Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mzee Joseph Butiku atoa ushauri wake sakata la Uwekezaji Bandari " Watanzania hawajaridhika na jambo hili,tulisahihishe ama tuliache kabisa"
----
Natoa shukrani kwa Rais wetu Dkt. Suluhu Samia kwa mambo mawili, kwanza kwa kuruhusu Watanzania kuzungumza, Watanzania tulikuwa na aibu ya kuzungumza lakini tangu Rais Samia aingie ametutaka tuzungumze, na tuzungumze waziwazi, ukweli na yote tuliyonayo moyoni
Hili jambo la bandari limeshakwenda serikalini na bungeni, raia tukaulizwa maswali kidogo na tukajibu. Baada ya hapo jambo hili la bandari lilirudi bungeni na kupitishwa na Bunge. Kwa mujibu wa utaratibu wa kikatiba, limeshapitishwa na hivyo ni la kutekeleza. Hivyo sasa wanaposema tuzungumze, tuzungumze kitu gani?
Ninaamini hoja zilizotolewa kuhusu bandari, serikali imezifuatilia. Kwa maoni yangu katika jambo hili (la bandari) ni kwamba Watanzania bado wana uoga, wasiwasi na hawana hakika kama maamuzi yaliyofanywa na serikali ni kwa faida ya nchi yao. Na sauti hiyo unaisikia nyakati zote, lakini ukitazama mitandao na ukisikiliza watu wakisema katika majukwaa mbalimbali ni kama Watanzania wanasema hatujardhika
Ukiniuliza kuhusu option ya serikali kwamba inaweza kuachana na jambo hili (la bandari), jibu langu ni ndio. Kama kuna makosa sehemu fulani fulani, kusahihisha huwa kuna gharama, hivyo serikali ikubali na kama Taifa tukubali kuwa gharama ya kusahihisha ni kubwa
Uamuzi wa kuendelea na mazungumzo haya (ya bandari) mimi haunipendezi na unaonekana unatugawa, na sijawahi kuona jambo kama hili ambalo watu wanazungumza kwa hisia kali wengine waziwazi na wengine chini chini, hata tunaodhani wamekubali pengine hawakukubali. Na tusiruhusu uamuzi wowote ukatuondolea sifa yetu ya msingi ambayo ni umoja wa Taifa hili
Wenzetu walioomba kushirikiana na sisi (serikali ya Dubai kupitia kampuni ya DP WORLD) isikilize maoni ya Watanzania na tusaidiane namna ya kuboresha maamuzi ya kutazama jambo hili (la bandari) au kuachana nalo. Na si vibaya kwa taifa letu kutazama upya jambo la bandari
Ukitoa hoja kuwa huyu mwekezaji ana meli 100 au ana utajiri mkubwa hiyo sio hoja, hoja ni kwanini uruhuhusu jambo hili (la bandari) litokee, na pia hoja ni kwamba umewashirikishaje unaowaongoza waelewe na tatu je umejiridhisha wamelielewa, na kama wamelielewa wafanye nini
Hakuna mtu anayeweza kuuza Tanzania bali mtu anaweza kufanya vitendo vya kukidhalilisha akidhani anaiuza Tanzania na hata hilo suala la uwekezaji wa bandari sio kuuza Tanzania.
Wawekezaji hata hawa wanaweka na kisha na wao wanachukua, dunia ya leo ni nipe nikupe lakini yako maeneo mengine ukifanya nipe nikupe inaleta shida ni kama mtu anagusa chumbani kwako. Bandari ni mali yetu kubwa mno ndio maana sisi inatupa shida.
Jambo