Mzee Butiku, kazi yenu imekwisha kwa mujibu wa sheria tuachie wananchi wenyewe tufanye maamuzi yetu

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,536
Hivi karibuni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amesema hatua ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kusogeza mbele tarehe ya Kura ya Maoni ya Katiba inayopendekezwa, iwe mwanzo wa kutafakari na ikiwezekana kurejesha mambo ya msingi yaliyoondolewa katika Rasimu ya Pili ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Bwana Butiko ameyasema hayo baada Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alitangaza kusogezwa mbele kwa mchakato huo wa kura ya maoni.

Butiku aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya Jaji Joseph Warioba, alisema kuahirishwa kwa upigaji Kura ya Maoni ni nafasi pekee kwa NEC kujipanga upya na kuhakikisha wananchi wanaandikishwa kwa kiwango kikubwa katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Alisema pia ni wakati mwafaka kuwapo kwa majadiliano ya kina ili kuangalia nini kinatakiwa kirudishwe kutoka katika vile vilivyoenguliwa kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba kama itawezekana.

Maswali yangu kwa Butiku wanataka kutuamisha kuwa kila walichoandika katika rasimu ya pili ya katiba ndicho sahihi kwa watanzania na hazikustahili kuondolewa?Kama rasimu ya kina warioba haikustahili kuongezwa neon au kupunguzwa neno kwani warioba na tume yake waliupeleka bungeni na badala yake ungeletwa kwetu wananchi tukafanya maamuzi?

Mzee wangu Butiko kwanini kila sku mmekuwa nyie tu wa taasisi ya mwalimu ndio mnaleta hayo mashiniko hali ya kuwa katika tume hamkuwa peke yenu? Au mlikuwa mmebeba ajenda nyingine nyuma ya pazia ambayo watanzania hatuijui ndio maana mmekuwa manalalama kila leo wakati wenzanu wametulia.

Mzee wangu Butiku kazi yenu ilikuwa ni kukusanya maoni baada ya hapo kuyapeleka katika ngazi iliyofuta ambalo ni bunge na baada ya bunge sasa ni zamu yetu wananchi kwa mujimu ya sheria na sasa mtuache tufanye maamuzi yetu wenyewe sisi wananchi
 
Kalime tu kiteto!! Haya mambo n mazito kwako!!..

Nikukumbushe tu, Nyerere aling'atuka mwaka 1985 lakini mpaka anakufa hakuacha kukosoa pale palipobidi!..

Kwa hiyo usimshangae Butiku,, yuko sahihi!!
 
Hakuna wenye hati miliki ya nchi hii wewe ni nani haswa mpaka wengine wakose haki??
 
kuna kundi hapa Tanzania, linadhani hii ni nchi yao pekee yao, na kila wanachosema wananchi hakina maana ila wanachosema wao ndicho kizuri hata kama ni kibovu. Na ni hao hao wanajiita wazalendo wakati wanaila nchi. Kumbuka Radar, richmond, meremeta, escrow, EPA nk. N akwenye katiba pendekezwa wameweka kipengele cha kutofirisiwa mali na serikali kwa sababu wanajua madudu waliyofanya hivyo wamejiwekea kinga ya kikatiba hata kama ni wezi katiba itawalinda. Hawaoni hata aibu wanawashambulia hadharani walio upande wa wananchi, very sad
 
We mshamba Wa kiteto acha shutuma zisizo na maana soma kazi za tum
e kwanza
 
.....
Mzee wangu Butiku kazi yenu ilikuwa ni kukusanya maoni baada ya hapo kuyapeleka katika ngazi iliyofuta ambalo ni bunge na baada ya bunge sasa ni zamu yetu wananchi kwa mujimu ya sheria na sasa mtuache tufanye maamuzi yetu wenyewe sisi wananchi
Hivi Mzee Butiku na wajumbe wengine wa iliyokuwa Tume ya kuratibu maoni ya Katiba Tanzania, kuvunjwa kwa Tume yao/kumaliza kazi kwa tume yao kunawaondelea haki ya kuwa wananchi wa Tanzania hivyo kuwa na haki ya kutoa maoni juu ya katiba pendekezwa...?

Kwa kumbukumbu nilizonazo, Tume yao ilikuwa inakusanya na naratibu maoni. Kuna uwezekano hawakupata furusa ya kutoa maoni na sasa wanayatoa na kutoa ufafanuzi wa yale maoni yaliyoratibiwa. Maana inasemekana kunaupotoshwaji wa maoni ya wananchi wao(Mzee Butiku na wenzake) walivyokuwa wameyaratibu.

Kwa maelezo hayo hapo juu. Nadhani si busara kuwazuia wajumbe wa Tume kuzungumzia katiba Pendekezwa.

Sasa nafasi kwako kutoa hoja nyingine.
 
Wewe bhana hao kazi yao ilishapita wawaachie wengine wafanye kazi zilizobaki, kama hujui hao ndo waanzilishi wa vurugu zote hizi kuhusu katiba hii inayopendekezwa, cjui wanataka nini aseee.
 
Butiku angetuambia hayo anayoyata yaingie kwenye katiba pendekezwa kwa sheria ipi?
 
Butiku angetuambia hayo anayoyata yaingie kwenye katiba pendekezwa kwa sheria ipi?
Sawa sawa kabisaa, yani hawa watu ni ving'ang'anizi asee cjawah ona, kazi walishapewa wamefanya wamemaliza sasa cjui kwanini wanasumbua sumhua hapa nchini.
 
Mleta mada umetumwa na Nina wasiwasi na kilichoko kichwani mwako kama sio mavi Basi ni tope maana unasahau kuwa mzee Butiku nae ni mtanzania ana haki ya kutoa mawazo yake mbele ya jamii
 
Tutajie wajumbe wengine wa Tume ya Warioba ambao si wa taasisi ya mwalimu Nyerere, ili tuone kama wao hawalalamiki.
Pili Tume ya Warioba ndiyo ilipita nchi nzima kukusanya maoni ya wananchi, hivyo maoni waliyoyakusanaya wanapoona yametupwa, wana haki ya kutujulisha, maana mimi niliyeko Nansio siwezi kujua aliyeko Kilambo alisema nini, lakini wao wanajua kuwa sote tulisema jambo fulani - acha watutetee.
Kwenye Bunge maalum la katiba ni mbunge gani aliyekwenda kuwakilisha maoni ya hao aliodaiwa kuwawakilisha. Nilimsikia mbunge wa Karagwe akisema ametumwa na wananchi tena wa mkoa mzima wa kagera, lakini alipobanwa humu ndani atoe maelezo ya wapi, na lini alikutana na wanachi na kuwauliza hayo aliyoyasema, alishindwa kujibu. Na waina yake wako wengi tu,
 
Usitusemee bwana mawazo yetu mbona yamo mengi tu mi mwenyewe nimesoma sura zote 19.
Hata kama likiachwa moja tu, unapaswa katiba uikatae mpaka ujiridhishe kwa nini limeondolewa. Kama yako machache hayamo, na yangu machache hayamo na mtu mwingine machache hayamo - katiba inafaa vipi?
Labda nikuulize swali moja tu - wewe unaona ni sawa kwa katiba kuweka utaratibu wa kuweza kumuondoa rais wa nchi madarakani kabla ya muda wake kuisha, lakini ikakaa kimya juu ya kumuondoa mbunge asiyetekeleza wajibu wake?
 
Uwongo dhambi ndugu,acha kupotosha umma
 
Chambua - lipi la uongo?
Ulichoongea hapo juu naona malengo yako ni kuweka mijdala isiyokuwa na maana humu, hao viongozi wa tume walishafanya yao na yamepita, sasahv ni zamo yako kuisoma na kuipigia kura katiba inayopendekezwa, kuendelea kuwatajataja humu mnaonekana kama mmetumwa na hao wajumbe ama mna ajenda zenu binafsi ambazo na uhakika kamwe hamtafanikiwa, kwa maana hii katiba itapita kwa kishindo kwa kura zenu nyingi za Ndiyo ikiwemo na yangu na yako pia.
 
Jitokeze kujiandikisha ili uweze kupiga kura ya ndio kwa katiba inayopendekezwa wakati utakapofika,katiba inayopendekezwa kwa maendeleo endelevu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…