TANZIA Mzee Chrisant Majiyatanga Mzindakaya Afariki dunia

RIP Mzindakaya...nguli wa siasa za TAnzania zenye figisu na fitina, uzandiki, ujinga, 99.7%

Wabunge vijana akina Makamba jr. Kigwangala, Nape, Ridhiwan, nk kuna lolote la kujifunza kutoka kwa wanasiasa aina ya marehemu? hebu jiulizeni mtakumbukwa kwa yapi mliyoyatenda kwa Watanzania?

Ewe mtanzania bila kujali kama wewe ni mwanasiasa, mkulima, mvuvi, nk jiulize unakufa leo utakumbukwa ya lipi? idadi ya michepuko?
 
Pole sana ndugu yangu/ mshikaji wangu Paul,najua ni kipindi kigumu sana ila mungu akupe ujasiri na moyo wenye subra
RIP Mzee wangu
 
hivi huyu marehemu fisadi Dr yake ilikuwa ya nini na aliipatia wapi?

Huyu Mzee alisoma Mpaka darasa la nne enzi hizo na akawa ameajiriwa kama bus conductor kwa muda mrefu baada ya hapo ndio akaingia kwenye siasa. Kwenye siasa alikuwa mjanja mjanja sana na kujipendekeza kwa viongozi wakuu na pia kutumika Bungeni kuibua shutuma nyingi za mawaziri waliokuwa si msaada kwa mambo yake.

Katika uhai wake aliwahi kuwa naibu Waziri wa Viwanda wakati huo Mzee Msuya akiwa Waziri mkuu na pia aliwahi kuwa RC wa Mkoa wa Kigoma. Kuhusu huo udaktari wake, ni wa heshima aliopata kiujanja ujanja kutoka chuo kimoja cha kimagumashi huko Marekani lakini hakuwahi hata siku moja kukaa kwenye lecture room!!
 
duuuh, kumbe Nyerere nae alikuwa haheshimu kura za wananchi wala mahakama...

Mzindakaya kacheza faulo akanyang’anywa ubunge na mahakama, Nyerere akamwingiza bungeni kwa teuzi... so much for Baba wa Taifa

Spika Ndugai nae kadanganya bunge kwamba Mzee kapiga 45 years non- stop, wakati kumbe alikaa benchi 1981 mpaka 1982...
 
RIP Mzindakaya. Pole kwa wafiwa
 
Mkuu wewe bado unaamini yatokayo katika kinywa cha Jobo? Ameshafahamisha umma kuwa "huwa anasinzia akiwemo... lakini huwa hayupo huku akiwepo!!"
 
Mkuu wewe bado unaamini yatokayo katika kinywa cha Jobo? Ameshafahamisha umma kuwa "huwa anasinzia akiwemo... lakini huwa hayupo huku akiwepo!!"
daaaah.... jamaa muongo sana

Spika anakuaje hana records za wabunge waliofutwa ubunge na mahakama kwa kucheza rafu ?

tena alikuwa anasoma makaratasi anasema itakuwa vigumu kuvunja rekodi ya miaka 45 ya mbunge Mzindakaya.....

ni aibu kwa bunge na Taifa inapotokea Jamiiforums wana records za bunge ambazo Spika hana!
 
APUMZIKE KWA AMANI MZEE WETU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…