Boniphace Kichonge
JF-Expert Member
- Jul 31, 2017
- 1,605
- 1,957
Wadau.
Leo Novemba 12,2019 Mzee Wetu na Rais Mstaafu Wa Awamu Ya Tatu Benjamin Mkapa Anatimiza Miaka 81 ya Kuzaliwa.
Tukio Hilo linaambatana na sherehe Mubashara muda Huu wa Uzinduzi wa Kitabu Chake Cha "My Life, My Purpose"
Hongera Sana Mzee Wetu.
----
Benjamin William Mkapa is a Tanzanian politician who was the third President of Tanzania, in office from 1995 to 2005. He was also Chairman of the Revolutionary State Political Party.
Born: November 12, 1938 (age 81 years), Ndanda
Presidential term: November 23, 1995 – December 21, 2005
Spouse: Anna Mkapa
Previous office: President of Tanzania (1995–2005)
Education: Kenyatta University, Main Campus, Makerere University, Columbia University, Pugu Secondary School
Books: The Mkapa Years: Collected Speeches
Baba yangu alinitamkia angelipendelea ningekuwa Padri, Daktari na ikishindikana uwe Mwalimu, badala yake nimekuwa Rais wa Tanzania kwa miaka 10, kitu ambacho hakuwahi hata kukiota.
Nimepata bahati ya kufanya kazi na Mwalimu Nyerere kwa muda mrefu, na bahati hii imenijenga kwenye misimamo yangu mbalimbali kuhusiana na uongozi. Katika kitabu changu nimetumia sura nzima kumuelezea Mwalimu Nyerere.
Kwenye kitabu nimemuelezea Mwalimu kwa mtazamo wangu na alivyokuwa, na hilo limenipa faraja sana na nimefurahi Mwalimu kuwa 'mentor' wangu
Mwalimu ametutoka miongo miwili iliyopita lakini falsafa, mitazamo na mawazo yake bado yapo, tuendelee kuyahuisha mawazo na falsafa zake"
Kitabu changu kitachangia kuboresha historia ya nchi hii kama nilivyolezea kwa mawazo yangu, pia yatachagiza kujiamini kwa wanaotafuta kuwa Viongozi wa baadae
Kujitegemea ni muhimu sana niruhusu kukupongeza Rais Magufuli kwa juhudi zako,fikra za kutegemea watu wengine waje kutuletea maendeleo ni fikra duni, haimaanishi tusithamini au tusiombe ila tuombe katika jambo ambalo tumelianza.
Kuna baadhi ya matukio najua ni magumu, sikutaka kuyahadithia lakini kama kiongozi najua anajengwa na mambo chanya na hasi, najua kama binadamu wakati mwingine tunafanya makosa ili viongozi wa sasa wajifunze.
Ni matumaini yangu hichi kitabu kitazua mjadala kutokana na matukio ambayo nimeyaeleza kwa sasa, mijadala kama hii itajenga ujasiri kwa viongozi wa sasa.
Zaidi soma....
Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa ambaye leo ndio siku yake ya Kuzaliwa na kufikisha umri wa miaka 81 alitoa shukurani kwa wale wote waliomuunga mkono katika kutayarisha kitabu hicho huku akimuelezea Rais Julius Kambarage Nyerere kwa jinsi alivyojifunza mambo mengi kutoka kwake.
Alieleza kuwa suala la kujitegemea ni moja ya mada aliyoiandika katika kitabu chake hicho na kumpongeza Rais Magufuli kwa kulipa kipaumbele suala hilo huku akieleza kuwa kitabu hicho kitampa fursa ya kutoa shukurani kwa wale wote aliofanya kazi nao sambamba na kueleza ukombozi wa bara la Afrika.
Alieleza kuwa katika kitabu chake hicho amemuelezea Mwalimu Nyerere kwa mtazamo wake kama anavyomjua jambo ambalo limempa faraja kubwa sana. Na kueleza kuwa kitabu hicho kitawasaidia wanafunzi na viongozi pamoja na vizazi vijavyo.
Mapema Profesa Joseph Semboja Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi alitoa maelezo mafupi ya Mradi wa Tawasifu na kueleza kuwa taasisi yake iliyoanzishwa mwaka 2010 ndio iliyokuwa na jukumu la kutayarisha kitabu hicho na kumuunga mkono.
Alieleza kuwa hivi karibuni Taasisi hiyo itatoa kitabu cha Maisha ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi na kuongeza kuwa viongozi wengi wakiwemo wa nchi za Magharibi wamekuwa na utamaduni wa kuandika vitabu vya historia ya maisha yao na kutoa shukurani kwa viongozi hao ambao hufanya hivyo na watu kupata kuvisoma na kuwasaidia
Kwa bahati mbaya Profesa Semboja alieleza kuwa viongozi wengi wa Bara la Afrika hawapati nafasi ya kuandika vitabu vyao kutokana na mazingira yao na badala yake hujifunza maandishi kutoka kwa nchi nyengine wanazoandika vitabu kama hivyo.
Alieleza kuwa historia ya kiongozi katika bara la Afrika si historia yake binafsi bali ni historia ya nchi nzima na kueleza kuwa Mzee Mkapa ameandika historia ya nchi na sio historia yake binafsi na ndio maana uzinduzi wake umejumuisha makundi mbali mbali na tukio hilo si la kifamilia bali ni la Kitaifa.
Aliongeza kuwa mwaka 2016 mchakato wa kuandika kitabu hicho ulianza na kutoa shukurani kwa watu walioshiriki kwa namna moja ama nyengine kufanikisha kitabu hicho..
Kampuni ya Uchapishaji ya Mkuki na Nyota kimechapisha kitabu hicho ambapo jumla ya TZS Milioni 230 sawa na Dola za Kimarekani laki Moja zimetumika ambapo gharama hizo sio kubwa ikilinganishwa na gharama za vitabu vinavyochapishwa na viongozi wengine katika nchi nyingi duniani wakiwemo viongozi wastaafu wa Marekani.
Alieleza kuwa kitabu hicho kinauzwa kwa bei nafuu na kinapatikana sehemu mbali mbali Hapa Tanzania ikiwemo Jijini Dar-es-Salaam, Zanzibar, Mwanza, Dodoma na sehemu nyenginezo ikiwa ni pamoja na kwenye mitandao.
Nae Profesa Rwekaza Mukandala Mgoda wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alitoa uchambuzi wa Kitabu hicho cha Rais Mkapa ambacho kina Sura 16 na kurasa 320 pamoja na utangulizi uliotayarishwa na Rais mstaafu wa Msumbiji Rais Chisano.

HOTUBA KWA UFUPI WAKATI MZEE MKAPA AKIZINDUA KITABU CHAKE