivyokutana nae tu huyo stivu (Steve) ukajua mjanja mjanja, eti?? Usipende kumchafulia mtu jina pasipo kumjua undani wake, your point is irrelevant.
 
Unategemea robot za Lumumba zikuelewe?
 
Kwa Sisis wa Zamzni tunamfahamu saana kwani ndio watu/ wasomi wa mwanzo waliopractice ki-private. iLA NATUARLLY ALIKUWA MTU HUMBLE SANA ASIYEPENDAA MEDIA NADHANI NDIO MAANA alikuwa hajulikani saaana wengine tunaijua moaka nyimba yake Mororgoror Road- maeneo ya Kibaha.
All in all ni vema historia engefahamika ( kwa kasi hii) kwa muda mrufu. Kwa tunaomfahamu likitazwa tu Soko La Kariakoo is equal to Beda Amuli ( R.I.P). Na kumbe kuna mengi aliyoyafanya pamoja na Kilimanjaro hotel labda tu nbahati mbya alikuwa chini ya Kampuni. Aidha alihamasisha watu wa kwao wasome na kuanzasha Trust Fund.
 
Ndio yupi kati ya hao wawili? Huyo ndio alitakiwa apewe kazi ta kuchora terminal III ya airport. Sio tule tuvichuguu tulitojengwa pale...

Terminal three inatia aibu sana, unaweza kifukiri ni ma godown za Azam pale opposite na TAZARA!!

Tazara Railway station pamoja na kujengwa mwanzoni mwa miaka ya sabini bado ina mvuto zaidi ya terminal three!
 
Kingine nachofahamu Masasi ana nyumba nyingi zilizojengwa kama kota kwenye eneo moja. Ni nyumba zenye muenekano mzuri hata kwa wakati huu japo zimejengwa miaka ya 90 ,halafu alikuwa anamiliki Range Rover na ndilo lilikuwa pekee kule Masasi, pia alikuwa mtu wa karibu na Rais Mstaafu Mkapa Mwisho alikuwa Msomi ambaye hakujipendekeza kwa Viongozi ili apewe madaraka japo alikuwa na ukaribu nao.
 
Inawezekana hata ile Nkrumah hall ya UDSM pia alihusika huyu. Maana naskia walijenga waisrael sasa unaweza kuta ndo hiyo hiyo kampuni aliyekuwamo
Architect B.J. Amuli alipata Elimu yake ya Architecture nchini Israel kabla ya kufungua firm yake ya B.J. Amuli alifanyakazi kama partner wa kampuni ikiitwa Zevet in early 70s
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…